Tuesday, May 14, 2013

Vodacom yazidi kuimarisha huduma zake vijijini


Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Elius Nyakia akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara mpya wa Vodacom katika kijiji cha Lukanga Wilaya ya Misungwi. Anaemsaidia kukata utepe huo ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa Herieth Koka. Wanaoshuhudia uzinduzi huo kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim, Mwenyekiti wa Kijiji cha Lukanga Bw Enos Malale na Meneja wa Vodacom Foundation Mwamvua Mlangwa. Kabla ya Vodacom kujenga mnara huo, kijiji hicho hakijawahi kuwa na huduma za uhakika za simu za mkononi.
Wakazi wa kijiji cha Lukanga wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza pamoja na wa maeneo mbali mbali nchini wameendelea kunufaika na teknolojia ya simu za mikononi ikiwemo kupunguza gharama za maisha baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kuendelea kuyafungua na kuyaimarisha kimawasiliano maeneo yao.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Vodacom ilizindua rasmi huduma zake katika kijiji hicho kufuatia kujengwa kwa mnara mpya ambapo kabla ya hapo wakazi wa kijiji hicho na vijiji vya jirani ikiwemo kijiji cha Ishokera maarufu kwa shughuli za uchimbaji madini hawakuwa na huduma za uhakika za mawasiliano ya simu za mkononi na hivyo kuwalazimu wananchi kusafiri au kulazimika kuvizia mawimbi ya mawasiliano kwa baadhi ya nyakati.

“Tunafuraha kubwa sana leo hapa kijijini, sio ya kuwa na wageni bali kuona nasisi wana Lukanga tukiingia kwenye historia ya kuwa na mnara wa simu unaotupa huduma za uhakika za simu za mkononi,.”Alisema Mwenyekiti wa Kijiji cha Lukanga Bw. Enos Malale wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mnara huo.

“Hatuna tena sababu ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za simu z amkononi au kupanda juu ya vichuguu na milima kupata huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi kwani Vodacom sasa imetuleletea mawasiliano sebuleni na vyumbani kwetu.” Aliongeza

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa ilikuwa ndoto kwao kuweza kuunganishwa kimawasiliano na sehemu nyingine kwa muda mrefu. “hivyo basi kwa niaba ya wanakijiji wa Lukanga na wa vijiji vya jirani tunawashukuru sana Vodacom kwa hatua hii nasi leo tunaunganishwa na ulimwengu, tutawakumbuka wakati wote”Alisema Mwenyekiti huyo huku akiungwa mkono na mayowe ya wananchi walioonekana kuwa na furaha wakati wote wa hafla hiyo

Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye hafla hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Bw. Elius Nyakia aliipongeza Vodacom kwa kuendelea kuwekeza nchini hususan vijijini na hivyo kuwawezesha watanzania kuishi katika zama za sayansi na teknolojia.

“Hakuna ambae hafahamu kwamba katika karne ya 21 teknolojia ya habari na mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika maisha yetu. Vodacom inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wateja lakini bado wameendelea kuwekeza ili kila mmoja anufaike na huduma za simu za mkononi na kurahisisha maisha.”Alisema Bw. Nyakia

Aidha Bw Nyakia aliwataka wananchi kutambua fursa zinazopatikana kwa kuwa na huduma za mawasiliano ya simu za mtandao wa Vodacom kubwa ikiwa ni kuitumia kwa ukamilifu huduma ya M-pesa ili kuepukana na vishaiwishi vya wizi, ujambazi au hata kupoteza fedha kwa kukaa nazo majumbani ama kusafiri nazo umbali mrefu.

“Nawaomba sana wakazi wa kijijiji hiki kutumia teknolojia kurahisisha maisha yenu na hasa hii huduma ya M-pesa wote ni mashahidi jinsi inavyotusaidia, hivyo itumieni na muachane na utamaduni wa kuhifadhi fedha majumbani au kwa wale wafanyabishara kusafiri nazo. Kupitia M-pesa mnaweza kutuma au kutoa fedha benki au kufanya malipo ya huduma mbalimbali.”Alisema Nyakia huku akiutaka uongozi wa kijiji kuhakikisha mnara huo na miundombinu yake unalindwa ili kutorudisha nyuma maendeleo.

Awali akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa Herieth Koka alisema katika kipindi cha mwaka 2012/2013 kampuni ya Vodacom imefanya kazi kubwa ya kuboresha na kusogeza huduma zake katika maeneo yote ya kanda ya ziwa kazi ambayo bado inaendelea

“Mnara tunaouzindua leo ni mwanzo tu, tuna minara mingi mipya tuliyoijenga pamoja na kuiongezea nguvu iliyopo ili kuhakikisha wakazi wa kanda ya ziwa wanaendelea kunufaika na huduma mbalimbali ambazo kutoka Vodacom Pekee unaweza zipata kwa urahisi na wepesi. Lengo letu likiwa ni kuwawezesha wananchi kubadili maisha kupitia teknolojia na huduma ya simu za mkononi”Alisema Herieth

Amesema Vodacom itaendelea kuwa karibu na wakazi wa mikoa ya kanda ya Ziwa kama inavyofanya maeneo mengine nchini ikitambua umuhimu wa watu katika ustawi wa biashara wa kampuni sanjari na inavyoungwa mkono na watanzania na hivyo kuiwezesha kuwa kampuni inayoungoza nchini.

“Lengo letu sio kuongoza tu bali kuendelea kuwa kampuni iliyo karibu na watu na inayowafikia watanzania kila mahali na kuleta tofauti katika maisha yao. Tumekuwa tukifanya hivyo na ahadi yetu ya kuwaunganisha watanzania kimawasiliano na hatimae kubadili maisha yao bado ipo imara”. Aliongeza Herieth.

Kutoka Vodacom pekee utapata huduma ya M-Pesa ambayo unaweza kulipia huduma mbali mbali zaidi ya mia mbili, kuweka na kutoa pesa kwa kasi na usalama.

No comments: