Na Mwandishi Maalum
Wakati milipuko ya
risasi na mabomu ikiendelea
kurindima nchi Syria, huku
mamia kwa maelfu ya raia wa nchi hiyo wakiendelea kuwa wahanga wa
milipuko hiyo. Kwa mara ya tano Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, limepitisha Azimio kuhusu
hali ilivyo nchini humo likichagiza pande zinazohusika kusitisha mapigano.
Jana (Jumatano ) Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,
lilipigia kura Azimio nambari A/67/L. 63 kuhusu
Hali nchini Syria. Azimio hilo liliwasilishwa mbele ya wajumbe wa Baraza na Qatar kwa niaba ya Umoja
wa Falme za Kiarabu likiungwa mkono na
nchi kadhaa yakiwamo baadhi ya mataifa
makubwa isipokuwa China na Urusi.
Azimio hilo
lilipitishwa kwa kura za ndiyo 107,
hapana 12, na 59 za kutofungamana na upande wowote. Kati ya
nchi zilizopiga kura ya hapana ni
Urusi na Uchina, wakati Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa kati ya nchi 59 zilizopiga kura ya kutofungamana na upande
wowote.
Pamoja na
kwamba Azimio hilo limepitishwa
bado nchi nyingi zikiwamo hata baadhi
ya zile zilizopiga kura ya ndiyo, zimeelezea kutoridhishwa na baadhi ya vipengele vilivyomo ndani ya Azimio na namna mchakato mzima wa maandalizi yake
ulivyofanyika.
Wawakilishi wa Nchi zilizopiga kura ya kutofungamana
na upande wowote akiwamo Mwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, walipata
fursa ya kuelezea sababu zilizowafanya wakafikia uamuzi huo.
Baadhi ya sababu kubwa zilizoelezwa na wawakilishi hao ni pamoja na, kwamba,mkachato wa majadiliano ya
Azimio hilo haukuwa wazi, shirikishi na haukuzingatia
hoja zilizotolewa na wajumbe wengine
ikiwamo hoja iliyotolewa na Kundi la Nchi za Afrika ya kutaka uwasilishwaji wa
Azimio hilo uahirishwe ili kutoa nafasi ya kulijadili zaidi.
Kwamba, Azimio hilo lilikuwa limeegemea upande mmoja
na kuelekeza lawama na shutuma dhidi ya serikali ya rais Al- Assad kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu
na sheria za kimataifa , huku likiwa kimya kuhusu ukatili na ukiukwaji
unaofaywa na makundi yenye silaha yanayopigana nchi humo.
Kwamba, Azimio hilo lilikuwa linakaribisha uanzishwaji uliofanyika mwezi Novemba 2012 wa
Muungano wa Kitaifa kwajili ya Mapinduzi nchini Syria na Makundi ya Upinzani(National Coalition for
Syrian Revolution and Opposition Forces) kama chombo halali cha kusimamia na
kushiriki majadiliano kuelekea mabadiliko ya kisiasa na serikali ya mpito.
Ukaribishwa wa muungano huo ndani ya Azimio, unaelezwa
na baadhi ya wanadiplomasia hao kwamba
kwanza haikuwa kazi ya Baraza Kuu ya kuutambua Muungano huo likini ilikuwa ni
hatua inayoashiria mwelekeo wa kuiondoa
kinyemela serikali iliyoko madarakani hatua
ambayo siyo tu ni kinyume na
sheria za kimataifa lakini pia ni uingiliaji wa mambo ya ndani ya nchi nyingine na ni jambo baya.
Kwamba, Azimio
hilo halikuwa na chochote kipya ambacho kinaweza kuleta matumaini
kwa
raia wa Syria na kwamba lilikuwa halitoi usuluhisi wa kisiasa .
Kwamba,
Azimio hilo halikuwa na mashiko
kuletwa wakati huu ili hali ni siku chache tu zilizopita , Mawaziri wa
Mambo ya Nje wa Marekani na Urusi John Kerry na Bw. Sergey Lavrov
walikuwa wametangaza nia ya kuitisha mkutano wa Kimataifa kuzungumzia
hali ya Syria. Tangazo ambalo
lilipokelewa vema na jumuiya ya kimataifa.
Pamoja na hoja hizo na nyingine nyingi wawakilishi wa nchi zilizopiga kura ya kutofungamana na
upande wowote walieleza bayana kwamba kutounga mkono azimio hilo hakumaanishi kwamba walikuwa wanaunga
mkono ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na machafuko
yanayoendelea nchini humo.
Kwa upande wa wawakilishi waliopiga kura ya ndiyo
kuunga mkono, hoja kubwa kwao ilikuwa ni kwamba kwa kupitisha azimio hilo, ili
kuwa ni kujaribu kwa mara nyingine kwamba Jumuiya ya Kimataifa haijawasahau
wananchi wa Syria.
No comments:
Post a Comment