Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya (katikati) akikagua mfumo wa
umwagiliaji bustani za mbogamboga katika maonesho yanayoendelea ya
nanenane kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akipokea maelezo kutoka kwa
wataalam wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) juu ya gari
iliyotengenezewa mfumo wa nishati ya gesi katika maonesho ya nanenane
kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akikagua bidhaa mbalimbali
kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi katika maonesho ya
nanenane kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya. Mkuu huyo wa Mkoa
ameridhishwa na vifungashio vingi vilivyotumika katika maonesho hayo
mwaka huu na wajasiriamali wa Mkoa wa Rukwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiangalia "shamba jiko"
ambalo staili yake ni ya kupanda mbogamboga nyumbani katika eneo dogo
kwenye maonesho ya nanenane kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akikagua maji aina ya Dew
Drop, maji pekee yanayotengenezwa Mkoani Rukwa Mjini Sumbawanga na
Mjasiriamali wa ndani, maji ambayo wananchi na wadau wengi wanasifia
ubora wake kuwa ni ya kiwango cha juu. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa huo
Alhaj Salum Mohammed Chima.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na Katibu Tawala Mkoa huo
Alhaj Salum Mohammed Chima wakikagua banda la Halmashauri ya
Manispaa Sumbawanga ambalo limesifika kwa umaridadi wake.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akikagua samaki mbalimbali
waliopo katika moja ya banda la Wilaya ya Nkasi katika maonesho ya
nanenane kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya. Samaki hao
wamekaushwa kitaalam na wana uwezo wa kukaa mda mrefu bila kuharibika.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na Katibu Tawala Mkoa huo
Alhaj Salum Mohammed Chima wakipata maelezo kwa mtaalam wa hali ya hewa
walipotembelea kituo cha hali ya hewa kilichopo katika maonesho hayo.
Kifaa kinachoonekana kinatumika kupima wingi wa mvua.
TanSeed wakitangaza bidhaa zao za mbegu kwa staili ya aina yake.
Ebony
Fm Radio ya nyanda za juu kusini ambayo makao makuu yake ni Mjini
Iringa ikifanya mahojiano ya moja kwa moja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Mhandisi Stella Manyanya mara baada ya kiongozi huyo kuzungukia mabanda
kuzungumzia maonesho hayo kwa ujumla wake.
Picha
ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na
baadhi wafanyakazi wa Radio ya Ebony FM ya Mjini Iringa maara baada ya
Interview.
MC MIMA, Misasi Marco akipaisha vokali zake.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akitangaza rasmi
kuzaliwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya katika usiku
wa maonesho ya nanenane "Rukwa Day" katika ukumbi wa JKT Nanenane
Jijini Mbeya saa 12:01 Usiku wa tarehe 04/08/2013. Kulia ni Mkuu wa
Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiwa amebebwa juujuu na
wananchi pamoja na watumishi walioshiriki hafla fupi ya "Rukwa Day"
katika maonesha ya nanene nyanda za juu kusini Jijini Mbeya ikiwa ni
pongezi kwake katika siku yake ya kuzaliwa ya tarehe 04/08.
Kaimu
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
Ndugu Respich Maengo akimpongeza Mhe. Manyanya kwa siku yake ya
kuzaliwa.
Simon
Mutabazi Mkaguzi wa ndani Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akimpongeza
Mhe. Manyanya kwa siku yake ya kuzaliwa. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa Rukwa "rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment