Makamu mwenyekiti wa UTPC Bi Jane Mihanji akitoa tamko la UTPC dhidi ya Chadema kutaka kutumia kifo cha Mwangosi kisiasa.
Rais wa UTPC Bw Keneth Simbaya kushoto akimpongeza makamu wake Bi Jane Mihanjo kwa tamko zuri alilolitoa.
Akitoa tamko kwa niaba ya bodi ya UTPC jana , Makamu wa Rais Jane Mihanji wakati mkutano mkuu maalumu wa kupitisha marekebisho ya Katiba ya UTPC uliyofanyika Mjini Dodoma kwa muda wa siku mbili.
Alisema kuwa Chama hicho kisitumie kifo cha mwandishi wa habari huyo kujinufaisha katika maslahi binafsi ya kisiasa kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na ukiukwaji wa haki za binadamu katika kutumia vifo kama mtaji wa kisiasa. |
“..Sisi kama UTPC tunatoa tamko hilo kwa uchungu na pia chama hicho kisitumie kifo cha Daudi Mwangosi katika maslahi ya kisiasa kwani hatuko tayari na swala hilo au zoezi hilo la kujenga mnara kwenye sehemu hiyo kwani tunapinga vikali ujenzi huo unaotarajiwa kufanywa na chama hicho’Alisema Mihanji.
|
Alisema ujenzi wa mnara huo ambao inatarijiwa kufanywa na chama sio kazi yao kwa ili wanatafuta umaharufu wa kwenye majukwaa na kuwataka waache wakawaachia wahusika wenyewe jumuhia za waandishi wa habari ambao ndiyo wenye mamlaka na si vinginevyo.
|
Mihanji alisema kuwa, Mwangosi hakuwa mwanasiasa bali alikuwa ni mwana taalumu katika tasnia ya habari “Kwani yeye kufuatia mauaji yake hakuwa katika harakati za kisiasa bali alikuwa kikazi ambayo ni ya kitaaluma kwahiyo wenye mamlaka ya ujenzi au kufanyiwa jambo fulani la kihistoria ni wahusika ambao ni wanataaluma wenyewe na siyo chama cha kisiasa.
|
“UTPC ndiyo wenye mamlaka ya kufanya suala au zoezi hilo na siyo chama hicho kwahiyo ni vema swala hilo waakaliacha kama lilivyo kwani sisi ndiyo wahusika kwahiyo tunajua nini tunataka kufanya juu ya Mwangosi kwahiyo tamko letu ndiyo hilo kwa chama hicho swala hilo liachwe na tuachiwe wenyewe”Alisema makamu wa rais huyo.
|
Mwangosi alikuwa mwandishi wa kituo cha Televisheni cha Chanel ten Mkoani Iringa ambaye pia alikuwa ni mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoani humo (Iringa Press Club) ambapo ameuawa mikononi mwa jeshi la polisi mnamo 2012.
Hata hivyo hadi sasa bado suala la kifo cha Mwangosi limeendelea kupigwa dana dana kutokana na kesi yake kutosikilizwa na hakuna mwandishi aliyeitwa kutoa ushahidi wake juu ya mauwaji hayo .
Mwangosi hakuuwawa kama mwanachama wa Chadema bali aliuwawa akiwa kazini kutimiza wajibu wake wa kitaalum ya uandishi hivyo kwa kitendo cha Chadema kutaka kushirikiana na IPC katika ujenzi huo itakuwa ni kuvuruga mwenendo wa kesi na kupingana na msimamo wa awali ya IPC ,UTPC na vyombo vingine kuhusu taarifa za awali ambazo jeshi la polisi lilianza kutaka kupotosha kuwa eti alikuwa ni mwanachama wa Chadema jambo ambalo si kweli.
|
No comments:
Post a Comment