Wednesday, May 1, 2013

WANAMUZIKI WANAOWANIA TUZO ZA KILI MUSIC AWARDS 2013 WAPIGWA MSASA LEO

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wanamuziki walioingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa New World Cinema,Mwenge,jijini Dar es Salaam.
Mdau wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013,Taji Liundi akitoa maelezo ya kina namna mchakato wa Academy ulivyofanyika na mpaka kuwapata washindani walioingia kwenye kinyang'anyiro hicho,wakati wa semina ya siku moja kwa wanamuziki watakaowania tuzo hizo, iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa New World Cinema,Mwenge,jijini Dar es Salaam.
Taji Liundi akiendelea kusisitiza jambo kwa wanamuziki hao.
Muwakilishi wa Kampuni ya Inovex akifafanua jambo kwa wanamuziki hao wakati wa semina ya siku moja kwa wanamuziki watakaowania tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013, iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa New World Cinema,Mwenge,jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa Kundi la TMK Wanaume Family,Said Fella akiuliza swali kwa Wadau wa wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013.
Mkongwe wa Muziki wa Miondoko ya Mwambao (Taarab) hapa nchini,Khadija Koppa akiuliza swali lake lenye kutaka kufahamu kwamba kwanini Bendi ya TOT haijawahi kuingizwa kwenye kinyang'anyiro cha Tuzo hizo na wakati yeye amekuwa akiingia mara nyingi?
Produza Man Water akiuliza swali.
Isha Mashauzi nae akifunguka kwa namna yake.
Nikki wa Pili.
Barnabas Elias akichangia mada.
Ney wa Mitego
Sehemu ya washiriki wa Semina hiyo ya siku moja ya wanamuziki walioingia kwenye kinyang'anyiro cha Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013  iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa New World Cinema,Mwenge,jijini Dar es Salaam.

No comments: