Mke wa waziri mkuu Mama Tunu Pinda ( wa tatu kushoto) akiwasikiliza viongozi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya TARWOC DROP-IN iliyopo Mkimbizi mjini Iringa pindi alipotembelea taasisi hiyo juzi wengine pichani ni viongozi wa taasisi hiyo akiwemo mkurugenzi wake Bi, Lediana Mng'ong'o ambae ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa wa tatu kushoto na wapili kushoto ni mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Terresia Mahongo
Siku mbayo shirika lilionyesha mfano kwa kutoa Baiskeli kwa Mbarozi wa Kata 20 wakisubiri kukabidhiwa usafiri wa Baiskeri, nje ya kituo cha shirika la TARWOC DROP IN.
Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki, akikabidhi Baiskeri kwa mabarozi wa Kata, kutoka Manispaa ya Iringa na Iringa Vijijini.
Baadhi ya mabarozi wakiwa na Baiskeri zao, baada ya kukabidhiwa rasmi na naibu Meya wa Manispaa ya Iringa
Pendo Luoga (kushoto) Meneja wa kituo cha TARWOC DROP IN- Mkimbizi na Benedict Kibiki (mwenye suti) Ofisa mkuu wa shirika la TARWOC DROP IN- Wakishangilia baada ya makabidhiano hayo.
Na FrancisGodwinblog-mzee wa matukio daima
MKE wa waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mama Tunu Pinda amepongeza jitihada mbali mbali zinazofanywa na kituo cha TARWOC DROP-IN cha mkimbizi katika Manispaa ya |Iringa kinachoongozwa mkurugenzi wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Lediana Mafulu Mng'ong'o kwa kazi nzuri
Mama Pinda alitoa pongezi hizi juzi baada ya kutembelea kituo hicho na kupokea pongezi nyingi kutoka kwa baadhi ya wanaume ambao walikuwa wakiongoza kwa unyanyasaji wa kijinsia kwa wake wao na wanawake waliokuwa wakinyanyasika na waume zao ambao kwa sasa wameungana na kuishi kwa amani.
Akitoa pongezi hizi kituoni hapo mama Pinda alisema kuwa jitihada zinazofanywa na m bunge Mng'ong'o katika kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia na kudumisha mausiano kwa wanandoa ni hatua ya kupongezwa na kila mtanzania na angetamani kuona vituo kama hivyo vinaanzishwa nchi nzima.
Tunu Pinda alisema kuwa suala la ukatili wa kijinsia kwa wanawake limeendelea kuchukua kasi kubwa na kuwa bila jitihada kama hizo za TARWOC katika kutoa elimu upo uwezekano wa watoto na wanawake kuendelea kunyanyasika zaidi.
Hivyo alisema kuwa ili Tanzania kuendelea kuwa nchi ya amani ni vema suala la amani likaanzia katika familia kwa wanandoa kujenga utamaduni wa kupendana na kuela familia badala ya kutengana na kusababisha familia kuishi katika mazingira duni.
Hata hivyo mama Pinda amekubali kuendelea kuwa karibu na kituo hicho ili kuwezesha kujulikana zaidi na kuipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa chini ya mkurugenzi wake Terresa Mahongo kwa kuendelea kuwa karibu na kituo hicho bora nchini Tanzania.
Kwa upande wake meneja wa kituo hicho Pendo Luoga alisema kuwa toka kituo hicho kimeendelea kupata mafanikio makubwa katika kuwasaidia watu wanaonyanyasika bila kujali wapi wanatoka .
Huku afisa mkuu kituo hicho cha TARWOC DROP- IN BenidickKibiki akizsema kuwa kituo chake kimehudumia zaidi ya waathirika 1500 wa unyanyasaji na ukatili wa kijisia, na tatizo kuu likiwa ni uwepo wa mila na destuli potofu, uchumi mdogo pamoja na unywaji wa pombe.
"Tatizo hili linatokana na baadhi ya mila na destuli zetu zilizopitwa na wakati, hasa kwa hili la kujiona sisi wanaume kama ndiyo kila kitu, lakini suala la uchumi nalo linachangia ukatili na unyanyasaji, mtu mwanaume au mwanamke mwenye kipato duni anafanyiwa unyanyasaji kutokana na hali yake duni, la tatu ni kukosekana kwa elimu miongoni mwa jamii, kwani baadhi ya wananchi hawana elimu ya namna ya unyanyasaji," Alisema Kibiki.
Aidha aliongeza kuwa changamoto inayokikabili kituo hicho cha TARWOC DROP- IN cha Mkimbizi ni kukosekana kwa ausafiri wa gari, na hivyo kushindwa kuwafikia wananchi waishio maeneo ya mbali na kituo.
Kibiki alisema Kata 16 zilizopata baiskeri hizo ni kutoka ndani ya Manispaa ya Iringa huku Kata 4 za Iringa vvijijini ambazo ni Kata ya Mseke, Ifunda, Kihologota na Kata ya Kising'a.
Huku viongozi wa serikali ya mtaaa huo wakudai kuwa hatua ya kituo hicho kukabidhi usafiri kwa mabalozi ni kusaidia kupingana na ukatili Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bi Mahongo alisema kuwa jitihada zinazofanywa na kituo hicho zimeivutia halmashauri hiyo hivyo wamelazimika kutoa ardhi zaidi ili kujengwa kituo kikubwa kitakachowezesha huduma hiyo kuboreshwa zaidi.
Kwa upande wake mbunge Mng'ong'o mbali ya kump;ongeza mama Pinda bado alisem akuwa lengo lake ni kuhakmikisha mkoa wa Iringa na Tanzania kunakuwepo amani na hakuna mwanake wala mtoto anayenyan yasika.
No comments:
Post a Comment