Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha maombolezo alipofika mkoani
Arusha leo Kuwapa pole ndugu na jamaa ambao ndugu zao wamefariki katika machimbo
ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha. Maporomoko hayo yametokea
jana na kusababisha vifo vya watu13 na majeruhi wawili ambao mmoja
ameruhusiwa na mwingine amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru
Waziri Mkuu akiwa na wabunge wa Arusha na Meya pamoja na mkuu wa mkoa kwenye msiba huo mzito. Toka Kushoto ni Mbunge wa Arusha Mjini Mhe Godbless Lema, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Magessa Mulongo, Meya wa jiji la Arusha Mstahiki Gaudence Lyimo, Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari na Mbunge wa kuteuliwa Catherine Magige
Sehemu ya majeneza ya marehemu katika ibada hiyo maalumu leo
Kiongozi wa kidini akiombea marehemu
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akitoa pole kwa wafiwa
Sehemu ya machimbo ya Moramu iliyopotomoka na kuua watu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akiwa na wabunge wote wa mkoa wa Arusha na viongozi wengine akitembelea machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha
Waziri Mkuu akitembelea sehemu ya tukio
ukaguzi ukiendelea
Waziri Mkuu akitoa maelekezo baada ya kutembelea machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha. Picha zote na Chris Mfinanga
No comments:
Post a Comment