Thursday, July 4, 2013

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ATUA IRINGA KUUNGANA NA WAKAZI WA NDULI KUOMBOLEZA MSIBA WA DIWANI CHONANGA



 Mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu wa pili  kulia akitoa akiitambulisha familia ya marehemu diwani Idd Chonanga  aliyekuwa  diwani wa kata ya Nduli aliyefariki dunia  jana 


 Mtoto  mkubwa wa  marehemu  Idd  Chonanga Bw Greyson Chonanga akipewa  mkono wa pole na waziri mkuu Mizengo Pinda aliyefika  nyumbani kwao eneo la kijiji cha Nduli  kuhani msiba  huo jioni ya leo. Anayeshuhudia ni  mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu 


 Viongozi  mbali mbali wa CCM na  serikali mkoa wa Iringa  wakiwa na  waziri mkuu Mizengo Pinda pamoja  na  waombolezaji  wa msiba wa aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli Idd Chonanga aliyefariki jana 

 Mtoto  mkubwa wa diwani  Chonanga  akitoa maelezo kwa  waziri mkuu Pinda juu ya kifo cha baba yake 
 Waziri Mkuu Mizengo  Pinda akiomboleza  msiba wa  diwani Chonanga  leo katika  kijiji cha Nduli Iringa mjini 
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa  Jesca Msambatavangu akiwaaga  waombolezaji  leo 
 Waziri mkuu akiaganga na familia ya marehemu Chonaga  leo kijiji  cha Nduli Iringa mjini 

 Mtoto mkubwa wa marehemu Chonanga  akimuongoza waziri mkuu na msafara  wake  kuondoka  eneo hilo 
 Mwenyekiti  wa CCM mkoa wa Iringa akiwapa pore  wafiwa  
 Waziri Pinda akiwapa pore  wafiwa leo katika msiba wa  diwani wa kata ya Nduli mjini Iringa Idd Chonanga  aliyefariki dunia  jana 
 Ndugu  wa diwani Chonanga  wakiangana na  waziri mkuu Pinda 
 Waziri Pinda akiagana na famili ya  marehemu Chonanga leo 
 Mkuu  wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma kushoto akiwa na mke wa  waziri mkuu mama Tunu Pinda na viongozi wengine wa CCM mjini Iringa 
 Mwenyekiti  wa CCM mjini Iringa Abed Kiponza akimng'ata sikio mama Tunu Pinda 
 Familia ya  marehemu Chonanga akifurahia  baada ya  kutembelewa na waziri mkuu 
 Kamanda  wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas akiwapa pore  wafiwa  leo kamanda  huyo aliongozana na waziri mkuu Mizengo  Pinda  mlezi wa CCM mkoa wa Iringa leo 
 Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa  Salim Asas akiwa na familia ya Chonanga na  wakazi wengine wa Nduli leo 




 Msafara  wa  waziri mkuu Mizengo  Pinda  ukitoka  kuhani msiba wa diwani wa kata ya Nduli Idd Chonanga aliyefariki jana na kuzikwa  kesho kijijini hapo.
Viongozi mbalia  mbali ya  serikali ya chama tawala  mkoa  wa Iringa  wakiwa wamejipanga tayari kumpokea  waziri mkuu Mizengo Pinda ambae ni mlezi wa CCM mkoa wa Iringa  aliyetua Iringa kwa ziara ya kichama mkoani hapa , kutoka  kushoto ni mjumbe wa NEC Iringa mjini Bw Madenge, mjumbe wa NEC na mbunge wa Kilolo Prof Peter Msolla ,meya wa Iringa mjini Amani Mwamwindi, mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Bw Kiponza ,mwenyekiti wa CCM Iringa vijiji mama Mtafilalo na madiwani wa Iringa vijiji na kamada wa UVCCM mkoa Salim Asas  wa 8 kulia
Wahudumu wa Ndege  iliyomleta  waziri mkuu  wakijiandaa kuagana nae
Mwenyekiti  wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akimpokea  waziri mkuu Mizengo Pinda
Mkuu  wa wilaya ya  Iringa Dr Leticia Warioba  akimpokea  waziri mkuu
Mkuu  wa wilaya ya Mufindi Evarista kalalu akimpokea  waziri mkuu
Mkuu  wa wilaya ya  Kilolo Bw Gerald Guninita  akisalimiana na waziri mkuu
Ofisa wa magereza  Iringa akimpokea  waziri mkuu
Kamanda wa polisi wa mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi akisalimiana na waziri mkuu Mizengo Pinda ikiwa ni kwa mara ya kwanza toka alipoteuliwa  kuongoza mkoa wa Iringa kama kamanda wa polisi baada ya Michael Kamuhanda kupandishwa  cheo
kada wa CCM mzee My Studio akisalimia na  waziri mkuu
Jembe la manispaa ya Iringa mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa Teresia Mahongo akimpokea  waziri mkuu Mizengo Pinda  kwa tabasamu kali
Meneja  wa Tanroads mkoa  wa Iringa ambae anafanya makubwa katika  barabara ya Iringa - Dodoma Paul Lwakurwa akipongezwa na waziri mkuu kwa kazi nzuri
Makada wa CCM kutoka  vyuo  wakimpokea  waziri mkuu pichani na Bwana Alcard
Makada wa  CCM familia ya My Studio
Wadau  wa masuala ya utalii  mkoa  wa Iringa ambao  wanapigania kuitangaza  hifadhi ya  Ruaha na hifadhi za  kusini
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo JOseph Muhumba akisalimiana na  waziri Pinda
Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas akiteta jambo na  waziri mkuu Mizengo Pinda katika uwanja wa Ndege Nduli leo

Picha na habari na Francis Godwin

WAZIRI  mkuu wa jamuhuri ya muungano  wa Tanzania Mizengo Pinda ambae ni mlezi wa chama  cha mapinduzi (CCM) mkoa  wa Iringa jioni  ya  leo amewasili  mkoani Iringa na kufika nyumbani kwa   aliyekuwa diwani  wa kata ya marehemu Idd Chonanga na kuungana na  waombolezaji katika  kuifariji familia  ya diwani huyo.

Waziri  Pinda ambae  aliongoza na  mkewe mama Tunu Pinda na viongozi wengine wa CCM mkoa  wa Iringa pamoja na  viongozi wa  serikali ya  mkoa  wa Iringa wakiongozwa na mkuu wa mkoa  wa Iringa  Dr Christine Ishengoma  walifika nyumbani kwa  marehe mu Chonanga  eneo la Nduli  majira ya saa 10.56 na  kutumia muda wa zaidi ya  dakika  10 kuifariji  familia  hiyo.

Akiwa  nyumbani kwa marehemu  Chonanga  waziri  Pinda na mkewe wametoa  pore kwa familia  hiyo  ya Chonanga na  kuwaomba  kuendelea  kuwa na uvumilivu katika kipindi  hiki kigumu cha maombolezo na  kuwa  wao  katika  chama wapo pamoja na familia  hiyo katika maombolezo hayo .

Waziri  Pinda  amesema kuwa  binafsi kama mlezi  wa CCM mkoa  wa Iringa ameguswa na kifo cha  diwani Chonanga na kuwa kutokana na  kuwa katika  ziara ya kichama mkoa  wa Iringa ameona ni vema  kabla ya  kuanza  shughuli za chama  kufika  kuhani msiba  huo .

Kwa  upande  wake  mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu alisema  kuwa  CCM wilaya ya Iringa mjini na mkoa kwa ujumla  wamepata  pigo kubwa  kwa kifo  cha  diwani  huyo na  kusema kuwa  CCM itashiriki kwa  asilimia 100 mazishi  hayo yatakayofanyika mapema  kesho katika kijiji  hicho cha Nduli.

Kwa  upande  wake Greyson Chonanga ambae ni mtoto wa marehemu Chonanga  ameeleza  kufurahishwa na hatua ya waziri  mkuu  kufika  kuhani msiba  huo na  kuwa  wao kama familia hawakutambua  kuwa msafara mkubwa kama  huo wa kitaifa  ungefika kuhani msiba  huo.
Huku  wakazi  wa eneo hilo la Nduli  wameelezwa  kufurahishwa na umoja  wa kweli uliopo ndani ya  serikali ya  CCM kutokana na  viongozi  wake  kuwajali watu wa chini wanaowaongoza na  kuwa  utu ambao  waziri mkuu ameonyesha ni upendo tosha kwa wana Nduli kwa serikali ya  CCM.
Alisema Adam Kalinga mkazi  wa kata  hiyo ya Nduli ambae alikuwepo msibani hapo kuwa katika  kuenzi  kazi za marehemu Chonanga  wao wataendelea  kutambua mchango  wake .

1 comment:

Anonymous said...

Kupeana pole ni wajibu kwani hilo si ls mmoja tuko hapa duniani kwa muda tu sote ndo njia yetu hiyo. Mungu aiweke roho ya marehemu pema peponi.Ameen