Madereva boda boda wakiwa tayari kuelekea nyumbani kwa mshindi wa nyumba eneo la Frelimo mjini Iringa leo
Safari ya kuelekea Frelimo ikianza
Hakika Airtel Yatosha wengi kujiunga na Airtel
Madereva wa boda boda mjini Iringa wakitoka maeneo ya Frelimo mjini Iringa wakati wa ziara ya wafanyakazi wa Airtel makao makuu na Iringa kumtembelea mshindi wa nyumba ya kwanza ya Airtel Yatosha Bw Sylivanus Juma Wanga ambae ni mhasibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya TARWOC ambae amekabidhiwa fungu ya nyumba na kuelekea jijini Dar es Salaam kukabidhiwa nyumba yake
Mshindi wa nyumba ya Airtel Yatosha Bw Sylivanus Wanga kulia akimpokea kwa furaha ofisa mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando baada ya kumtembelea mtaani kwake Frelimo Iringa
Mshindi wa nyumba ya kwanza ya Airtel Bw Bw Sylivanus Juma Wanga na ndugu zake wakifurahia kutembelewa na wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Airtel nyumbani kwao Frelimo mjini Iringa kwa ajili ya kukabidhiwa funguo na hati ya nyumba yao kabla ya kuelekea Dar es Salaam kukabidhiwa nyumba yake kulia wa kwanza ni ofisa mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando, meneja wa Airtel nyanda za juu kusini Beda Kinunda ,mke wa mshindi Bi Veronica Wanga ,Bw Sylivanus Wanga na shemeji yake Bi Martha Kibiki
Ofisa mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando (kushoto) na meneja wa Airtel mikoa ya kusini Beda Kinunda wakiwa nje ya nyumba ya mshindi wa nyumba ya kwanza ya Airtel yatosha eneo la Frelimo mjini Iringa
Ofisa habari wa Airtel Bw Jackson Mmbando wa pili kulia akizungumza lengo la ziara yao mjini Iringa kwa mshindi wa nyumba ya kwanza ya Airtel Yatosha nyumbani kwake Frelimo Iringa
Mmoja kati ya wafanyakazi wa taasisi ya TARWOC Bw Beni Kibiki akiwa nyumbani kwa mshindi wa nyumba ya kwanza ya Airtel Yatosha leo eneo la Frelimo mjini Iringa
Mshindi wa nyumba ya kwanza ya Airtel Bw Bw Sylivanus Juma Wanga na ndugu zake wakifurahia kutembelewa na wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Airtel nyumbani kwao Frelimo mjini Iringa kwa ajili ya kukabidhiwa funguo na hati ya nyumba yao kabla ya kuelekea Dar es Salaam kukabidhiwa nyumba yake kulia wa kwanza ni ofisa mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando, meneja wa Airtel nyanda za juu kusini Beda Kinunda ,mke wa mshindi Bi Veronica Wanga ,Bw Sylivanus Wanga na shemeji yake Bi Martha Kibiki
Hii ndio nyumba anayoishi mshindi wa nyumba ya Airtel Yatosha iliyopo eneo la Frelimo mjini Iringa
Meneja wa Airtel yatosha mikoa ya kusini Beda Kinunda akiogoza familia ya mshindi wa Nyumba kuelekea ukumbini katika hafla ya kukabidhiwa funguo na hati ya nyumba kabla ya kuelekea jijini Dar es Salaam kukabidhiwa nyumba yake
Eneo la Frelimo mjini Iringa ambalo mshindi wa nyumba ya kwanza ya Airtel yatosha anaishi
Wafanyakazi wa Airtel wakiwa nje ya gari wakimsubiri mshindi wa nyumba kushuka
Mke wa mshindi wa nyumba ya Airtel Yatosha Bi Veronica Wanga akishuka katika gari tayari kwenda ukumbini kukabidhiwa funguo na hati yao
Mshindi wa nyumba wa pili kushoto akiwa ameshuka katika gari tayari kuelekea ukumbini
Wafanyakazi wenzake na mshindi wa nyumba kutoka taasisi ya TARWOC
Baadhi ya wafanyakazi wenzake na wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo wakianza kujiounga na shindano hilo
Ofisa mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando akionyesha funguo ya nyumba aliyoshinda Bw Sylivanus Juma Wanga (kushoto) kulia ni meneja wa Airtel mikoa ya kusini
Ofisa mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando akimpongeza mshindi wa nyumba ya kwanza kati ya nyumba tatu zinazoshindaniwa Bw Sylivanus Juma Wanga kushoto huku meneja wa Airtel mikoa ya kusini Beda Kinunda akishuhudia
Meneja wa Airtel mikoa ya kusini Beda Kinunda akimkabidhi funguo ya nyumba mshindi wa nyumba ya kwanza ya Airtel Yatosha jana kutoka Frelim mjini Iringa Bw Sylivanus Juma Wanga wanaoshuhudia ni mke wa mshindi Bi Veronica Wanga na ofisa mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando
Mmbando akitoa ufafanuzi juu ya mshindi huyo alivyopatikana kabla ya kumkabidhi hati yake ya nyumba leo
Ofisa mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando akionyesha hati ya nyumba
Mshindi wa nyumba ya Airtel yatosha akisoma hati ya nyumba yake aliyoshinda baada ya kukabidhiwa leo
Mshindi wa nyumba ya Airtel Yatosha akionyesha hati yake ya nyumba aliyokabidhiwa leo,huku akiwa na wafanyakazi wenzake waliofika kushuhudia
Ofisa mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando akimkabidhi mke wa mshindi wa nyumba ya Airtel yatosha Bw Sylivanus Juma Wanga Bi Veronica Wanga huku kushoto mume wake ambae ni mshindi akishuhudia mshindi huyo ni mhasibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya TARWOC inayojihusisha na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia mkoa wa Iringa ,wengine pichani ni wafanyakazi wenzake waliofika kushuhudia hafla hiyo iliyofanyika Hotel ya M.R mjini Iringa
............................. .............................. ...........................
• Kusafirishwa na Airtel kuja dar alhamisi
wiki hii kupokea nyumba yake
Hatimaye mshindi wa nyumba ya kwanza ya Airtel Yatosha yenye thamani
ya shilingi milioni 65/- iliyotolewa na Kampuni ya mitandao ya simu za
mkononi Airtel, mwishoni mwa wiki hii amekabidhiwa rasmi funguo yake
baada ya kuibuka mshindi kupitia promosheni maalumu ya Airtel yatosha
shinda nyumba 3.
Huku wananchi wa mji wa Iringa wakijipanga barabarani kumshangilia na kuipongeza kampuni ya simu ya Airtel kwa kuonyesha njia kwa makampuni mengine. Makabidhiano ya funguo hiyo kwa mshindi, Bw. Silvanus Juma yalifanyika
mwishoni mwa wiki hii mkoani Iringa na kushuhudia mshindi huyo wa
Airtel akikabidhiwa funguo pamoja na cheti kinachoonesha kwamba yeye
ni mshindi wa kwanza wa nyumba katika nyumba tatu zinazoshindaniwa
kupitia promosheni ya Airtel Yatosha.
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema hafla hiyo ya kukabidhi funguo imefanyika ikiwa sambamba ya kumtembelea mshindi huyo nyumbani kwake eneo la Frelimo mjini Iringa ili kujionea maisha yake kabla ya kukabidhiwa nyumba yake.
“ makabidhiano ya hizi funguo ni ya awali lakini Alhamisi ya wiki hii
mshindi huyu Bw. Silvanus Juma atakabidhiwa rasmi nyumba yake iliyopo
maeneo ya Kigamboni jijini Dar es salaam”
Aliendelea kwa kusema Airtel inayo furaha kubwa kumkabidhi mshindi wao
huyo zawadi hiyo na itaendelea kutoa zawadi zilizo bora kwa wateja
wake nchi nzima kupitia promosheni mbalimbali zinazoendeshwa na
Kampuni hiyo.
“Kama alivyo na furaha mshindi wetu ndivyo na sisi tunavyofurahi na
hii sio kikomo bado kuna zawadi mbalimbali kwa wateja wa Airtel nchi
nzima na cha muhimu ni wao kujiunga na vifurushi mbalimbali
vinavyopatikana kwenye promosheni hii ya ya Airtel yatosha shinda
nyumba 3. mbalimbali za Airtel ili kushinda,” alisema Mmbando.
Aliongeza Mmbando kwamba ili mteja wa Airtel aweze kujiunga na
vifurushi hivyo anapaswa kupiga *149*99# na kuchagua 1 au 2 kisha
aweze kujiunga na kifurushi chochote cha wiki, siku au mwenzi hiyo ndo
njia pekee ya kushinda.
Mpaka sasa Airtel imeweza kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wake
nchi nzima ambapo imetoa shilingi milioni 37 kwa washindi 37 na
inaendelea na promosheni hiyo ambayo inadumu kwa siku 90, sambamba na
hilo nyumba mbili kati ya tatu zilizopo Kigamboni bado zinashindaniwa
kupitia promosheni hiyo ya Airtel yatosha, shindanyumba 3.
Akielezea furaha yake Bw. Juma alisema zawadi hiyo ya nyumba ni bahati
ya kipekee ambayo hakuitarajia hapo awali na hata alipopigiwa simu
hakuamini kwa sababu alijua kitu kama hicho hakiwezekani na hawezi
kupata nyumba katika msimu kama huo.
“Nilipopigiwa kwanza nilijua ni utani, pengine mtu amejisikia tu
kunitania lakini nilipigiwa tena na hapo ndipo nilipoanza kuamini.
Nawashukuru sana Airtel kwa zawadi hii na ni kielelezo wazi kuwa
Airtel ni mtandao unaojali na kuthamini wateja wake,” alisema Juma.
Bw Juma alipatikana baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kwanza katika
makao makuu ya Airtel Dar es salaam mwisho wa mwenzi wa saba mwaka huu
ilyopelekea Bw. Juma kuibuka mshindi wa kwanza katika promosheni hiyo.
Wakati huo huo baadhi ya wananchi wa mji wa Iringa katika maeneo mbali mbali ambayo msafara wa mshindi huyo ulipita walionekana kujipanga barabarani kumshangilia mshindi huyo na Airtel kwa kumpungia mikono, huku baadhi ya shughuli zikisimama kwa shauku ya kumuona mshindi wa nyumba ya kwanza ya Airtel Yatosha kutoka mjini Iringa.
Akizungumza kwa nibaya ya wananchi wenzake Pendo Luwoga alisema kuwa wamelazimika kufika kushuhudia tukio hilo kutokana na wengi wao kutokuwa na imani na bahati nasibu mbali mbali zinazochezeshwa na makampuni ya simu ila kwa tukio hilo la Airtel kweli wameamini kuwa hakuna ubabaishaji na wao wapo tayari kujiunga na Airtel na kuendelea kucheza mchezo huo ili ikiwezekano mkoa wa Iringa kuonyesha maajabu kwa kushinda nyumba zote.
No comments:
Post a Comment