Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (aliyevaa miwani katikati), akifuatwa na wananchi baada ya kumaliza mkutano wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni.
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akimsikiliza Mweka Hazina wa Kikundi cha Kuweka na Kukopa (VICOBA), Anjela Ndigula ambaye alipokea sh. 50,000 alizotoa msaada kwa Muya Thabit ili ajiunge na kikundi hicho, baada ya kuambiwa hana haki hivyo anashindwa kulipia pango. Msaada huo aliutoa katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni.
Muya Thabit akicheza kwa furaha baada Mbunge Mtemvu kumsaidia fedha za kujiunga na vicoba
Diwani wa Kata ya Temeke, Khamis Nsombo, akiwazawadia fedha wasanii wa kikundi cha Msimamo
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akikizawadia fedha kikundi cha sanaa cha Msimamo kilichokuwa kinatumbuiza katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni. Pia aliahidi kukipatia kikundi hicho sh. 500,000 za kununulia vifaa zikiwemo ngoma.
Mtemvu akiangalia wakati msanii wa Msimamo akicheza ngoma
Wasanii wakicheza ngoma ya Lizombe ya asili ya Mkoa wa Ruvuma
Msanii akichangamsha mkutano huo
Mtemvu akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Temeke, Khamis Nsombo
Nsombo akiteremka kutoka jukwaani baada ya kuhutubia
Mtemvu akiwasalimia wananchi
Muya Thabit akiomba fedha kwa Mbunge Mtemvu ili alipe pango
Wananchi wakiuliza maswali kwa Mbunge wao Mtemvu
No comments:
Post a Comment