Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi
SERIKALI imetoa wito kwa mamlaka ya mawasliano Tanzania TCRA kuangalia
namna ya kupata mbinu mpya za kisasa katika kudhibiti wale wachache
wanaojaribu kutumia teknolojia hiyo kuvunja umoja ,amani na utulivu.
Kauli hiyo ilitolewa jana na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama
wakati wa semina ya siku moja iliyowashirikisha wakuu wa mikoa fanyika
katika hotel ya Sarsalenero iliyopo mjini Moshi na kuwashirikisha
wakuu wa mikoa pamoja na makatibu tawala wa mikoa ya
Arusha,Tanga,Manyara na Kilimanjaro.
Gama alisema matummizi mabaya ya teknolojia ya mawasiliano sanjari na
uwepo wa tovuti na Wavuti zinazo kiuka kuharibu mila,destuli na
maadili ya mtanzania ni miongoni mwa changamoto zinazo ikabili sekta
hiyo kwa sasa .
Alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii na
simu za mkononi katika kueneza fitna,chuki,matusi na uhasama miongoni
mwa jamii ya watanzania jambo ambalo alisema TCRA inapaswa kuengalia
eneo hilo kwa makini zaidi ili mitandao hiyo isije ikatumika katika
kuwagawa watanzania.
Alisema ukuaji wa shughuli za kiuchumi zinazohusiana teknolojia ya
mawasiliano ya habari zinaongezeka kwa kasi kubwa kanda ya kasikazini
na kuwa kichocheo kikubwa katika sekta za Kilimo ,utalii na biashara
katika mikoa ya kanda ya kaskazini sambamba na kupatikana kwa fursa
mpya za ajira.
Awali akieleza malengo ya semina hiyo naibu mkurugenzi wa shughuli za
kanda wa TCRA, Victor Nkya alisema mamlaka ya mawasiliano imelenga
kujitangaza na kuwaelimisha wakuu wa mikoa juu ya shughuli za mamlaka
hiyo ili kutambua haki na wajibu kama watumiaji wa mawasiliano.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA ikiwahusisha wakuu wa mikoa na makatibu
tawala wa mikoa ya Manyara,Tanga,Arusha na Kilimanjaro.
Meneja wa mamlaka ya mawasiliano kanda ya kaskazini mhandisi Aneti Matindi akiteta jambo na injinia wa masafa wa TCRA ,Sadath Kalolo wakati wa semina ya wakuu wa mikoa ya kanda ya kaskazini.
Meneja wa mamlaka ya mawasiliano kanda ya kaskazini mhandisi Aneti Matindi akiwasilisha mada wakati wa semina ya wakuu wa mikoa ya kanda ya kaskazini.
Mkuu wa mkoa wa ManyaraEraston Mbwilo akichangia mada katika semina hiyo
Semina ya TCRA kwa wakuu wa mikoa ya kanda ya kaskazini.
Naibu mkurugenzi wa shughuli za Kanda wa TCRA Victor Nkya akiwasilisha
mada katika semina hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Chiku Gallawa pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mwilongo wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa wakati wa semina iliyoandaliwa na TCRA kwa wakuu hao wa mikoa ya kanda ya ksakazini.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mwilongo akichangia mada katika semina hiyo.
Meneja mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano TCRA wa kanda ya kaskazini Innocent Mungi akitoa mada katika semina hiyo.
Washiriki katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment