Baadhi ya washiriki wa mbio za Baiskeli Kanda ya Ziwa (Safari Bike Race) 2013, Wanaume wakichuana kuelekea Nzina (Igunga) km 210 kutoka Shinyanga na kurudi wakati wa sherehe za sikuu ya nane nane ambazo hufanyika kila mwaka kwa kanda hiyo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Kaimu katibu tawala Rasilimali na Watu wa Shinyanga, Projestas Lubanzibwa(kushoto) akimkabidhi bingwa wa Mbio za Baskeli Kanda ya Ziwa (Safari Bike Race) 2013, Masunga Duba kutoka Mwanza, kitita cha shilingi milioni moja (1000000/=) zilizofanyika Mkoani Shinyanga wakati wa sherehe za siku kuu ya nanene ambazo hufanyika kila mwaka.
Bingwa wa Mbio za Baskeli Kanda ya Ziwa (Safari Bike Race) 2013, Masunga Duba kutoka Mwanza(kulia) akionyesha kitita cha shilingi milioni moja (1000000/=) mara baada ya kukabidhiwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Kaimu katibu tawala Rasilimali na Watu wa Shinyanga, Projestas Lubanzibwa zilizofanyika Mkoani Shinyanga wakati wa sherehe za siku kuu ya nanene ambazo hufanyika kila mwaka.
Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa wamefurika katika Uwanja wa mpira wa Miguu wa Kambarage Mkoani Shinyanga kushuhudia mbio za Baiskeli kwa kanda ya Ziwa zinazojulikana kwa “Safari Bike Race” wakati wa kusherehekea sikuu ya nane nane ambazo hufanyika kila mwaka kwa kanda hiyo.
Msanii wa kutoka kampuni ya Integrated Comminications,Jembe Ulaya akitumbuiza mara baada ya mashindano ya Mbio za baiskeli Kanda ya Ziwa(Saafari Bike Race) wakati wa kusherehekea sikuu ya nane nane ambazo hufanyika kila mwaka kwa kanda hiyo.
No comments:
Post a Comment