Monday, July 29, 2013

UWAKILISHI WA KUDUMU NEW YORK ULIVYO MUAGA BALOZI MERO

Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, mwishoni mwa wiki uliandaa hafla fupi ya kumuaga Afisa mwenza Bw. Modest Mero na Familia yake, Bw. Mero aliteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais Jakaya Kikwete kuwa Balozi wa Tanzania Geneva, hafla hiyo ilifanyika katika Makazi ya Balozi Tuvako Manongi yaliyoko 86 Jadison. zifuatato ni baadhi tu ya picha ya hafla hiyo iliyoambatana na nyama choma na chakula cha jioni.
Moja ya Zawadi ambazo wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa waliyomizawadia Bw. Mero kama kumbukumbu, kutoka kushoto ni Balozi Tuvako Manongi na mkewe Upendo, Balozi Modest Mero na mkewe Rose.
Balozi Modest Mero akitoa shukrani zake kwa niaba ya familia yake nyumayake ni watoto wake na aliyekaa kushoto ni Bw. Ken Kanda Balozi wa Ghana katika Umoja wa Mataifa.
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, akizungumza machache wakati wa hafla hiyo ambapo alimuelezea Balozi Mero kama mchapa kazi , anayejituma na wakati wowote alipohitaji au kuulizwa chochote alilkuwa tayari kukifanya au kujibu.
Balozi Modest Jonadhan Mero akiwa na Mke wake, Bibi Rose Mero.
Sehemu ya wageni waalikiwa waliojumuika katika hafla hiyo.
Balozi Mero akiwa na Afisa kutoka Ubalozi wa Uganda pamoja na mkewe wake.
Balozi Mero akiwa na Muwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi, Bw. Perfait Onanga-Anyanga akiwa na mkewe Annett.
Picha ya pamoja na maafisa na wafanyakazi wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

No comments: