Tuesday, August 27, 2013

BARAZA LA KATIBA LA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA LAFUNGULIWA RASMI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akizungumza na Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim kabla ya ufunguzi rasmi wa Baraza la Katiba la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Ufunguzi huo uliowahusisha Mabalozi Wastaafu, Watumishi wa Wizara na Taasisi na wadau wengine ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa chaJulius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Agosti, 2013. Wengine katika picha ni Bw. John Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Mstaafu, Mhe. David Kapya.

Mhe. Membe akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Wizara ya Mambo  ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim kufungua rasmi Baraza hilo.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza hilo ambao ni Mabalozi Wastaafu wakimsikiliza Mhe. Membe wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo.
Mgeni Rasmi na Mjumbe wa Tume ya Mambadiliko ya Katiba, Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim akifungua rasmi Baraza la Katiba la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mhe. Dkt. Salim (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Baraza la Katiba la Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha.

Bw. Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mmbo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwakaribisha Wajumbe kwenye ufunguzi huo.

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya Mabalozi Wastaafu wakati wa ufunguzi huo.

Wajumbe zaidi wakati wa ufunguzi huo.

Wajumbe wakiwemo Mabalozi Wastaafu na Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakati wa ufunguzi.




Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Bertha Semu-Somi akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Wilson Masilingi wakati wa ufunguzi wa Baraza la Katiba la Wizara.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza ambao pia ni Wakuu wa Idara na Vitengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano  wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Baraza hilo.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza ambao pia ni Maafisa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walioshiriki ufunguzi wa Baraza la Katiba la Wizara.




Baadhi ya Wajumbe kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) walioshiriki ufunguzi wa Baraza la Katiba la Wizara.
Mgeni Rasmi, Mhe. Dkt. Salim na Mhe. Membe wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mabalozi Wastaafu.

Mgeni Rasmi, Mhe. Dkt. Salim na Mhe. Membe wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mabalozi Wastaafu na Wakurugenzi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Taasisi zake.

Mgeni Rasmi, Mhe. Dkt. Salim na Mhe. Membe wakiwa katika Picha ya Pamoja na Wajumbe wote wa Baraza la Katiba la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Picha na Reginald Philip.

No comments: