Kaimu katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu Tamisemi,Jumanne Sageni akitoa
hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha halmashauri za
miji 18 Tanzania bara uliofanyika mjini Moshi.
Mwakilishi wa benki ya dunia,mkurugenzi mkazi Philippe Dongies akitoa
hoyuba yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha halmashauri za
miji 18 Tanzania bara uliofanyika mjini Moshi.
Washiriki wa warsha hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Hawa Ghasia akitoa
hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha halmashauri za
miji 18 Tanzania bara uliofanyika mjini Moshi.
Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia washiriki wa warsha ya uzinduzi
wa mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 Tanzania bara
uliofanyika mjini Moshi.
Washiri wa warsha hiyo.
Waziri mkuu Mizengo Pinda akikata utepe katika vitabu kuashiria
kuzinduliwa kwa mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 Tanzania
bara,Uzinduzi huo uliofanyika mjini Moshi.Kushoto ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Hawa Ghasia na kulia ni Mwakilishi wa
benki ya dunia,mkurugenzi mkazi Philippe Dongies wakishuhudia.
Waziri mkuu Mizengo Pinda akionesha makablasha kuashiria kuzinduliwa
kwa mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 Tanzania bara,Uzinduzi
huo uliofanyika mjini Moshi.Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu Tamisemi, Hawa Ghasia na kulia ni Mwakilishi wa benki ya
dunia,mkurugenzi mkazi Philippe Dongies wakishuhudia.
Washiriki katika picha ya pamoja.
Waziri mkuu akisalimiana na mmiliki wa ukumbi wa Moringe hall uliopo
mjini Moshi ambako kumefanyika uzinduzi wa mradi wa kuimarisha
halmashauri za miji 18 Tanzania bara.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi
SERIKALI imesema tatizo la ufuatiliaji wa karibu wa miradi
iliyoibuliwa na halmashauri za wilaya nchini sanjari na utekelezaji
wake ndio chanzo cha ubadhirifu na matokeo mabaya katika utekelezaji
wa miradi hiyo kwa baadhi ya halmashauri.
Hayo yameelezwa jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi
wa mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 Tanzania bara
iliyofanyika katika ukumbi wa Moringe katika manispaa ya Moshi.
Waziri mkuu Pinda alisema katika mradi huo serikali kuu itahakikisha
inaufuatilia kwa karibu na ili kujenga imani kwa wananchi na wafadhili
wa mradi huu ambao ni benki ya Dunia na kwamba iwapo miji hiyo
itatekeleza mradi huo vizuri na kwa viwango vinavyotakiwa, serikali
itapata nguvu ya kufanya mazungumzo ya namna ya kuiangalia miji
mingine.
Alisema mafanikio ya mradi huo utaongeza matumaini kwa wananchi na pia
kuwavutia wadau wengine kushirikiana na halmashauri za hapa nchini
katika kuteleza miradi ya kimaendeleo, ambapo pia alitoa rai kwa
wakurugenzi wa halmashauri zilizoko kwenye mradi huo kutosita kuomba
ushauri pale itakapoonekana kuna vikwazo katika kuutekeleza.
“Mradi huu unatuhusu sote, halmashauri na wananchi, kila mtu awajibike
kulipa kodi zinazotakiwa kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri zetu na
kuwezesha utoaji wa huduma nyingine ikiwemo utunzaji wa mradii huu
katika halmashauri zote husika”, alisema Pinda.
Waziri Mkuu Pinda aliendelea kusema kuwa kuteuliwa kwa Tanzania kuwa
nchi ya kwanza Barani Afrika kufanya majaribio ya mfumo wa miradi ya
aina hiyo inaonyesha dhahiri jinsi Tanzania inavyoaminika na kusifika
kimataifa na kwamba ni vyema mradi huo ukatekelezwa vizuri ili
kuilinda heshima hiyo.
“Mkishindwa nyinyi ni kwamba Tanzania imeshindwa, hivyo serikali
haitakuwa tayari kusikia visingizio wala sababu zozote zitakazolenga
kukwamisha kazi hii njema”, alisema Pinda.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Hawa
Ghasia, amesema mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha
miaka mitano ijayo na kuleta mabadiliko makubwa Tanzania.
Ghasia amesema mradi huu utazihusisha halmashauri za Morogoro,
Tabora, Moshi, Sumbawanga, Shinyanga, Songea, Singida, Musoma, Iringa,
Njombe, Lindi, Bukoba, Kibaha, Babati, Geita, Korogwe, Mpanda na
Bariadi .
Naye Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, hapa nchini Philippe Dangier,
alisema benki hiyo imeipa Tanzania mkopo wa Dola za Marekani 255
milioni zitakazotumika katika kutekeleza mradi huo unaotarajiwa
kukamilika mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment