Monday, July 8, 2013

MLANDIZI VETERANI YATWAA KOMBE LA HAMOUD CUP 2013

 Diwani wa Kata ya Mlandizi, Euphrasia Kadala  akikagua timu ya Mlandizi Veterani.
 Wachezaji wa timu ya Muungano wakisalimiana na wenzao wa Mlandizi Veterani kabla ya kuanza kwa mchezo.
 Mshambuliaji wa timu ya Mlandizi Veterani, Kindema Salum akitafuta mbinu za kumtoka kiungo wa timu ya Muungano, Shaban Juma katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa, uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mlandizi mkoani Pwani.
 Mchezaji wa Mlandizi Veterani akitmtoka mchezaji wa Muungano.
 Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa akifuatilia mchezo huo.
 Mchezaji wa Muungano akitolewa nje kwa staili ya aina yake baada ya kuumia.
 Mchezo wa kuvuta kamba ulipamba fainali hizo.
 Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa akiruka kamba
 Moja mbili tatuuuuuu
 Mashabiki wakiofuatilia mchezo huo.
 Ulinzi uwanjani hapo ulihimarishwa.
 Mwamuzi bora akipokea cheti na fedha taslimu kiasi cha sh. 50,000.
 Mashabiki.
 Diwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya Kibaha Vijijini, Mwajuma Denge akipokea zawadi ya khanga kutoka kwa mgeni rasmi baada ya kushinda katika mchezo wa kuruka kamba.
Timu ya soka ya Mlandizi Veterani ikiwa na kombe la baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi
Diwani wa Kata ya Mlandizi, Euphrasia Kadala akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Mlandizi Veterani, Norbet Mshiu baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mbunge wa Kibaha Vijijini, (Hamoud Cup 2013) uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mlandizi. Katikati ni Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa. 

Na Mwandishi Wetu, Mlandizi

TIMU ya Mlandizi Veterani juzi jioni ilifanikiwa kuwa mabingwa wa kwanza wa mashindano ya Kombe la Mbunge wa Kibaha Vijijini mwaka huu (Hamoud Cup 2013) baada ya kuifunga Muungano goli 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mtongani iliyoko Mlandizi mkoani Pwani.

Goli pekee katika fainali hizo zilizohudhuriwa na mashabiki mbalimbali wa jimbo hilo lilifungwa na Robert Mshiu katika dakika ya 47 ambapo mabeki wa Muungano walijichanganya na kumpa nafasi mfungaji aliyekuwa amesimama peke yake na kufunga bao hilo.

Wenyeji wa uwanja huo Muungano ndiyo walianza kwa kasi katika mchezo huo lakini washambuliaji wake mara kadhaa walikuwa wakipiga nje mipira na kuikosesha timu yao nafasi ya kufunga na hatimaye kumaliza wakiwa wapili kwenye mashindano hao.

Baada ya mchezo huo kumalizika, Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa, aliwakabidhi mabingwa zawadi ya kikombe na fedha taslimu Sh. 300,000 wakati Muungano walikabidhiwa Sh. 200,000.
Nafasi ya tatu katika mashindano hayo yaliyoanza Aprili 6, mwaka huu na kushirikisha timu 16 zinazotoka kwenye jimbo hilo ilichukuliwa na Mtongani ambayo iliifunga Mihande magoli 3-0 na hivyo kujipatia zawadi ya Sh. 100,000 kutoka kwa mbunge huyo wa CCM.

Kamati ya mashindano hayo iliitangaza timu ya Mihande kuwa ndiyo timu yenye nidhamu huku Joseph Sinde wa Super Academy akiwa ndiye kipa bora wakati Muhsin Mohammed aliyefunga magoli 16 aliibuka kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo na kila mmoja alipata zawadi ya Sh. 50,000.

Timu ya kuvuta kamba ya Mlandizi iliibuka kidedea dhidi ya wenzao wa Mtongani huku pia timu ya netiboli ya Mlandizi Queens ikipata zawadi kufuatia ushindi wao mara mbili dhidi ya Bongo Movie na Manzese Queens.
Mbunge Hamoud aliwashukuru mashabiki wote waliojitokeza katika fainali hiyo na tangu mashindano yalipoanza ambapo aliahidi kuiboresha hapo mwakani.
Pia aliwaelezea ataendelea kuwa karibu nao kutokana na heshima waliyompa na anaamini michuano hiyo imevumbua vipaji kwa ajili ya kupata wachezaji wa timu ya wilaya.

Mgeni rasmi katika mashindano hayo, Diwani wa Kata ya Mlandizi, Euphrasia Kadala, aliwataka wakati wa jimbo la Kibaha Vijijini kudumisha urafiki kupitia michezo ambayo pia husaidia kujenga afya.

No comments: