Sunday, May 5, 2013

Wizara ya sayansi yajivunia mafanikio iliyopata


Katibu mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Techinojia Dkt. Forens Turuka (katikati) akisisitiza jamboa baada ya kumkabithi kitabu cha Majukumu na Mafanikio ya Wizara hiyo toka kuanzishwa kwake mpaka mwaka 2011, Mwenyekiti wa Taifa wa Tughe Dkt. Diwani Mruttu(wa pili kulia).Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Raslimali watu Bi Mazoea Mwera kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi ulifanyika mwishoni wa wiki jijini Dare s Salaam.
Katibu mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Techinojia Dkt. Forens Turuka (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo mwishoni mwa wiki. Mwenyekiti wa Taifa wa Tughe Dkt. Diwani Mruttu ( wapili kulia), Watatu kulia kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Utumishi , Bi. Mazoea Mwera.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Techinolojia imesema imeweza kutekeleza majukumu yake makubwa kwa ufanisi mkubwa katika mwaka wa fedha uliopita hivyo kuwapongeza wadau na wafanyakazi wake kwa kufikia malengo.

Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Technolojia Pof.Makame Mbarawa amewapongeza wafanyakazi wa Wizara hiyo kwa kazi nzuri waliyoifanya kupita Mkutano wa Baraza la wafanyakazi la Wizara hiyo .

“Suala la bajeti ndogo halikuwa kikwazo kwa wafanyakazi kutekeleza majukumu yao na akawataka kuendelea na moyo huo wa kutumia rasilimali kidogo zilizopo kwa ufanisi mkubwa,” alisema Prof.Mbarawa katika hotoba yake iliyomwa na Katibu Mkuu katika Wizara hiyo Dk. Florens Turuka kwenye Baraza la Wafanyakazi mwishoni mwa wiki.

Amesema vizara imeweza kutekeleza kwa mafanikio makubwa malengo iliyojiwekea pamoja na kuwepo kwa changamoto zilizojitokeza na kusema maeneo ambayo yalileta changamoto katika utekelezaji wake kuwa yatafanyiwa kazi katika mwaka wa fedha unaoanza. Amesema baraza ndio chombo cha uwakilishi wa wafanyakazi wa Wizara kwahiyo chochote kikienda hovyo katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara baraza la wafanyakazi ndilo litawajibika kujibu maswali toka kwa menejimenti.

Amewataka wafanyakazi kuwa na moyo wa kujituma na akasisitiza kuwa kupitia kauli mbiu ya “kwa dhamira ya kweli,uwajibikaji wa kweli,yote yanawezekana” mengi yameweza kufanyika.

Ameyataja baadhi ya maeneo ambayo wizara inajivunia kuyatekeleza kwa ufanisi kuwa ni eneo la kufungwa kwa mkongo wa taifa ambao umepunguza gharama za kuunganisha simu tioka mtandao mmoja kwenda mwingine hivyo kuwapunguzia wateja mzigo wa kutembea na simu zaidi ya tatu.

Eneo lingine ni kuanzishwa kwa timu maalum ya kudhibiti mawasiliano kwenye komputa ili kudhibiti watu wenye nia mbaya ambao wanaingilia mitandao ya wenzao na kufanya mambo yasio na heshima kwa jamii.

Ametaja kuanzishwa kwa Taasisi ya Techolojia ya Nelson Mandela ambacho ni moja kati ya Chuo bora katika afrika chenye mlengo wa kuibua wanasayansi bora ambao wataweza kubadili sura ya taifa kimaendeleo kutokana na elimu waliyoipata.Suala la utambuzi wa makazi pamoja na anuani za makazi hayo nalo limetajwa kuendelea vizuri.

Wakati huo huo,Mwenyekiti wa Tughe Taifa Dkt Diwani Mruttu amewataka wafanyakzai wa wizara hiyo kuendelea na moyo wa kujituma kufwatia unyeti wa sekta wanaoiongoza.

Amesema watu wengi hawaoni umuhimu wa wizara hiyo ila siku simu zote zikizima kwa mda wa saa moja ndipo watu wanaweza kuona umuhimu wa wizara hiyo.”Kama simu zingezimwa siku ya mgomo wa madaktari mwaka jana ata mgomo usingekuwepo……,tungeratibu vipi mgomo huo bila mawasiliano?”alihoji.

Amewataka wafanyakazi kuwa na utamaduni wa kujifanyia tahthimini ya kile wanachokifanya ili kuweza kugundua mapunguafu na kuchukua hatua haraka.

Amewaasa wafanyakazi kuwa na utamaduni wa kupima afya zao na wasingoje mpaka wajisikie kuumwa ndio waendendee hospitali kwani kufanya hivyo kutosimamisha kazi za wizara hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya wizara hiyo.

No comments: