Mmoja kati ya madiwani wa Manispaa ya Iringa akiwa ameshika picha ya marehemu diwani Chonanga
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (mwenye Suti) na katibu wa Chadema Iringa mjini Suzana Mgonakulima wa kwanza kushoto wakiwa na madiwani wa CCM katika msiba wa diwani Chonanga leo
Msaidizi wa askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Blaston Gavile akiendesha ibada ya mazishi ya diwani Chonanga leo makaburi ya Mtwivila mjini Iringa
Hili ni gari ambalo lilkuwa likiufuata msafara wa waziri mkuu jambo ambalo lingeweza kusababisha ajali katika msafara huo hapa ni eneo la Mtwivila mjini Iringa
Msafara wa waziri mkuu Mizengo Pinda ukielekea makaburi ya Mtwivila kuongoza mazishi ya aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli Iddi Rashid Chonanga leo
Mwili wa marehemu Chonanga ukishusha kaburini na madiwani wa Manispaa ya Iringa
Mlezi wa CCM mkoa wa Iringa waziri mkuu Mizengo Pinda (kushoto ) mkewe Tunu Pinda wakiweka shada la maua katika kaburi la diwani Iddi Chonanga leo
Waziri mkuu Pinda akimsubiri mke wake Tunu Pinda aweke shada ya maua kabla ya kutoa heshima yao ya mwisho leo
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma akiweka shada la maua katika kaburi ya diwani Chonanga leo
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) wakishirikiana kuweka shada la maua katika kaburi la diwani Iddi Chonanga ,enzi za uhai wake diwani Chonanga na familia yake walikuwa wakikabiliwa na kesi ya kumtishia kumuua mbunge Msigwa kwa maneno kesi ambayo bado hukumu yake kutolewa
Mbunge wa jimbo la Kilolo na MNEC Prof Peter Msolla na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Lediana Mafulu wakiweka shada la maua katika kaburi la Chonanga leo
Mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi akipokea shada kutoka kwa afisa habari Manispaa ya Iringa Sima Bingileki ili kuweka katika kaburi la diwani Chonanga
Meya Mwamwindi akiweka shada la maua katika kaburi la Chonanga
Naibu meya wa Manispaa ya Iringa Bw Gervas Ndaki kushoto akiongoza madiwani kuweka mashada ya maua katika kaburi la diwani Chonanga leo
Katibu wa Chadema Iringa mjini na diwani wa viti maalum Suzana Mgonakulima kushoto akiweka shada la maua katika kaburi la Diwani mwenzake Chonanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Terresia Mahongo akiweka shada la maua leo kwenye kaburi la diwani Iddi Chonanga
Picha na habari na Francis Godwin Blog- Mzee wa matukio Daima
WAZIRI mkuu Mizengo
Pinda ambae ni mlezi wa
chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa
leo ameongoza wakazi wa mkoa
wa Iringa katika mazishi ya
aliyekuwa diwani wa kata ya
Nduli marehemu Iddi Rashid Chonanga huku akijitolewa kusomesha
watoto wake wawili na yatima mmoja aliyekuwa akisomeshwa na marehemu Chonanga.
Waziri Pinda alitoa
ahadi leo katika makaburi ya Mtwivila
mjini Iringa wakati akitoa
salam zake za rambi rambi kwa wakazi
wa kata ya Nduli na wananchi wa mkoa wa Iringa kufuatia
kifo cha diwani huyo .
Alisema kuwa kifo cha
diwani Chonanga kimeacha
pendo ndani ya familia na hata
katika chama chake
cha CCM kutokana na mchango
mkubwa ambao amepata kuutoa katika kupigania
chama hicho na kuwa kutokana na maombi kusomeshwa yaliyotolewa na watoto hao ambao
waliyatoa jana alipofika kuhani msiba
huo katika kijiji cha Nduli
Kuwa kwa upande wake
amejitolea kuisaidia familia hiyo
ya Chonanga kwa kusomesha
mtoto mmoja anayeendelea na masomo katika chuo
cha IFM jijini Dar es Salaam pia kumsomesha
kijana wake mmoja ambae
yupo sekondari pamoja na
kuendelea kumsomesha mtoto mmoja yatima ambae diwani
Chonanga alikuwa akimsomesha
katika shule ya Sekondari ya Miyomboni
mjini Iringa.
Mbali ya
kujitolea kusomesha watoto hao
bado waziri Pinda alilitaka
baraza la madiwani la Halmashauri
ya Manispaa ya Iringa na mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo kuangalia
uwezekano wa kumuenzi diwani Chonanga kwa kazi kubwa za maendeleo
alizozifanya katika kata yake kwa kuisaidia
familia yake .
“ Mimi nawashauri
madiwani pamoja na mkurugenzi wa Manispaa kutokana na mchango mkubwa ambao diwani Chonanga aliutoa katika kuwatumikia wananchi
wa kata ya Nduli ….sasa kuangalia
uwezekano wa kuisaidia familia yake…..sisi kama
chama leo tulikuwa na Halmashauri
kuu ya CCM tumechangishana kiasi cha
zaidi ya Tsh 800,000 ambazo
tunazikabidhi kwa familia”
Katika hatua nyingine
waziri Pinda amekipongeza
chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema)
wilaya ya Iringa mjini chini ya
mbunge wa jimbo la Iringa mjini
mchungaji Peter Msigwa kwa
kuonyesha ushirikiano mkubwa
katika mazishi hayo .
“ Kweli kwa moyo mkunjufu kabisa napenda kuwashukuru
sana viongozi wa Chadema
Iringa chini ya mbunge mchungaji Msigwa kwa ushiriki mzuri wa mazishi ya
diwani Chonanga ….nasema ahsanteni
sana mheshimu mbunge Msigwa na
wananchi wote ambao leo mmefika hapa”
Awali akiendesha
ibada ya mazishi hayo msaidizi wa askofu
wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya
Iringa Blaston
Tuluwene Gavile alitaka viongozi
wa serikali na kisiasa
kukumbuka kumcha Mungu na kuiga mfano wa Chonanga ambae mbali ya
kufanya shughuli za kisiasa ila katika dini alikuwa mstari wa mbele akiwa kama mshauri wa usharika wa
Nduli .
Alisema kuwa mara
kwa mara Chonanga alikuwa akipigania maendeleo ya
kata yake ya Nduli na
wananchi wake na kuna wakati alipata kumtamkia wazi wazi kuwa yupo tayari kufa na hata agopa binadamu yeyote katika kuwapigania
wananchi wake.
“ Marehemu alikuwa
mtetezi wa kweli
wa maendeleo ya wananchi wake
ndani ya chama chake na hata katika kanisa pia
ndio maana leo umati mkubwa
wa watu
wamejitokeza kumzika ila sisi kama kanisa tunasema kifo katika Kristo ni furaha kubwa
na leo hii mama mzazi
wa Chonanga ambae ana miaka zaidi
ya 83 ameomba kubatizwa rasmi “
Akisoma histori ya marehemu Chonanga mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Terresia Mahongo alisema kuwa
Chonanga alizaliwa mwezi Februari ,1947 katika kijiji
cha Malolo wilaya ya Kilosa
na elimu yake ya msingi
aliipata katika shule ya kati ( Middle School ) Kidodi wilaya ya Kilolo na kujiunga na mafunzo ya ualimu
katika chuo cha ualimu Songea mkoani
Ruvuma mwaka 1970
Katika uhai wake
marehemu aliajiriwa kama mwalimu
wa shule ya msingi mwaka 1972
ambapo miongoni mwa shule alizopata
kufundisha ni pamoja na Mwembetogwa ,Kilimani , Nyabula, Nduli na
Kitelewasi zilizopo mkoani Iringa pia marehemu aliwahi kuwa
mratibu elimu kata ya kalenga
kuanzia mwaka 1994-1999
alipostaafu kwa mujibu wa sheria na
mwaka 2000 alifanya kazi ya ualimu kwa
mkataba wa mwaka mmoja
Katika uongozi
amepata kuwa mwenyekiti wa CCM kata ya Nduli
kati ya mwaka 2000-2005 na mwaka
2010 alichaguliwa kuwa diwani wa
kata ya Nduli katika Halmashauri hiyo ya
Manispaa ya Iringa na katika baraza la madiwani
wa Halmashauri hiyo alikuwa ni
mwenyekiti wa kamati ya maadili na mjumbe wa kamati ya fedha na uongozi .
Mkurugenzi huyo
alisema kuwa katika kipindi
cha uongozi wake alikuwa ni
jasiri ,mfuatiliaji wa mambo,mshauri na mjenga hoja katika vikao vya madiwai .
Marehemu Chonanga
alianza kusumbuliwa na maradhi
ya moyo usiku wa tarehe 2/7/2013
na alfajiri ya tarehe 3/7/2013
alipelekwa Hospital ya Rufaa ya
mkoa wa Iringa kupata matibabu na mbali ya
jitihada zilizofanywa na
madaktari ila zilishindikana na majira
ya saa 7;45 mchana alifariki dunia .marehemu Chonanga ameacha mjane
mmoja watoto 10 na
wajukuu 9
Mungu ailaze
roho ya marehemu Iddi Rashid
Chonanga mahali pema peponi
AMINA
No comments:
Post a Comment