Monday, May 13, 2013

SHAMRASHAMRA ZA UFUNGUZI WA SHINA LA CCM CARDIFF WALES TAWI LA CCM UNITED KINGDOM

 Baadhi ya Viongozi, Wajumbe na  Wanachama Wapya katika picha ya pamoja
  Mwenyekiti wa CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Maina Ang’iela Owino akimkabidhi vitendea kazi  ikiwemo katiba ya chama kwa Ndugu Chande Kigwalilo mwenye kofia Mwenyekiti Shina jipya la Cardiff.
Katibu wa CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Bi. Mariam Mungula akimkadhi kadi za wanachama wapya Katibu wa shina Jipya la CCM Cardiff Bi. Rosemary Kiputa.
 Mwenyekiti wa TAWI LA CCM UK Ndugu Maina Ang’iela Owino akiongoza nyimbo za chama katika shamrashamra za ufunguzi wa shina jipya la CCM CARDIFF WALES.
 Wajumbe wakitega sikio kusikia machache toka kwa Mwenyekiti wa TAWI LA CCM UK
Ndugu Maina Owino hayupo pichani.
 Naibu Katibu CCM TAWI LA  UNITED KINGDOM Ndugu Albert Ntemi, Naibu katibu Itikadi Siasa na Uenezi CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Abraham Sangiwa na Bi Rose Kiputa Katibu shina jipya la Cardiff wakifuatila kwa makini mada muhimu katika ufunguzi huo.
 Makamu Mwenyekiti CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Said Sukwa akitoa yake machache katika ufunguzi huo.
 Wajumbe wa Shina jipya la CCM Cardiff Wales.
 Wajumbe na wanachama wapya CCM Shina la Cardiff.
 Naibu Katibu Itikadi Siasa na Uenezi CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Abraham Sangiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Shina la CCM Cardiff Ndugu Chande Kigwalilo na Mjumbe wa Shina la CCM Cardiff Bi. Prudencia Kimiti.
 Viongozi waliochaguliwa Shina la CCM Cardiff wakichukua nafasi zao aliyesimama na kutoa machache ni Ndugu Chande Kigwalilo Mwenyekiti Shina la CCM Cardiff akiwashukuru wajumbe kwa kumpa nafasi ya kuongoza shina hilo.
 Wajumbe wa CCM Cardiff wakipeana mkono wa pongezi toka kwa Mwenyekiti CCM UK Ndugu Maina Owino.
 Dr. Abdallah Saleh Mwenyekiti wa CCM Shina la Northmpton akifafanua jambo katika ufunguzi huo.

Bi. Prudencia Kimiti Mjumbe wa CCM Shina la Cardiff akitoa shukrani zake kwa uongozi wa TAWI LA UNITED KINGDOM kwa kuwezesha ufunguzi wa Shina Jijini CARDIFF.

Na Abraham Sangiwa Itikadi Siasa na Uenezi CCM – UNITED KINGDOM

Katika ufunguzi huo uliojaa shamrashamra na nderemo na  kuhudhuriwa na viongozi wote wa Tawi la CCM UK, Mwenyekiti wa Tawi la CCM UNITED KINGDOM Ndg  Maina Ang'iela Owino, Makamu Mwenyekiti  Ndugu Said Sukwa, Katibu Bi. Mariam Mungula, Naibu Katibu Ndugu Albert Ntemi, Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Leybab Mdegela, Naibu Katibu Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Abraham Sangiwa, Katibu wa Uchumi na Fedha Ndugu John Juma Lyimo, Naibu Katibu Uchumi na Fedha Ndugu Mohamed Upete na wanaCCM toka mashina mbalimbali ya CCM UK.
 Mwenyekiti wa Tawi la CCM UNITED KINGDOM Ndg  Maina Ang'iela Owino aliwashukuru Watanzania hao kwa kujitokeza kwa wingi kuandaa, kuyakubali madhumuni  na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.  Ndg Owino  aliwakumbusha kuwa uhalali wa shina lao unajumuishwa katika Sera ya nje na matawi yake katika Katiba ya CCM.
Ndg Owino aliwakumbusha kuwa kujiunga na CCM kunaambatana na kuzingatia masharti ya kuheshimu watu, kufanya juhudi za kuielewa, kuielezea, kuitetea na kuitekeleza Itikadi na Siasa ya CCM. Pia kwamba CCM inathamini haki na wajibu wa mwanachama.
Aidha Ndg Owino hakusita kuwakumbusha kuwa CCM na Serikali yake inaendelea kujijenga na kuboresha taasisi zake ili kuendana na mahitaji ya kizazi na wakati uliopo na hivyo basi  wanaCCM Cardiff wasioneane haya wala kuogopa kuchagua viongozi wenye sifa za kutosheka na wasio tawaliwa na tamaa na watakao zingatia miiko ya uongozi kama inavyoainishwa katika katiba ya CCM.
Kabla ya kuhitimisha hotuba yake Ndg Owino alichambua na kuainisha kwa kina na kuishirikisha halaiki kufanya tathmini ya wazi ya jinsi CCM imeiongoza serikali kutekeleza ilani yake ya uchaguzi ya 2005/2010 na mafanikio dhahiri yanayopatika katika kutatua kero za wananchi. Aidha alisema baadhi ya changamoto zilizopo nchini ni matokeo ya mabadiliko endelevu, kukua na kuendelea kwa mifumo na taasisi za umma na sekta binafsi na kwamba CCM na serikali yake inaendele kujiimarisha kuyakabili kwa mikakati na mipango endelevu ya muda mfupi na mrefu, pia Ndugu Maina aliwakumbusha Wana CCM UK Kuwa mchango wao unathaminiwa na ni wamuhimu katika kuleta mabadiliko yatayowanufaisha wengi katika nyanja mbalimbali muhimu za kimaendeleo na kichumi
Idara ya Itikadi Siasa na Uenezi na ile ya Uchumi na Fedha walitoa machache yanayohusu idara zao na namna zinavyofanya kazi ili kuwapa mwanga wanachama wapya na viongozi katika shina hilo.
Ufunguzi huo ulifuatiwa na uchaguzi wa Viongozi mashina uliosimamiwa na Katibu wa CCM UK, Bi Mariam Mungula.
Viongozi waliochaguliwa katika shina hilo jipya la Cardiff – Wales ni;
  1. Chande Kigwalilo                    Mwenyekiti wa Shina
  2. Bi. Rosemary Kiputa              Katibu wa Shina
  3. Prudencia Kimiti                      Mjumbe wa Shina
  4. Munde Nyirambo                     Mjumbe wa Shina
  5. Alen  Mguto                             Mjumbe wa Shina
Mara baada ya uchaguzi huo Mwenyekiti wa shina jipya la Cardiff Ndugu Chande Kigwalilo alitoa machache na kushukuru wajumbe na wanachama kumpa nafasi ya kuliongoza shina na kushukuru uongozi wa tawi kwa kufanikisha ufunguzi huo na kuwakarakibisha Jijini Cardiff.

Imetolewa na Idara ya Itikadi Siasa na Uenezi
CCM TAWI LA UNITED KINGDOM

1 comment:

Anonymous said...

Sasa CARDIFF kimeeleweka changamoto bado zipo kwani kuna mambo mengi tunahitaji kuisadia serikali yetu kufanya mabadiliko na kwenda na wakati katika uchumi endelevu