Saturday, April 13, 2013

DKT. SHEIN Afungua Nyumba ya Walimu Skuli ya Kusini Makunduchi leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Makunduchi Mzuri kaja, Maalim Rashid Makame Shamsi,(kulia) alipotembelea Nyumba ya Walimu baada ya kufungua leo huko Skuli ya Kusini Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe kuifungua Nyumba ya Walimu Skuli ya Kusini Makunduchi leo, iliyojengwa na Jumuiya ya ya Maendeleo ya Makunduchi Mzuri kaja,kwa ushirikiano na Jumuiya ya Bus 4 Afrika,yenye Makao Makuu yake nchini Sweden.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Wazee na Wananchi alipowasili Skuli ya Kusini Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja leo, kuifungua Nyumba ya Walimu,iliyojengwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Makunduchi Mzuri kaja,kwa ushirikiano na Jumuiya ya Bus 4 Afrika,ya nchini Sweden.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na Mwakilishi wa Jimbo Makunduchi pia Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Maalim Haroun Ali Suleiman,baada ya kuifungua Nyumba ya Walimu ya Skuli ya Kusini Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
Baadhi ya Wazee na Wanafunzi wa Skuli ya Kusini Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja,wakiwa katika sherehe za ufunguzi wa Nyumba ya Walimu, iliyojengwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Makunduchi Mzuri kaja,kwa ushirikiano na Jumuiya ya Bus 4 Afrika,ya nchini Sweden.
Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe ya Ufunguzi wa Nyumba ya Walimu,Skuli ya Kusini Makunduchi iliyojengwa na Jumuiya ya ya Maendeleo ya Makunduchi Mzuri kaja,kwa ushirikiano na Jumuiya ya Bus 4 Afrika,ya nchini Sweden,wakifuatilia kwa makini harakati za sherehe hiyo ilivyoendelea katika viwanja vya skuli hiyo leo.
Wanakikundi cha mazoezi ya Viungo cha Jitenge,wakionesha mtindo wao wa Mazoezi wakati wa sherehe za Ufunguzi wa Nyumba ya Walimu,Skuli ya Kusini Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja,akiwa mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Katibu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Makunduchi Mzuri kaja, Maalim Rashid Makame Shamsi, akisoma risala ya wanajumuiya wakati wa sherehe ya Ufunguzi wa Nyumba ya Walimu,Skuli ya Kusini Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya Viongozi mbali mbali walioalikwa katika sherehe za ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Skuli ya Kusini Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja leo,wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,aliyoitoa mbele ya wananchi katika sherehe hiyo.
Mwakilishi wa Jumuiya ya Bus 4 Afrika yenye Makao Makuu yake Nchini Sweden Bibi Hannah Mc Carrick,akitoa salam wakati wa Sherehe ya Ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Skuli ya Kusini Makunduchi,iliyojengwa na Jumuiya hiyo na Ushirikiano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Makunduchi Mzuri kaja, iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi cheti Mwakilishi wa Jumuiya ya Bus 4 Afrika yenye Makao Makuu yake Nchini Sweden Bibi Hannah Mc Carrick,wakati wa Sherehe ya Ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Skuli ya Kusini Makunduchi,Wilaya ya Kusini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi cheti Mstaafu Diwani Ameir Simai Pope,wakati wa Sherehe ya Ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Skuli ya Kusini Makunduchi,Wilaya ya Kusini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Makundhuchi Mzurikaja,Mzee Haji Setti,wakati wa Sherehe ya Ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Skuli ya Kusini Makunduchi,Wilaya ya Kusini Unguja leo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamuhuna,akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kuzungumza na Wananchi na Wanajumuiya ya Maendeleo ya Makunduchi Mzuri kaja,Wilaya ya Kusini Unguja, wakati wa Sherehe ya Ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Skuli ya Kusini Makunduchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Wananchi na Wanajumuiya ya Maendeleo ya Makunduchi Mzuri kaja,Wilaya ya Kusini Unguja, wakati wa Sherehe ya Ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Skuli ya Kusini Makunduchi, iliyojengwa na Jumuiya ya ya Maendeleo ya Makunduchi Mzuri kaja,kwa ushirikiano na Jumuiya ya Bus 4 Afrika ya Sweden.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

No comments: