Bwana michuzi nashukuru sana kwa kazi yako ya kutuelimisha na kutujulisha kwa mambo yanayotekea nyumbani nashukuru pia kwa kuweza kutuwekea hoja kubwa kama hii katika mtandao na kutupa uwanja wa kuweza kuchangia maoni yetu katika kupata katiba ambayo itakuwa ni ngao ya watanzania wa bara na visiwani,
Ningependa kwanza kwaombea wazee wetu walio tangulia kwenye haki waanzilishiwa taifa letu TANZANIA MZEE J.K.NYERERE NA MZEE ABEID AMANI KARUME, Wazee wetu hawa wakati wanaanzisha huu muungano walikiuwa na nia nzuri ukifatiria na hali ya siasa iliyo kuwepo wakati huo ,ni kweli kabisa upendo wa wazee hawa ulikuwa ni wa haina yake na mpaka walipofikia kuamua kitendo hicho walikuwa ni majasiri na mashujaa.
Ni kweli muungano umetuletea mambo mazuri mengi na kunamambo ambayo ukiangalia kwa kirefu au kwa upana unaona kuna makosa ambayo yanaweza kutatuliwa na watu wanaoipenda Tanzania (maana yake naposema hivi kuna vibaraka wanaotumiwa na watu kutoka nchi za nje ili kuvunja muungano huu hau kuigawanya nchi kwa makabira na kwa dini)
Wa Tanzania kubomoa ni rahisi na kujenga siyo mchezo ndugu zangu tukumbuke kitukimoja sisi kama waafrica tumetawailiwa na waarabu wariotoka makwao tumetawaliwa na wazungu walio toka makwao na kutufanya watumwa na kuuwa mababu zetu waliokuwa wakitembea maili na maili na kutufanya sisi ni mbwa na leo hii hayo yote tuna aanza kuyasahau na kutaka kurudi katika ukoloni wa mambo leo,
Ndugu zangu tukumbuke haya yote na damu za mababu zetu kutokea mwanza,kigoma,tabora,songea, tanga manyema congo,na ungunja,pemba, na mikoa yote ya TANZANIA,Damu iliyomwangika isije ikapoteabure tukumbuke tunapotoka ndio tupate katiba yenye utaifa, ni mazuri ghani yaliyopo kwenye katiba ya zamani? na mambo ghani ambayo hayafai kwenye katiba hiyo ya zamani,
je mfumowa serikali mbili unafaa au vipi? au serikari tatu? au tuwe na serikali moja tuu na nchi iwe na state maana yake itakuwa inaitwa UNITED STATE OF TANZANIA and tuwe na Raisi ,makamu waRaisi na Waziri mkuu ?
ndugu zangu kwanza hapa shida siyo serikari tatu au mbili au moja shida ni moja tuu ambayo inarudisha maendeleo nyuma na kufanya asilmia karibu 65 ya waTanzania kubaki masikini na kuendelea kuwa masikini,Tatitizo ni hili hapa ni Good governance, Responsibility.
Acountabilty, Deliverance and good economic policies.nakingine ni hiki agenda ya Tanzania au Manifesto ya Tanzania iko wapi wakati wa mwalimu ilikuwa ni ujamaa wa kujitegemea je sasa hivi nini?
kwa upande wangu kutokana na nchi yetu kuwa bado ni maskini hatuwezi kuwa na serikari tatu uendeshaji wake utakuwa ni wagharama na pila atuwezi kuwa na maraisi watatu,maoni yangu yako very simple ningependa tuwe na serikali moja tuu maana yangu mimi sijui kuna nchi inaitwa Tanganyika au Zanzibar kitu nachojuwa ni kwamba nchiziliungana na kutengeneza au kuzaa taifa linaloitwa Tanzania,
kwa maana yangu au kuelewa kwangu ni kwamba tunapashwa kuwa serikali moja ambayo itakuwa na Raisi na makamu wake na waziri mkuu,
baadala ya ya kuwa na mikoa tuwe na state na hizi state zitakuwa chini ya serikali ya katikati au central,
hizi state zitakuwa na Katikiro natumia jina la kiafrika ambaye hatakuwa anachaguliwa na wananchi na kazi zake ni kuwatumikia wananchi na kuhakikisha hanatimiza mipango yote ya serikali kwa uhakika na bila mchezo na muda wake wa kufanya kazi ni miaka kumi mitano,na mitano kama hatachaguliwa na wananchi tena.
Raisi hatachaguwa Governor ambaye kazi yake ni kuangalia mambo ya utendaji wa sela za serikali yani sera za nchi siyo za chama na kazi ya usalama yaani ataitwa Overseer na hii ndiyo itakuwa kazi yake tu na anaweza kuongezewa majukumu mengine,
Jee hizi state zitaendeshwa vipi zitakuwa zinakusanya mapato na asilimia 37 yawe yanabaki kwenye state na asilimia 63 yanaenda kwenye Central government na tuwe na mawaziri wa kuitumikia nchi moja na na tuwe na bunge moja tu lenye wabunge 250 wabunge 70 kutoka visiwani na wabunge 180 kutoka bara na tuwe na bunge la wezee au nyumba ya juu amabayo itakuwa na wazee 50 tuu ambayo itakuwa na wawakilishi wa dini waislam2,wakristu2,wahindu2, wazee wetu wa au wakuu wa chief2,nafasi zilizi baki watachuguliwa na bunge na kuteuliwa na raisi yaani retired jaji,police,wakuu wa majeshi,doctors,Raisi, mawaziri,na kiwango cha umri ni kuanzia miaka 60.
Pamaoja na haya yoteniliyosema bado tutakuwa pale pale kama hatutaweza kuwa na agenda au manifesto ya nchi siyo ya CCM,au CHADEMA ,au CAF,DP,auTLP ni mengi ya kusema hapa lakini naona kwanza ni achihe hapo kwenye swala la serikari moja,
Je kuhusu serikali mbili ni vipi? Kama tutaendela kuwa na serikali mbili je nini kinachotakiwa kufanywa sababu visiwani kunaonekana kwake mpaka sasa inaonekana kama ni nchi ndani ya muungano iko na bendera,iko na wimbo wa taifa, lakini bara hakuna wimbo wala bendera kw upande wangu tungeweza kujifunza kwa wenzetu wa hapa uingereza wako na nchi nne ndani ya muungano wa united kingdom, je nini ambacho tunacho weza kujifunza kutoka kwao au tunaweza kijifunza nini kutoka kwa hawa jamaa wa united emirates
Ndungu zangu ningependa sana hoja hii tuichambuhe kwa makini na kwa kirefu kutokana na historia yetu na tunapotoka sababu naamini Tanzania ya leo iko na wasomi wengi na wenye vipaji naomba sana tufunguke tuwe wazi tutoe maoni kwakirefu
Natanguliza shukrani kwa bwana Mchuzi na kwa waTanzania wote watako soma maoni yangu au kuchangia maoni yetu
Asanteni sana
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRICA
Na Mdau Yussuf
3 comments:
Nakubaliana na mtoa mada kwamba 'tuwe na serikali moja tuu'. Shida ni kwamba wenzetu wa visiwani watakubali unguja na pemba ziwe majimbo ndani ya serikali moja?
Kama watagoma, ambalo pia linawezekana. basi kuwe na magavana wawili ndani ya serikali moja. yaani gavana wa bara na gavana wa visiwani wenye hadhi sawa.
Raisi awe mmoja na makamu wake mmoja. ila sharti ni kwamba raisi akitoka bara makamu lazima atoke visiwani au kinyume chake.
Aisee hiyo kiswahili umetumia ni hatari, yani ni mchanganyiko wa maandiko mpaka unajiuliza nini umekusudia!
Kwa ufupi tu ungelijua kwamba muungano ni international legal treaty usingelikuja na mawazo ya kuvunja nchi za watu na kubaki na moja. Vipi Tanganyika iliweza kujiondolea jina la nchi yake na kutoweka hicho ni kitendawili ambacho wewe ungelitusaidia kukitegua. Zanzibar haijawahi kuwa state(jimbo) na haitokua hivyo. Muungano wa kweli ni ule utaoheshimu makubaliano ya awali ya waliouunda na kuheshimu mipaka ya makubaliano ya mkataba wa muungano wenyewe,leo hata huo mkataba serikali inaogopa kuuweka hadharani ukaonekana kilichomo ndani yake.
msiumize vichwa wazanzibari hawataki muungano , na hao waingereza muungano wao uko gatigati yao hawayasemi , skotilandi na wairish hawataki muungano wanalazimishwa , karibu watafanya kura kuamua hilo kwa kuwa wenzetu wana demokrasia ya kweli.
Post a Comment