Monday, September 16, 2013

JINSI MBEYA CITY ILIVYOWAKIMBIZA MCHAKAMCHAKA YANGA NA KUTOKA NAYO SARE YA 1 - 1


Mashabiki wa timu ya Mbeya City wakiishangilia timu yao
Mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo akiingia uwanjani
RPC Mbeya kamanda Diwani akionyesha ishara ya ushindi huku akiwa ametinga jezi ya Mbeya city
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo akionesha fedha taslimu sh. milioni mbili ambazo aliahidi kuizawadia timu ya Mbeya City iwapo ingeshinda mchezo huo, hata hivyo alitoa sh. milioni moja baada ya timu hiyo kutoka sare
Meneja wa Uwanja wa Sokoine Modestus Mwaruka akiwa na mayai matatu yaliyochorwa chorwa ambayo alidai kuwa ameyakuta katikati ya uwanja
Mkuu wa mkoa Mbeya Abasi Kandoro akienda kukagua timu 
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa Mbeya City, uwanja wa Sokoine Mbeya.
Timu ya Mbeya City
Timu ya Yanga
Mambo yameshaanza
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo akiwa katikati ya mashabiki wa Mbeya City wakishangilia timu yao
Meneja Mahusiano ya  wa Vodacom Salum Mwalimu wapili toka kushoto  akiwa na wenzake wa vodaco wakifuatilia kwa makini mechi kati ya Mbeya City na Yanga
Hawa dogo wanataka kuniaharibia kazi kocha wa yanga
 Basi la Yanga baada ya kupasuliwa na chupa katika kioo cha kulia mwa dereva kama inavyoonekana (Tundu kulia dirishani)
Dereva wa basi la yanga alijeruhiwa mkono wake wa kulia
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akiongea na waandishi wa habari mara baada ya mpira kwisha
Mara baada ya mecho kwisha wachezaji wakipongezana
Wachezaji wa yanga hawaamini kilichotokea 
Kocha wa Timu ya Yanga akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mechi kati ya timu yake na Mbeya City timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1. Picha na Mbeya yetu

No comments: