Wednesday, May 29, 2013

TASWIRA ZA ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR NCHINI CHINA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo wakati alipotembelea sehemu za Kihistoria zilizopo katika mji wa Beijing nchini China kiwa katika ziara ya kiserikali na ujumbe wake
 Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mw3amamwema Shein,akiangalia kitabu wakati alipotembelea makumbusho ya kihistoria katika Mji wa Beijing  nchini China,katika ziara ya Kiserikali kwa mualiko wa serikali ya Jamhuri ya Watu wa China,(kulia) Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi zake Zanzibar,Bibi Chen Qiman
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na ujumbe wake wakitembelea sehemu mbali mbali za  Kihistoria zilizopo katika makumbusho ya Mji wa  Beijing nchini China kiwa katika ziara ya kiserikali
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na ujumbe wake wakitembelea sehemu mbali mbali za  Kihistoria zilizopo katika makumbusho ya Mji wa  Beijing nchini China kiwa katika ziara ya kiserikali
 Pichani inaonekanwa  moja wapo ya Majengo yaliyokuwemo katika Eneo kubwa sana la kumbukumbu za Kihistoria katika Mji wa Beijing,ambapo wananchi wa China wakiwa na ukarimu wa aina yake
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiuliza suala kwa waongozaji na watoa maelezo katika sehemu za kihistoria zenye kumbukumbu nyingi,zinazopelekea wageni wa aina tofauti kutembelea katika mji huo wa Beinjing nchini China

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, na Naibu Waziri wa Biashara wa China Liu Cigui,katika ukumbi wa Mikutano wa World Hotel China,ambapo alifanya mazungumzo na kutiliana saini Makubaliano masuala ya Biashara
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Uchumi wa Maendeleo Omar Yussuf Mzee,akitiliana saini makubaliano ya kibishara kwa upande wa serikali ya Zanzibar na Naibu Waziri wa Biashara wa China Liu Cigui,katika ukumbi wa mikutano wa China World Hotel,wakishudiwa na baadhi ya mawaziri na maafisa wa Serikali zote mbili Zanzibar na China
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Uchumi wa Maendeleo Omar Yussuf Mzee,akibadilishana Hati ya saini ya Mikataba ya uhusiano wa biashara na Naibu Waziri wa Biashara wa China Liu Cigui,baada ya kutilianan saini katika ukumbi wa mikutano wa China World Hotel. 
Picha zote na Ramadhan Othman,China

No comments: