Sunday, February 24, 2013

Maonesho ya SHANGAA-Art of Tanzania yatia fora New York

Sehemu ya Sanaa zilizopamba maonesho ya SHANGAA- Art of Tanzania ya kwanza na ya aina yake kufanyika nje ya Tanzania na Ujerumani yameandaliwa na Queens Community Collage moja ya Vyuo vya Mtandano wa Vyuo Vikuu vya Jiji la New York.(CUNY) kwa kushirikiana na Dr. Gary Van Wyk, mtaalam wa Historia ya Afrika amefanya tafiti zake nchini Tanzania na kutokana mapenzi yake makubwa kwa Tanzania amempatia mtoto wake jina la Mayala, mwingine aliyeshirikia maandalizi hayo ni Mkurugenzi wa Art Gallery Bw. Faustino Quintanilla. 

Maonesho hayo yaliyokusanya zaidi ya sanaa 121 kutoka kwa wadau mbalimbali yalipambwa na Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na aliwashukuru waandaaji wa maonesho hayo kwa uamuzi wao wa kutangaza mila, tamaduni na historia nzuri ya Tanzania. 

Naye Dr. Van Wyk licha ya kuelezea historia nzuri ya Tanzania na watu wake, amewataka washiriki wa maonesho hayo kuitembelea Tanzania kwa kuwa ni nchi yenye amani, utulivu na watu wenye upendo licha ya tofauti zao za kikabila, dini na rangi














No comments: