Ni Mhitimu wa Chuo Kikuu Cha Sokoine Morogoro (SUA ), Mkaazi wa Njombe! Zawadi Nono Ya Fedha Taslimu, Shilingi Laki Tano ( Tsh.500,000/=) Za Kitanzania, kutolewa kwa mtu atakaye fanikishwa kukamatwa kwa tapeli hili la mtandaoni.
Hatimaye yule tapeli sugu wa mtandaoni aliyekuwa akiwatapeli wananchi mbalimbali kwa jina la RafikiElimu akiwahadaa kuwapatia ajira ajulikana .
INAPOTOKA : Mnamo siku ya tarehe 11 Machi 2013, tuliripoti kupitia blogu yetu na katika blogu mbalimbali nchini kuhusu kuwepo kwa mtu anaye watapeli wananchi fedha kwa kutumia jina la taasisi yetu. Tapeli huyu asiye na hata chembe ya huruma kwa masikini wenzake, aliweka tangazo katika mtandao wa Zoom Tanzania, mnamo mwanzoni mwa mwezi February 2013 akitangaza nafasi za kazi z a kuvolunteer katika mikoa mbali mbali ya Tanzania bara. Baada ya watu kutuma maombi yao, tapeli huyo
aliyekuwa akijitambulisha kwa jina bandia la EMMANUEL ALBERT na kwamba yeye ni HR wa RafikiElimu, aliwaambia kuwa wamepata nafasi, na kuwatumia fomu za kujaza kisha kuwataka wamtumie
shilingi elfu Tano ( Tshs. 5,000/=) za kitanzania kwa mpesa kwenda namba 0763906931 ( AMBAYO MBAYA ZAIDI AMEISAJILI KWA JINA LA RAFIKIELIMU ).. Baada ya kumtumia pesa , tapeli huyo aliwatumia barua na kuwaagiza kuripoti kazini katika taasisi mbalimbali, huku mmoja kati yao akimuagiza aje kuripoti katika ofisi zetu.
Tulibaini juu ya uwepo wa utapeli huu mara baada ya kutembelewa na mmoja kati ya wahanga wa utapeli huo. Dada huyo aliye jitambulisha kwa jina la HAWA MUSSA ambaye ni Muhitimu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ( 2012 ) aliripoti katika ofisi zetu siku ya tarehe 11 Machi 2013 saa nne kamili
asubuhi na kuomba kumuona HR . Baada ya kufanya naye mazungumzo ndipo tulipo baini kuwepo kwa utapeli unao fanyika kwa jina la taasisi yetu. Haraka haraka tukaenda kuripoti uhalifu huu kwenye kituo kidogo cha polisi cha Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam, na kukabidhiwa RB namba UD/RB/849/2013 WIZI
KWA NJIA YA MTANDAO.
No comments:
Post a Comment