Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea ua mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama jijini Gaberone nchini Botswana kutoka kwa binti Jessica Kissasi, anayesoma darasa la pili, Baobab International School t arehe 29.7.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Bwana Christopher Castle,Mkuu wa Idara ya HIV and Health Education kutoka Makao Makuu ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yaliyoko Paris nchini Ufaransa wakati Mama Salma alipowasiri kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama huko Botswana tarehe 29.7.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipewa maelezo mafupi na Dr. Patricia Machawira, Mshauri Mkuu wa HIV and AIDS wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika muda mfipi kabla ya kuanza kwa mkutano wa “High Level Group-Action on comprehensive sexuality education and health services for adolescents and young people in Eastern and Southern Africa “ unaofanyika Gaberone nchini Botswana tarehe 30-31.7.2013.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa High Level Group wakisikiliza hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Mama Salma Kikwete
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia wajumbe wa mkutano wa sikuk mbili wa “High Level Group” kutoka Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaofanyika katika hoteli ya Lansmore Masa Square jijini Gaberone nchini Botswana.
Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania ( kulia kwenda kushoto) Dr. Kadija Mwamtemi, Mwanahamisi Kitogo, Mshauri wa Rais kuhusu masuala ya huduma za jamii, Ndugu Daud Nassib, Katibu wa WAMA foundation na Balozi wa Tanzania nchini Botswana mwenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini Mheshimiwa Radhia Msuya Mtengeti wakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Mama Salma tarehe 30.7.2013.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipongezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki Mheshimiwa Jesca Eriyo baada ya kufungua mkutano wa “High Level Group” huko Gaberone nchini Botswana terehe 30.7.2013.
Na Anna Nkinda- Gaborone, Botswana
Imeelezwa kwamba ndoa za utotoni ni moja ya sababu inayowafanya watoto wa kike kukatiza masomo yao huku asilimia 24 ya watoto hao wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 18 wakiolewa katika nchi zilizopo kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Kutokana na umri wao watoto hao walitakiwa kuwa wanafunzi wa shule za Sekondari na siyo kuishi na wanaume hivyo basi jitihada za pamoja zinatakiwa ili kuhakikisha kuwa sheria na sera za kumlinda mtoto wa kike na kumjengea mazingira salama ya kuishi zinatungwa.
Hayo yamesemwa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wajumbe waliohudhulia mkutano wa kamati maalum ya viongozi wanaoshughulikia huduma na elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka nchi za Jumuia ya Afrika ya Mashariki (EAC) na Jumuia ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kikanda kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika katika Hoteli ya Lansmore Masa Square iliyopo mjini Gabarone nchini Botswana.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa mkutano huo unafanyika kipindi ambacho jitihada kubwa zinafanywa na nchi wanachama wa EAC na SADC ili kuhakikisha kuwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na mimba za utotoni zinapungua.
“Taarifa ya Kanda inaonyesha kuwa Ugonjwa wa Ukimwi ni changamoto kwa vijana wetu kwani kati ya maaambukizi mapya 620,000 yanatokea kila mwaka kuna vijana wadogo wenye umri wa miaka 15hadi 24 kati ya hao asilimia 60% ni wasichana hii inamaana kuwa kwa saa moja wasichana 31 na wavulana 21 wanapata maambukizi”, alisema Mama Kikwete.
Alisema ili kukabiliana na tatizo hilo jamii inatakiwa kuhakikisha kuwa kuwa mtoto wa kike anapata elimu ingawa idadi ya watoto wa kike ni kubwa katika elimu ya msingi lakini wakifika elimu ya sekondari idadi yao inapungua.
Mama Kikwete alisema, “Ingawa kuna jamii zingine ni mwiko kwa wazazi kuongea na watoto wao kuhusu afya ya uzazi lakini watoto hawa wanatakiwa kufahamu afya ya uzazi na mabadiliko ya miili yao ili waweze kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi na mimba za utotoni”.
Alisema nchini Tanzania kupitia Taasisi ya WAMA kuna kampeni isemayo mtoto wa mwenzio ni wako mkinge dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi ambayo inaihamasisha jamii kuwalinda watoto pia taasisi hiyo inafadhili elimu ya sekondari kwa watoto ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi.
WAMA imejenga mabweni ya wasichana katika shule za Sekondari, kutoa vifaa vya maabara,huduma ya maji safi na kuhamasisha watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi pia kupitia klabu mbalimbali za wanafunzi mashuleni wametoa elimu ya uzazi na jinsia ili vijana waweze kujilinda na maambukizi ya HIV na kujikinga na mimba za utotoni.
Akifungua mkutano huo Prof. Alaphia Wright kutoka UNESCO alisema mambo watakayoyajadili yatapelekwa katika Serikali za nchi husika ili ziweze kuongeza msukumo wa kisera na kibajeti na kuhakikisha kuwa wanatatua changamoto za afya na uzazi zinazowahusu vijana.
No comments:
Post a Comment