Monday, July 29, 2013

Taarifa Fupi Juu Ya Hali Ya Usalama wa kimtandao

Mr. Yusuph Kileo (Cyber Security and Digital 
forensics Investigations Expert)
Na Yusuph Kileo.

Hivi karibuni kwa takriban miezi miwili kumekua na midahalo mbali mbali ambayo imekua ikiendelea katika nchi nyiingi na nimepata kuhudhuria kama mwanachama wa kudumu wa kikundi kinacho jihusisha na maswala ya Ulinzi mtandao katika nchi za Africa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyo wasilishwa na Profesa Hamadoun Toure kutoka ITU (International Telecommunication Union) iliyo chini ya United Nations (Umoja wa Kimataifa) ilisema kuna mategemeo mwishoni mwa mwaka huu wa 2013 pakawa na watumiaji biilioni 2.7 wa mtandao na kwa takwimu hizo zimeonyesha kupanda kwa kasi kulinganisha na takwimu za awali zilizotolewa mwishoni mwa mwaka jana katika mkutano ulio fanyika nchini afrika kusiini. Katika Vikao tofauti vilivyo kaliwa majadiliano yalikua ni mengi ambapo hali ya usalama wa kimtandao imechambuliwa kwa ngazi ya kidunia na kudhihirika ya kua kumekua na ongezeko kubwa katika mwaka huu wa 2013 la makosa mtandao, Hadi sasa nchi baadhi tayari zimeweza kupiga hatu katika kukabiliana na hali hiyo.

Aidha ripoti iliyowasiilishwa na ITU huko Geneva  ilisema, kumekua na ongezeko kubwa la madhara ya mtandao ambapo ilielezwa mitandao imekua ikiathiriwa zaidi kwa Asilimia 30, “Phishing Sites spoofing social networks” imeongezeka kwa asilimia 125 na kuelezwa nusu ya vijana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 17 uliimwenguni kote wamekua wakiathirrika na kilichotambulishwa kama “Cyberbulling”.

Vile vile Tafiti zilizo wasilishwa katika ripoti ya “the World Federation of Exchanges and the
International Organization of Securities Commissions”
zime eleza nusu ya taasis za fedha duniani zimeweza kuathirika na “Cyber-attacks” pamoja na wizi mtandao hadi kufikia mwaka jana mwishoni huku ikielezwa kushindikana kutatua hali hiyo kwa takriban robo nzima ya taasisi hizo za fedha dhidi ya tatizo hilo.

Hayo na mengine mengi ambayo yamepata kujadiliwa kwa kina yalionekana kuwa ni changamoto kubwa katika dunia ya sasa ambapo kutakua na ugumu sana kukimbia utumiaji wa teknologia katika maisha yetu yakila siku. Kwa sasa hali ya utumiaji wa mitandao kuongezeka nchini katika sekta mbali mbali kuanzia kufanya miamala ya biashara hadi katika sekta za elimu na maeneo mengine mengi.

Wimbi kubwa nchini limeongezeka la watu kuwa na matumizi mabaya ya mitandao ambapo imekua ikileta athari kubwa kwa jamii katika maeneo mengi hasa yaki biashara lakini pia hata kutishia hali ya usalama wanchi kwa kusambazwa maneno mbali mbali ya kutishia Amani ya nchi kwa kipindi kifupi tofauti na awali wakati matumizi ya mtandao hayakua na ongezeko lililoko sasa.

No comments: