Thursday, June 13, 2013

BENKI YA KCB TANZANIA IMESEMA ITAENDELEA KUFANYA KAZI KWA KARIBU NA WAFANYABIASHARA WAKITANZANIA

Mkurugenzi wa huduma za kibenki kwa wateja wakubwa wa Benki ya KCB Tanzania Frank Nyamundege akitoa mada juu ya huduma za benki hiyo wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania Moezz Mir akiwahutubia wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
Mwenyekiti wa bodi ya Benki ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa (kushoto) akibadilishana mawazo na mjumbe wa bodi Nehemiah Mchechu (katikati) pamoja na mkuu wa kitengo cha sheria na katibu wa benki hiyo Edward Lyimo, muda mfupi kabla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi wa bodi ya benki ya KCB Tanzania Zuhura Muro akibadilisha mawazo na Chitrl Mallawarachchi ambaye ni mteja wa benki hiyo wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
Wasanii wa kikundi THT wakiwaburudisha wateja wa Benki ya KCB Tanzania wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi wa bodi ya Benki ya KCB Tanzania Zuhura Muro (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Moezz Mir (katikati) wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam juzi. Kustoto ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa wa benki hiyo Frank Nyamundege.


Picha ya pamoja.

BENKI ya KCB Tanzania imesema itaendelea kufanya kazi kwa karibu na wafanyabiashara wakitanzania wa ngazi zote ili kuwawezesha kukuwa kupitia huduma zake mbalimbali za kifedha.

Akizungumza wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam juzi, mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Moezz Mir alisema benki yake imedhamiria kusadidia maendeleo ya Tanzania kupitia huduma zake za kifedha na za kijamii.

Mir alisema Tanzania ina idadi kubwa ya watu kuliko nchi nyingine za Afrika mashariki ikiwa ni pamoja na ukuwaji wa pato la ndani wa asilimia 6.9 kwa mwaka 2012 pamoja na mali asili nyingi na kusisitiza kuwa nafasi za uwekezaji zinaendeleo kuongezeka kila kukicha.

Aliongeza kuwa, kwa miaka kadhaa, benki ya KCB imekuwa ikiwawezesha wateja wake waliopo katika eneo la Afrika ya mashariki kwa huduma mbalimbali za kifedha zinazoendana na mahitaji yao.

"Huduma zetu zipo za aina mbalimbali ambazo zimebuniwa kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wateja wetu ambao ni pamoja na watu binafsi, wafanya biashara wadogo na wa kati, asasi zisizokuwa za kiserikali na makampuni. Huduma tunazotoa ni pamoja na akaunti za akiba, mikopo ya nyumba, akaunti za uwekezaji, akaunti kwa ajili ya asasi za kijamii na nyingine, alisema.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa, benki ya KCB ndiyo kubwa kuliko zote katika eneo la Afrika ya mashariki ikiwa na rasilimali zenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 4.3 na mtandao wa matawi 226 huku ikienedela kukuwa.

Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo Dr Edmund Mndolwa alisema kutokana na uwezo mkubwa wa kifedha benki yake ipo katika nafasi nzuri ya kutoa mikopo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa.

Aliongeza kuwa, kwa kutumia uwezo wa kifedha wa benki hiyo pamoja na kushirikiana na vyombo mbalimbali vya serikali za Afrika ya mashariki benki hiyo itatoa mikopo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali mikubwa ya serikali za nchi za Afrika Mashariki kwa ajili ya manufaa ya wananchi wan chi hizo.

No comments: