Thursday, February 21, 2013

KONGAMANO LA 8 LA BIMA YA AFYA NA WANAHABARI LAFUNGULIWA MTWARA

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Seif Rashid (kushoto) akilakiwa na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athuman Rehani alipowasili leo asubuhi kufungua Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la Wanahabari kwenye Chuo cha Ualimu Mtwara. 


Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NHIF, Eugen Mikongoti. 
Naibu Waziri akisalimiana na Fortunata Raymond ambaye ni msimamizi wa NHIF Mkoa wa Lindi
 Naibu Waziri, akisalimiana na Meneja wa NHIF Mkoa wa Mtwara, Joyce Sumbwe.
Naibu Waziri wa Afya na Utawi wa Jamii, Dk. Rashid (kulia) akiwa na  Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Williman Kapenjama alipokuwa akiingia kufungua kongamano hilo.
Baadhi ya maofisa waalikwa kutoka taasisi mbalimbali nchini  wakiwemo wakuu wa wilaya wakipiga makofi wakati Naibu Waziri, Dk Seif Rashid akiingia ukumbini

Baadhi ya maofisa waalikwa na wanahabari wakiwa katika kongamano hilo
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba, akielezea mikakati mbalimbali ya kusambaza huduma za mfuko huo sehemu mbalimbali nchini. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Rashid.
Naibu Waziri wa Afya na Utawi wa Jamii, Dk. Rashid (wa pili kushoto) akiiongoza meza kuu kuowaombea watu waliopoteza maisha katika kipindi cha mwaka jana na mwaka huu akiwemo babake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi,Hawa Ghasia aliyefariki dunia hivi karibuni.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa mikoa nchini, Abbas Kandoro akihutubia wakati wa kongamano hilo.
Sehemu ya washiriki katika kongamano hilo
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Williman Kapenjama akiwakaribisha washiriki na kuwaelezea vivutio mbalimbali vilivyomo walayani humo, ukiwemo Mji Mkongwe wa Mikindani, Visiwa vya Msimbati pamoja na visima vya gesi.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu, Josepg Simbakali akihutubia katika kongamano hilo.
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akihutubia wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo. 
Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena akitoa shukrani kwa niaba ya wanahabari baada ya Naibu Waziri kufungua kongamano hilo.
 Baadhi ya watumishi wa NHIF wakisikiliza kwa makini wakati Naibu Waziri akihutubia.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba, akioneshakitabu chenye tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanahabari mwaka 2012, kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajili ya afya katika hospitali na zahanati mbalimbali nchini. 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na viongozi wengine wakipata stafutahi baada ya ufunguzi wa kongamano hilo. Picha zote na Kamanda wa Matukio

No comments: