Monday, June 3, 2013

The Mboni Show yaadhimisha mwaka mmoja kwa kutoa msaada wa vifaa vya matibabu Amana hospital

 Keki iliyoandaliwa maalum kwa Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Kipindi cha The Mboni Show ikiwa katika mkao wa kukatwa.
 Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa (pili kulia),Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana,Dkt. Meshack Shimwela (kulia) Muendeshaji wa kipindi cha The Mboni Show,Mboni Masimba (katikati),Mama wa Mboni Masimba (kushoto) pamoja na Binamu wa Mboni wote kwa pamoja wakishirikiana kukata keki ikiwa ni ishara ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuwanzishwa kwa kipindi cha The Mboni Show, ambapo walifika katika Hospitali ya Amana Ilala jijini Dar na kutoa msaada wa vifaa mbali mbali vya matibabu.
 Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa akisisitiza jambo mbele ya wageni mbali mbali waliofika kwenye hafla hiyo ya kutimiza mwaka mmoja ya kipindi cha The Mboni Show,iliyofanyika kwenye Hospitali ya Amani jijini Dar es Salaam ikiwa ni sambamba na kutoa vifaa vya matibabu pamoja na kupaka rangi katika wadi ya kinamama.
 Muendeshaji wa kipindi cha The Mboni Show,Mboni Masimba akitoa maelezo machache ya namna alivyoweza kufanikisha zoezi hilo.
 Makabidhiano ya baadhi ya vifaa hivyo vya matibabu kwa Mganga wa Hospitali ya Amana,Dkt. Meshack Shimwela huku Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa akishuhudia. 
 Sehemu ya vifaa hivyo. 
 Msanii Mad Ice akiimba moja ya nyimbo zake kwenye hafla hiyo.
 Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa (kati) akimuonyesha kitu kwenye Mganga wa Hospital ya Amana,Dkt. Meshack Shimwela.
 Mama Mboni Masimba na wadau wengine.
 Wadau wa EATV.
 Wadau wengi tu walikuwepo kwenye zoezi hilo.
 Zoezi la kupaka rangi wadi ya kina mama katika Hospitali ya Amana likiendelea.
 Mboni,Mad Ice na Mwasit wakiwa pamoja kwenye picha wakati wakiendelea na zoezi la upakaji rangi kwenye wadi ya kina Mama katika Hospitali ya Amana.

 Mboni katika picha ya pamoja na wadau mbali mbali. 
Mboni Masimba (kati),Mie pamoja na Mdau.

No comments: