Gari
Maalum la Hifadhi ya Kilimanjaro aina ya UNIMOG lililotengenezwa
Ujerumani linaloweza kuhimili njia ya kiutawala ya kufika hadi kituo cha
Kibo Mlimani Kilimanjaro.Wanahabari wakipanda gari hilo kwa ajili ya
kuelekea kituo cha Horombo kuangalia athari za moto.
Safari ikiendelea huku vumbi kubwa likitimka.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dk. Ibrahim Msengi (mwenye kofia nyeupe) alikuwa ndani ya UNIMOG kuelekea Horombo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiwa ndani ya gari kuelekea Horombo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama na ujumbe wake wakiwasili eneo la Horombo kukagua athari za moto.
Milima inayoonekana kwa mbali ndiyo iliyoungua na moto.
Mkuu
wa Hifadhi ya Kilimanjaro Erastus Lufungulo (kushoto) akisoma taarifa
ya moto kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama.
Mkuu wa Hifadhi akionyesha eneo lililoathirika na moto.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro akishika pande la barafu lililoganda eneo la
Horombo ambapo ni urefu wa Mita zaidi ya 3,700 juu ya uswa wa bahari.
Picha zote na mdau Pascal Shelutete
No comments:
Post a Comment