Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya BILELE FC imelazimika kupigana kufa na kupona ili waweze kutinga hatua ya fainali ikicheza dakika 90 na timu ya Kitendaguro fc bila ya kufuna na ikiongezwa dakika 30 imeweza kuifunga timu hiyo maarufu kwa jina la Makhirikhiri yeye maskani yake Kitendaguro - Kibeta.
Bao la pekee la timu ya Bilele limefungwa dakika kipindi cha kwanza cha dakika 120 na mchezaji Ndomondo, Huku wakicheza pungufu baada ya mwenzao kupewa kadi nyekundu kipindi cha pili cha dakika 90.
Ushindi huu unawasogeza Bilele hatua ya Fainali wakimsubiri mshindi wa kesho kati ya timu ya Kashai Fc na timu Rwamishenye Fc mtanange utakaochezwa kesho Jumatano saa 10.00 jioni.
Timu zikisalimiana muda mfupi kabla ya mtanange kuanza
Timu zikisalimiana muda mfupi kabla ya mtanange kuanza hapa kwenye Uwanja wa Kaitaba
Picha ya pamoja Waamuzi wa mtanange huu na timu kapteini
Waamuzi wa mtanange huu kwenye picha ya Pamoja
Kikosi Cha Pamoja cha Timu ya Bilele
Kikosi Cha Pamoja cha Timu ya Kitendaguro pamoja na viongozi wao (kushoto)
Mchezaji wa timu ya Kitendaguro akitaka kumtoka mchezaji wa Bilele hapa...
Frii kiki kuelekea kwenye lango la timu ya Bilele
Majanga hapa mchezaji wa Bilele kaumia..na hapa anapata msaada wa haraka
Hatari kwenye lango la timu ya Kitendaguro
Mchezaji wa Bilele akisonga kwenda mbele ya lango la timu Kitendaguro
Shabiki wa timu ya Bilele akiwaamasisha mashabiki wenzake kuwapa sapoti wenzao uwanjani hapa.
Patashika hapa..mpira ukiwaacha wote ....
Wachezaji wa timu ya Bilele wakicheza mtanange safi na kuweza kuwafunga wenzao Kitendaguro ambao ndiyo walikuwa wanapewa nafasi ya kushinda leo hii kwenye mtanage huu na wadau wengi.
Dakika 90 zinamalizika na kuongezewa muda wa dakika 30, kipindi cha dakika 120- kipindi cha kwanza Mchezaji wa Bilele Ndomondo anaachia mkwaju mkali na baada ya mabeki wa timu ya Kitendaguro kufanya makosa na mkwaju huo kuishilia nyavuni.
Wachezaji wote wa Bielele na Kiendagueo wakiteta jambo kuhusu kufanya mashambulizi katika kipindi hiki cha dakika 30 zilizoongezwa.
Diwani wa Kibeta Mzee Rwangisa na mama (kushoto) wakiwa wanaangalia mtanange wa timu yao ya Kitendaguro jioni hii, Hapa mzee akionekana kukata tamaa baada ya timu yake kufungwa bao katika kipindi cha kwanza cha dakika 120. Mtanange ukiwa mkali kweli kweli..
**********
RATIBA: HATUA YA NUSU FAINALI
Jumanne 13 Agosti
10:00 Jioni - Bilele 1 vs kitendaguro 0
Jumatano 14 Agosti
10:00 Jioni - Kashai Fc vs Rwamishenye Fc
Ijumaa 16 Agosti
Kutafuta mshindi wa tatu
Jumamosi 17 Agosti
Fainali
No comments:
Post a Comment