Bodi ya taifa ya Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO), yenye dhima ya kikomo ya kuratibu na kuendesha mashindano ya Miss Utalii Tanzania, imetangaza kusimamisha kufanyika mashindano hayo katika ngazi zote kwa msimu wa 2013/2014 kwa lengo la kujipanga upya na kuboresha mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa mashindano hayo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo Erasto Gideon Chipungahelo, amesema uamuzi huo mgumu umechukuliwa katika kikao cha bodi hiyo kilicho fanya tathimini ya miaka mitano ya Miss Utalii Tanzania.
Mashindano ya Miss Utalii Tanzania yalifanyika mara ya kwanza nchini Mwaka 2004 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee na Fainali za Tano zilifanyika Mei 2013, jijini Tanga katika Uwanja wa Mkwakwani.
Bodi katika tathimini hiyo imebaini changamoto mbalimbali za kimfumo, utendaji na hujuma. Bodi pia imebaini changamoto mbalimbali ambazo zinapelekea sanaa ya urembo kudumaa au kuto kua kwa kasi inayo takiwa ukilinganisha na nchi jirani na hata nyinginezo Duniani.
Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na mfumo wa upatikanaji wadhamini, ambao umepelekea wabunifu wengi wa kazi za sanaa kukwama kwa kukosa wadhamini, changamoto nyingine ni hujuma za baina ya waandaaji, washiriki na hata wadhamini ambako kumepelekea kuwa na washiriki na viongozi mamluki wanao pandikizwa katika mshindano kwa lengo la kuchafua na kudhoofisha mashindano mengine.
Changamoto za udhamini na hujuma, zimekuwa ni tatizo kubwa kwa mashindano haya tangu kuanzishwa kwake ambapo kwa nyakati tofauti propaganda chafu dhidi ya shndan na viongozi zimekuwa zikienezwa kwa njia mbalimbali,majaribio mbalimbali ya wazi na mafichoni ya kupora shindano au hata kujeruhi viongozi.Hatua iliyo fikia hta kuporwa wadhamini waliojitokeza .
Licha ya ukweli kuwa katika umri wake wa miaka Miss Utalii Tanzania ndilo shindano lenye mafanikio makubwa zaidi kitaifa na kimataifa kuliko mashindano mengine yoyote nchini na hata Afrika mashariki na kati.
Mafanikio ambayo tumeyapata katika mazingira na mateso makubwa, ambayo yame tugharimu utu, hali na mali, na wakati mwingine kuweka rehani uhai wetu na mali zetu. Tofauti na mtizamo wa watu wengi, Miss Utalii Tanzania hatuja wahi kupata Mdhamini mkuu tangu kuanzishwa kwake, lakini pia hatuja wahi kupata udhamini wa zaidi ya 15% ya bajeti ya mashindano haya tangu kuanzishwa kwake. Kama kuna udhamini ulio patikana basi ni udhamini wa mashindano ya Dunia yaliyo fanyika nchini mwaka 2006, ambayo pia hakukuwa na udhamini wowote wa kampuni yoyote ya Tanzania.
Mafanikio tulipo anzisha mashindano haya hadi sasa ni pamoja na kuwa shindano pekee nchini , ambalo tumeshinda mataji katika mashindano yote ya dunia tuliyo shiriki yakiwemo ya Miss Tourism World 2005,Tourism Model Of The World 2006, Miss Tourism World 2006, Miss Africa 2006, Miss Tourism World 2007, Miss Freedom Of The World 2013, Miss Tourism World Internet 2008, Miss United Nation 2009 n.k.
Lakini kubwa zaidi ni kuwa shindano la kwanza nchini kutwaa taji la Dunia kabla na baada ya uhuru, hivyo kuitoa Tanzania kimasomaso, pia kuipa Tanzania heshima ya kuwa wenyeji wa fainali za Dunia 2006. Mafanikio hayo hayaishii hapo bali pia kwa Rais wa Mashindano haya Gideon Chipungahelo, kuwa mtanzania wa kwanza kuteuliwa katika uongozi wa ngazi ya Dunia wa Urembo , ikiwemo Mkurugenzi Bara la Afrika Miss Tourism World Organisation, Miss United Nation Organisation na Makamu wa Rais Dunia World Beauty Pageant Association, Miss Tourism University World Organisation na Miss Heritage World Organisation.
Katika kukabiliana na changamoto hizi, na kwa lengo la kuboresha mashindano, kuimarisha mfumo wa uongozi na mashindano, lakini pia kukabiliana na hujuma na tatizo la mamluki, bodi imebadili sera ya shindano na kuwa shindano la kijamii lisilo la kibiashara ( Non Profit Pageant) , ambapo matamasha ya ngazi zote za Miss Utalii Tanzania hayata kuwa na viingilio. Hatua hiyo inaenda sambamba na kubadilisha mfumo wa mashindano haya kuwa mashindano ya mfumo wa onyesho la Televisheni (TV Show), kupitia Miss Tourism Tanzania TV kuanzia ngazi za kanda.
Mfumo huu mpya unafuta fainali za jukwaani kuanzia ngazi za mikoa hadi majimbo, ambapo washindi wa ngazi za mikoa hadi majimbo watapatiakana kwa mtindo wa kuomba na kuteuliwa (Ideation). Kuanzia ngazi za kanda na kanda za vyuo vikuu ndipo warembo watapanda majukwaani. Fainali zote za ngazi za kanda hadi taifa zitakuwa LIVE katika Tv. Kwa lengo la kulifanya shindano kuwa la kimataifa kutakuwa na washiriki kutoka nje ya nchi (Dunia nzima) katika ngazi ya fainali za Taifa, ambao watakuwa mabalozi wa Tanzania katika nchi na mabara yao.
Utekelezaji wa mabalidiliko haya kunahitaji muda na timu makini ya kufanikisha mpango huu na kudhibiti changamoto zote zilizo jitokeza, ndio maana tumeona tusifanye mashindano kwa msimu mmoja ili kujipanga. Kwa mfumo huu mpya ambao utekelezaji wake unahusisha makampuni ya wataalam wa ndani na nje, washindi 1-5 wa Taifa wa Miss Utalii Tanzania kila mwaka kuanzia hawa wa mwaka huu watakuwa ndio maafisa uhusiano na wasemaji wa Miss Utalii Tanzania.
Hatua ya kutofanya mshindano kwa msimu mmoja wa 2013/2014 haimaanishi kusimama kwa shughuli za washindi Miss Utalii Tanzania 2013, wala asasi ya Miss Tourism Tanzania Organisation ( Miss Tourism Tanzania Limited), ikiwemo washindi hao kushiriki katika mashindano ya Dunia 2013/2014 kama ifuatavyo na nchi yakakako fanyika katika mabano Miss Tourism World 2013 ( Equatorial Guinea), Miss Face Of The World 2013 ( Afrika Kusini) , Miss Tourism United Nation 2013 ( Marekani), Miss International 2013 ( Japani), Miss Planet 2013 ( Ufaransa), Miss Tourism University World 2013 (Uingereza), Miss Heritage World 2013 (China).
Aidha bodi imeazimia kuwa yeyote atakaye bainika kuhujumu au kudhalilisha shindano na viongozi au washiriki atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya dola. Mfano ni hwa watu wanao tumiwa kuwarubuni washiriki wetu na kuwapiga picha za uchi, wako wanao warubuni washiri wetu na kuwatorosha kambini kwenda katika mashindano yao, lakini wapo pia ambao wanapandikiza washiriki wenye mienendo na maadili mabovu yakiwemo ya usagaji na ukahaba , hawa nao watakiona cha moto “Mchakacha Ujao Hautalengwa kwa Jiwe”
Asante,
Erasto Gideon Chipungahelo
Mwenyekiti Mtendaji
No comments:
Post a Comment