Beki wa timu ya Kirimanjaro Jamens
Geofrey (katikati) akiwatoka wachezaji wa
mbeya Yusuf Honroli (kushoto) na
Jackson Mwaibambe katika mechi ya fainali za Copa Coca-Cola Taifa kwenye
Uwanja wa Karume leo. Kilimanjaro walishinda 1-0.
Mshambuliaji wa timu ya
Kilimanjaro Selemani Mwalimu akiwania mpira na mshambuliaji wa Mbeya Hamfrey
Nyeo katika mechi ya fainali za Copa
Coca-Cola Taifa kwenye Uwanja wa Karume leo. Kilimanjaro walishinda 1-0.
Beki wa timu ya Mbeya Emmanuel
Ntindi (kulia) akipiga hesabu za kumtoka mchezaji wa Kilimanjaro James Geofrey katika mechi ya
fainali za Copa Coca-Cola Taifa kwenye Uwanja wa Karume leo. Kilimanjaro
walishinda 1-0.
Mshambuliaji wa timu
Mbeya Yusuf Honroli (kushoto) akimtoka beki wa Kilimanjaro Simon
Soka katika mechi ya fainali za Copa
Coca-Cola Taifa kwenye Uwanja wa Karume leo. Kilimanjaro walishinda 1-0.
Kiungo wa timu ya Mbeya Emmanuel Ernest ( katikati)
akitoa pasi huku walinzi wa Kilimanjaro Bernld Temba (kulia) na James Geofrey wakijiandaa kumzuia katika
mechi ya fainali za Copa Coca-Cola Taifa kwenye Uwanja wa Karume leo.
Kilimanjaro walishinda 1-0.
Mshambuliaji wa timu ya Mbeya,Yusuf Honroli (kushoto) akiwania mpira
na mabeki wa Kilimanjaro,Abidal Ramadhani (kulia) na Simon Soka katika mashindano ya Copa Cocacola kwenye
Uwanja wa Karume
Timu ya Copa Coca-Cola ikiwa uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kukwea pipa kuelekea
Afrika Kusini kwenye kambi ya mafunzo ya soka yakishirikisha timu za vijana
kutoka barani Afrika. Anayehojiwa ni Afisa Habari wa Coca Cola Tanzania Gerald Ndalahwa
Timu ya Arusha imeigaragaza timu ya Kagera 3-0 katika mchezo wa fainali za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 15 za Copa Coca-Cola 2013 katika uwanja
wa Tanganyika packers , Kawe jijini Dar es Salaam . Mpaka wanaenda mapumziko kagera walikua
wanaongoza 2-0
Arusha walionyesha kuwazidi wapinzani wao
kila idara ,kwa kucheza kandanda safi na kupata goli la kwanza katika dakika ya
pili kupitia kwa Mohamed Said ambaye alikuwa mwiba katika ngome ya Kagera. Goli
la pili lilipachikwa na mshambulia hatari Bakari Athanas katika dakika ya 27.
Katika kipindi cha pili Kagera walifanya
mashambulizi ya mara kwa mara katika lango la wapinzani wao lakini bila
mafanikio. Baada ya hapo timu ya Arusha ilifanya
mashambulizi mengi langoni mwa wa pinzani wao na kufanikiwa kupata goli la tatu
katika dakika ya 56 kupitia tena kwa Mohamedi Saidi.
Katika mechi nyingine ya Copa Coca-Cola
iliochezwa jana iliwakutanisha
Kilimanjaro na Mbeya katika uwanja wa kumbukumbu wa Karume ambapo Kilimankaro
waliibuka na ushindi wa 1-0 , goli lililofungwa na Selemani Mwalimu katika
dakika ya kwanza baaada Kilimanjaro kufanya
shambulio la ghafla.
Washiriki wapya katika michuano hii ya Copa
Coca-Cola timu ya Geita ilijikuta katika wakati mgumu sana baada ya kukubali
kipigo cha 4-1 kutoka kwa watoto wa mjini Temeke katika uwanja wa Tumbi ,
Kibaha ambao walitoka sare ya 1-1 dhidi ya wapinzani wao timu ya Ilala katika
mechi ya ufunguzi iliofanyika jumapili katika
uwanja wa kumbukumbu wa Karume jijini Dar es Salaam.
Akiongea katika ufunguzi
huo Makamu wa pili wa Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania
(TFF) Ramadhani Nasib , alisema kuwa mashindano ya vijana ni msingi wa kuibua
vipaji vya wachezaji ambavyo vitaleta mabadiliko katika medani ya soka nchini.
Kwa upande wake Meneja bidhaa wa Coca-Cola
nchini Maurice Njowoka alisema kuwa
Coca-Cola itaendelea kudhamini mashindano ya vijana kuanzia ngazi ya wilaya
mpaka taifa.
Alisema kuwa kubadilisha mashindano kutoka umri wa miaka
17 mpaka 15 ni moja kati ya juhudi za Coca-Cola pamoja na TFF na FIFA ili
kuwafikia vijana wadogo wakike na wakiume ilikukuza vipaji vyao.
Wakati huo huo timu ya Copa Coca-Cola
imeondoka kuelekea Afrika ya Kusini kwenye mafunzo ya wiki moja siku ya
jumapili. Mafunzo hayo yatawapa uzoefu vijana hao katika kuendeleza vipaji
vyao.
Mafunzo hayo yatawakutanisha timu kutoka
nchi mbaimbali katika bara la Afrika.
No comments:
Post a Comment