Na Mwandishi Maalum
Baraza Kuu la Usalama
la Umoja wa Mataifa, jana jumatano liliendesha majadiliano ya wazi
kuhusu usalama wa waandishi wa habari katika
maeneo yenye migogoro.
Majadiliano hayo yaliratibiwa na Marekani ambaye
ni Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa
Julai, na kuhudhuriwa na waandishi wanne wa kimataifa ambao
walipata fursa ya kuelezea
masahibu wanayokumbana nayo wakati wa
kitekeleza majukumu yao.
Majadiliano kuhusu
suala la usalama wa waandishi wa habari katika maeneo yenye migogoro ni
ya kwanza kufanyika ndani ya Baraza
hilo, tangu lilipopitisha Azimio namba
17 38 mwaka 2006 lililokuwa likizungumzia
suala hilo. Aidha hii pia ni mara ya kwanza kwa waandishi wa kimataifa
kuzungumza ndani ya Baraza Kuu la Usalama.
“ Hapa nilipo
mimi ni maiti anayetembea , ninatembea
pasi kujua nani anaweza kuondoa
uhai wangu,wakati wowote naweza kupotea maisha. naweza kuuawa
hata na kijana mdogo ilimradi
ana silaha”
Kauli hiyo ilikuwa ni ya Bw. Mustafa
Haji Abdinur anayeandikisha AFP akitoka
Somalia. Na kuongeza kwamba rafiki zake
wengi ambao ni waandishi wenziye tayari
wameshapotea maisha na kwamba kwa
yeyé kuwa hai mpaka sasa ni kama bahati
lakini ni suala la wakati tu.
Naye Bi. Cathleen Carrol ambaye ni
Mhariri Mtendaji wa Associated Press na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Kamati ya Kuwalinda Waandishi ( CPJ) pamoja na
kuelezea kwa uchungu mkubwa matukio ya mauaji yaliyowakumbua waandishi
wenzake katika maeneo mbalimbali
duniani anasema, katika shirika lao
kuna eneo ambalo limetengwa
maalum kwaajili ya kuwaenzi waandishi wote ambao wamepoteza maisha katika
utekelezaji wa majukumu yao.
Kwa
upande wake, mwandishi Richard Engel wa
NBC news, yeyé pamoja na kuelezea mikasa
mbalimbali ambayo amekwisha kumbana nayo
yakiwamo ya kutekwa wakati akiripoti matukio ya migogoro, yeyé alikwenda mbalia
zaidi kwa kuuliza ni nani hasa mwandishi wa habari.
Bw,
Engel alieza kwamba ulinzi wa waandishi wa habari hivi sasa unakuwa mgumu sana tofauti na miaka ya nyuma kutokana na kile alichosema kuibuka
kwa makundi mengi yanayofanya kazi za waadishi wa habari.
“
Wakati tukijadili hoja hii ya usalama wa waandishi wa habari, pengine pia ni
muhimu tukajiuliza hivi ni nani hasa mwandishi wa habari,
je mwanaharakati anaye shika
video au kamera na kalamu je naye
ni mwandishi, au je na yule mwanamgambo mwenye silaha lakini naye
ameshika kamera na kupiga picha je naye
ni mwandishi” akahoji Bw, Engel
Anasema
kwamba ni jambo la kawaida hivi
unapokwenda kwenye tukio fulani
kukutana na makundi ya watu kila mmoja akiwa ameshika kamera yake
akichukua matukio, na katika mazingira kama haya, ni vigumu kwa vyombo vya ulinzi na usalama kutofautisha nani hasa ni mwadishi aliyesomea
na kubobea kwenye fani hiyo na yupi mwanarakati.
Kwa
maoni yake anasema pamoja na hamu ya kila mtu kutaka kutaka kukukusanya
habari na kuzisambaza kupitia mitandao ya kijamii, ni vime kujiuliza nani anastahili na anapwashwa kupewa ulinzi anapotimiza
majukumu yake na kwa vyovyote vile anasema kama ilivyo kwa wanadiplomasia ambao
wanakinga vilevile waandishi waliosomea na wenye weledi na taaluma yao
wanatakiwa kupewa ulinzi.
Majadiliano
hayo yalifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson, na yalikuwa na mvuto wa ina yake hasa kutoka na kauli zilizokuwa zikitolewa na
baadhi ya wachangiaji.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu alieleza kwamba hujuma dhidi ya waandishi wa habari ni jambo
lisilokubalika kwa kile alichosema ni kubinya
uhuru wa upatikanaji na utoaji wa
habari, lakini pia ni ukiukwaji wa uhuru wa kujieleza. Akalipongeza Baraza kwa kuitisha mjadala huo
Akasema karne iliyopita waandishi wa habari wapatao
600 walipoteza maisha katika matukio mbalimbali
na wengine wakiishia magerezani, huku asilimia 90 ya matukio hayo hakuna
hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa.
Pamoja
na wachangiaji wengi kukiri kwamba
mazingira ya ufanyaji kazi kwa
waandishi wa habari yamezidi kuwa magumu
na hatari, walielezea pia kwamba mazingira hatarishi hayapo tu katika maeneo yenye vita bali hata katika nchi wazofanyia kazi. Ambapo
takwimu kutoka CPJ zinaonyesha katika kila waandishi watano kati ya sita wanauliwa wakiwa ndani ya
nchi zao.
Wengi
wa wazungumzaji walieleza kwamba baadhi
ya waandishi ama wamekuwa wakitishiwa maisha yao na familia zao au hata kupoteza maisha kwa kuandika na kuchapicha habari zinazofichua vitendo vya rushwa , vitendo vya jinai au
kashfa zinazohusu makundi mbalimbali ya jamii na vilevile kuandika habari za uchochezi kati ya
kundi moja na jingine..
Wengine
wakaenda mbali kwa kusema wakati
mwingine waandishi wenyewe wanajiweka katika mazingira ya hatari kwa kukiuka
misingi ya kazi zao, kwa kuandika habari zinazopendelea upande mmoja, au kufanya kazi kinyume cha matakwa na matarajio ya yule anayemfanyia
kazi.
Wazungumzaji
hao wakatoa wito kwa Baraza kuu la
Usalama kuangalia namna bora ya
kuboresha ulinzi wa waandishi wa habari katika mazingira hatarishi kama vile vita na migogoro na pia
wakatoa wito wito kwa waandishi wa
habari kuzingatia misingi ya taaluma zao
na kuepuka kujingiza katika mitengo isiyo ya lazima.
Suala
lingine lililozungumwa kwa kina ni lile
la kutofikishwa mbele ya mkono wa sheria watu wanaotuhumiwa kuwahujumu waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment