Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Moshi
SERIKALI imeyashukuru makundi mbalimbali pamoja na viongozi wa mkoa wa
Kilimanjaro kufanikisha zoezi la kuzima moto katika hifadhi ya mlima
Kilimanjaro ulioteketeza zaidi ya ekari 40 katika eneo la Amboni .
Naibu waziri wa maliasili na utamaduni Lazaro Nyarandu ametoa pongezi
hizo leo wakati akiwapokea vikosi vya askari polisi wa chuo cha
taaluma ya Polisi cha mjini Moshi pamoja na asakari mgambo
walioshiriki zoezi hilo la kuzima moto.
Amesema serikali imefurahishwa na moyo wa kujitolea uliofanywa na
makundi hayo ya askari pamoja na watu wengine kwani wameonesha moyo
wa uzalendo wa kuijenga nchi yao na kwamba ushirikiano huo ndio
unaohitajika ili kutokomeza majanga mengine yote yanyo tokea katika
taifa.
Amesema usalama na ubora na kuwepo kwa uhifadhi wa mlima Kilimanjaro
utasaidia uchumi wa nchi pamoja na wapenda milima na mazingira duniani
kuona uoto wa asili na theruji ya mlima huo vikiendelea kuwepo.
Awali akiwasilisha taarifa kuhusu kuzuka kwa moto huo Mhifadhi mkuu wa
hifadhi ya mlima Kilimanjaro Erastus Lufunguro amesema KINAPA iliweka
kambi tano maalum kwa ajili ya kuhudumia waliokuwa wakishiriki zoezi
la kuzima moto.
Amesema moja ya kambi hizo ilikuwa eneo la Marangu kwa ajili ya
kuhudumia eneo la Kilema juu ambapo zote kwa pamoja zilikuwa na askari
mgambo 128 kutoka wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro sanjari na askari
54 waliopo mafunzoni katika chuo cha polisi CCP.
Vikosi vya askari mgambo na askari polisi ambao
ni wanafunzi wa chuo cha taaluma ya Polisi Moshi wakishuka kutoka
mlima Kilimanjaro ambako walikuwa wakifanya shughuli za kuzima moto
uliowaka jumapili ya Julai
Mchakamchaka
Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro
Nyarandu akiwasili katika viwanja vya ofisi ya hifadhi ya taifa ya mlima
Kilimanjaro KINAPA kuwapokea na kuzungumza na asakari walioshiriki
zoezi la kuzima moto mlima Kilimanjaro.
Askari walioshiriki zoezi la kuzima moto.
Kaimu mkurunzi wa hifadhi za taifa Martin
Loibook akizungumza wakati wa kuwapokea asakri walioshiriki kuzima moto
mlima Kilimanjaro.kushoto kwake ni naibu waziri wa maliasili na utalii
Lazaro Nayarandu na katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Issa Faisal.
Askari shujaa
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya mlima
Kilimanjaro Erastus Lufunguro akisoma taarifa mbele ya naibu waziri
wa maliasili na utalii,Lazaro Nyarandu.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya mlima
Kilimanjaro Erastus Lufunguro akimkabidhi naibu waziri wa maliasili
na utalii Lazaro Nyarandu taarifa kuhusiana na moto uliokuwa
ukiwaka mlima Kilimanjaro.
Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro
Nyarandu akizungumza na kundi la askari walioshiriki zoezi la kuzima
moto mlima Kilimanjaro
Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro
Nyarandu akizungumza na kundi la askari walioshiriki zoezi la kuzima
moto mlima Kilimanjaro
Wakuu wa vikosi vilivyoshiriki kuzima moto mlima
Kilimanjaro.
Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro
Nyarandu akiwapongeza askari walioshiriki kuzima moto Mlima
Kilimanjaro.
Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro
Nyarandu akizungumza na wafanyakazi wa hifadhi ya taifa ya mlima
Kilimanjaro.
Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akizungumza na viongozi wa askari mgambo
Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro
Nyarandu akizungumza na viongozi wa askari mgambo ,kushoto kwake ni
mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro Erastus Lufunguro.
Picha zote na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi
No comments:
Post a Comment