Wednesday, March 13, 2013

mashindano ya nssf yapamba moto

 Kikosi cha timu ya TSN.
Kikosi cha timu ya Free Media.
 Mchezaji wa timu ya TSN, Sodi Ahmed (kulia) akimramba chenga Abdallah Fundi, wa timu ya Free Media, wakati wa mchezo wa michuano ya Kombe la NSSF 2013, uliochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu ya TSN imeibuka na ushindi wa mabao 5-0, mabao hayo yakiwekwa kimiani na wachezaji, Rashid Kagusa, aliyesalimia nyavu mara tatu, Evance Samwel, aliyefunga bao 1 na Said Kabasha, aliyetupia bao 1.
 Beki wa TSN, Sufianimafoto (kushoto) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Free Medi, saleh Ally, wakati wa mchezo huo.
 Mshambuliaji wa Free Media, Saleh Ally (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa TSN, wakati wa mchezo huo.
 Kiungo wa TSn, Rashd Kagusa, akimhadaa mchezaji wa Free Media.
 Mchezaji wa Tsn Sudi Ahmed (kulia) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Free Media wakati wa mchezo huo.
 Mchezaji wa Tsn, Sudi Ahmed ( wa pili kushoto) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Free Media, John Dande, wakati wa mchezo huo.
 Beki wa Tsn, Sufianimafoto, akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Free Medi. 
 Saleh Ally wa Free Media (kushoto) akiwania mpira na Sufianimafoto.
 Mchezaji wa Tsn, Jemedari Said (katikati) akiwania mpira na mchezaji wa Free Media, Suleiman Jumbe.
 Sufianimafoto, akimzunguka John Dande.......

No comments: