Wednesday, August 14, 2013

KAGASHEKI CUP 2013: KASHAI FC 1 vs RWAMISHENYE FC 2, TIMU YA KASHAI YAPEWA KIBANO, YACHINJWA 2-1 NA RWAMISHENYE!! SASA FAINALI NI BILELE FC NA RWAMISHENYE FC JUMAMOSI HII

Habari na Picha na Faustine Ruta, Bukoba 
 Timu ya Rwamishenye imeibuka shujaa na kufanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya michuano ya KAGASHEKI CUP 2013 baada ya kuchomoza na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Kashai Fc katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Rwamishenye ndio walioanza kufunga bao kupitia mshambuliaji Khalid Seleman kipindi cha kwanza nao Kashai wakiongeza bidii na kuweza kusawazisha bao hilo kipindi hicho hicho cha kwanza kupitia mchezaji wao Paulo Manu. 
Kipindi cha kwanza kikimalizika timu zote zikiwa nguvu sawa. Kipindi cha pili kilitawaliwa na timu ya Rwamishenye huku wachezaji wa timu ya Kashai Fc wakizembea kukaba wenzao na kuchoka ambapo  wachezaji wa Rwamishenye walitumia nafasi hiyo na kuweza kuwaongezea bao la pili kupitia mchezaji wao matata Hassan Hussein aliyeingia kipindi cha pili kwa mkwaju mkali uliompita mlinda mlango wa timu ya Kashai. 
 Ushindi huu walioupata Rwamishenye unawawezesha kutinga hatua ya Fainali siku ya Jumamosi hii tarehe 17 Agosti kuwavaa washindi walioifunga timu ya Makhirikhiri (Kitendaguro Fc) jana ambao ni Bilele FC katika uwanja wa Kaitaba. 
 Mchezo huu pia umeweza kuingiliwa na sintofahamu baada ya mashabiki wa timu ya Kashai Fc kuanza kufanya vurugu na kurusha mawe dakika za mwishoni baada ya kuona timu yao imefungwa na jambo hilo limeweza kunyamazishwa na askari wa FFU waliokuwa uwanjani humo na kuweza kuwaokoa wachezaji na waamuzi wa mtanange huo wasidhurike.

Timu zikiingia uwanjaniWachezaji wakisalimiana muda mchache kabla ya mtanage kuanza

Wachezaji wakisalimiana muda mchache kabla ya mtanage kuanza
Wachezaji wa timu ya Kashai wakiomba uwanjani
Wachezaji wa Rwamishenye.


Waamuzi wa mtanange huu
Kikosi cha timu ya Rwamishenye kilichoanza
Mtanange ukiendelea...
Hatari kwenye lango la timu ya Rwamishenye..
Furaha ikaanzia hapa...kwenye benchi la ufundi baada ya timu ya Rwamishenye kupata bao la kwanza
Wachezaji wa Timu ya Rwamishenye wakishangilia baada ya kupata bao hapa na kufanya 1-0 dhidi ya Kashai Fc
Hatari kwenye lango la timu ya Kashai Fc ...kipa akipangulia mpira kwa mbele..



Mashabiki wa Timu ya Kashai wakishangilia uwanjani Kaitaba
Mashabiki wa Kashai FC
Awe kaka ...Dada hapa wote walikuwa wakiishangilia timu..ya Kashai
Bao...bao.....
Mtanange ukiendelea hapa ...na hapa ni patashika kwenye goli la Rwamishenye..Timu ya Kashai ikisawazisha bao hapa kipindi cha kwanza...
Wachezaji wa Kashai wakishangilia baada ya kusawazisha bao na kufanya 1-1 dhidi ya Rwamishenye FC
Mashabiki wa Kashai Fc wakishangilia baada ya timu yao kusawazisha bao.
Mtangazaji Abdulzack wa Radio Kasibante Fm 88.5 akitangaza live mechi hii 
Hapa ni furaha kwa timu ya Rwamishenye baada ya kupata bao la pili, anaonekana kiongozi wa timu hiyo ya Rwamishenye akicheza na mwendesha Baiskeli 
Wachezaji wa Timu ya Rwamishenye nao wakishangilia na kupongezana kwa ushindi huo
Askari walilazimika kusindikiza waamuzi wa mechi hiyo baada ya refa kumaliza mtanange huo uliochezwa dakika 90 tu na timu ya Rwamishenye ikiibuka kidedea kwa 2-1
Wachezaji wa Rwamishenye wakicheza Ngwasuma hapa!
Chinja chinja sisi....bado Bilele!!!
Ushindi raha jamani!!!!!
RATIBA: HATUA YA  FAINALI

Jumanne 13 Agosti
10:00 Jioni  - Bilele  1 vs kitendaguro 0
Jumatano 14 Agosti
10:00 Jioni - Kashai Fc 1 vs  Rwamishenye Fc 2
Ijumaa 16 Agosti

Kutafuta mshindi wa tatu, itakuwa ni Kitendaguro FC vs Kashai FC 

Jumamosi 17 AgostiFainali

No comments: