Thursday, March 28, 2013

Mbunge Catherine magige atoa misaada arusha
















NA SHAABAN MDOE,ARUSHA.
MTOTO yatima wa jinsia ya kiume aliyedaiwa kutupwa na mmoja wa wazazi wake katika lango la kuingilia katika kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha Faraja Ophanage Home amemliza mbunge wa jumuiya ya vijana(UVCCM)mkoa wa Arusha Catherine Magige.
Magige ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya misaada ya Catherine Foundation aliangua kilio hicho alipokua akipokea taarifa kuhusu kituo hicho kutoka kwa mkurugenzi wake mchungaji Faraja Maliaki kilichopo eneo la Nduruma jijini Arusha alipofika kwaajili ya kukabidhi misaada mbalimbali kwaajili ya watoto hao kusherehekea sikukuu ya Pasaka.
Mbali na misaada hiyo aliyoitoa katika kituo hicho pia Catherine alimwaga misaada mingine katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru Arusha na kituo kingine cha kulelea yatima cha Lohaga kilichopo eneo la Shangarai jijini Arusha.
Misaada hiyo ni ile ya kibinadamu ikiwemo Mbuzi mnyama wawili,Mchele,Mafuta ya kula,Sabuni za unga za kipande na kipande za kufulia,Juisi,Pipi kwa watoto.
Magige alifikwa na hali hiyo na kushindwa kujizuia na kuangua kilio mbele ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Faraja na watu waliomsindikiza baada ya kupokea taarifa kuwa miongoni mwa watoto hao yupo mmoja aliyeokotwa nje ya langola kuingilia kituoni hapo anayedaiwa kutupwa na mama yake.
Akitoa maelezo ya kituo chake mbele ya mbunge huyo mkurugenzi huyowa wa kituo alisema siku moja asubuhi motto huyo aliokotwa na wahudumu wake akiwa usingizini pasipo kufahamika aliyemtupa.
Alisema mara baada ya kuokotwa kwa mtoto huyo walijaribu kumtafuta muhusikakwaajili ya kuzungumza nae na kuona sababu zilizomfikisha kufanya maamuzi hayo na ikiwezekana kumpatia msaada lakini haikuwezekana na mpaka sasa wanamlea motto huyo.
Alisema alianzisha kituo hicho kwa mambo makuu mawili ikiwemo kuwasaidia watoto hao waishio katika mazingira magumu na kuwaondo wasichana wanaojiuza katika biashara hiyo hatari.
Alisema hadi sasa kituo hicho kinalea na kuwasomesha watoto 200 wenye umri tofautitofauti pamoja na wasichana waliokua wakifanya biashara ya kujiuza katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha likiwemo eneo maarufu la Mrina.
Alisema miongoni mwa watoto hao wanaolelewa kituoni hapo wapo zaidi ya 20 walioathirika na ugonjwa wa ukimwi ambapo kutokanana hali zao wanaendelea kuwapatia virutubisho mbalimbali pamoja na vidongewa ARV kwaajili yakurefusha maisha yao.
Alisema pamoja na mazuri yote wanayoyafanya kituoni hapo bado kituo kinakabiliwa na changamoto malimbali zikiwemo za ukosefu wa fedha za chakula hali inayosababisha watoto kula mlo mmoja.
Pia alisema changamoto nyingine niya ukosefu wa malazi ambapo watoto wengine wanalazimika kulala katika maturubai yanayotandikwa chini kwa maisha yao yote hali inayoweza kuwasababisha mardhi yatokanayo na baridi ikiwemo Limonia.
Pia aliishukuru taasisi ya Catherine Foundation kwa msaada walioutoa kwakua utawezesha watoto hao kujisikia wapo katika makazi yao na wazazi wao katika kipindi hichi cha sikukuu ya Pasaka kutokana na ukweli kuwa wengi wao wamekua wakitamani hali hiyo muda wote wa maisha yao.
Akizungumzia Changamoto hizo kwa shida kutokana na kukabwa na kilio muda wote Magige alisema amejonea na kusikia changamoto hizo naatafanya juhudi zake binafsi pamoja na wadau wengine ili kuweza kuzitatua changamoto hizo ili kuwaweka katika mazingira mazuri.
Akizungumzia misaada aliyoitoa katika hospitali ya Mount Meru kupitia taasisi yake hiyo Magige alisema itawawezesha wagonjwa na wazazi kusherehekea vyema sikukuu ya Pasaka pamoja na kutojiona kama wametengwa katika kipindi hicho kigumu cha kuugua,kuuguza na kulea.
Alisema hii ni mara ya pili kwa taasisi yake kutoa misaada ya kibinadamu tangu kuzinduliwa kwa taasisi yake hiyo hapa mkoani Arusha ambapo siku ya uzinduzi iliweza kutoa baiskeli zaidi ya 20 kwa walemavu mbalimbali wa viungo.

No comments: