Monday, February 11, 2013

KIONGOZI WA KANISA KATOLIKI DUNIANI BABA MTAKATIFU BENEDIKTI WA 16 AUSHANGAZA ULIMWENGU BAADA YA KUTANGAZA KUJIUZULU

Baba mtakatifu Benedikti wa 16

Katika hali isiyotegemewa, kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki lenye kusadikiwa kuwa na wastani wa waumini billioni 1.2 duniani kote ; kiongozi huyo, baba mtakatifu Benedikti wa 16 ametangaza kujiuzulu. Sababu zilizotolewa kutoka kwa msemaji mkuu wa Vatican Padre Frederico Lombard, washirika la wamisionari Wajesuit ameuthibitishia ulimwengu kuhusu habari hizo kupitia radio Vatican. Sababu za Kiumri na kiafya ni baadhi ya sababu zilizohusishwa na kujiuzulu huko.

Baba mtakatifu Benedikti wa 16 alizaliwa 1927 na kubatizwa jina la Joseph Ratzinger. Amekuwa Pope wa 265 katika mlolongo wa viongozi wa kanisa hilo.

Ratzinger alikuwa na umri wa miaka 78 wakati alipochaaguliwa kuliongoza kanisa hilo mwezi April 2005.

Hakuna Pope ambaye amejiuzulu kwa hiari katika nyakati za hivi karibuni na Pope wakwanza kuachia ngazi alikuwa Pope Gregory XII mnamo mwaka 1415; yapata miaka – 598 iliyopita. Kabla ya yake Pope mwingine aliyejiuzulu kwa hiari ni Pope Celestine V mnamo mwaka 1294.

Kiongozi huyo mwenye asili ya Ujerumani, ametangaza uamuzi huo akiwa na umri wa miaka 85. Baada yakuliongoza kanisa Katoliki kwa takribani miaka nane ametangaza kuachia ngazi ifikapo tarehe 28/02/2013. Na habari kutoka vyanzo mbali mbali zinasema kuwa huenda kiongozi mpya wa kanisa hilo akachaguliwa ifikapo mwishoni mwa mwezi March mwaka huu.


Anakuwa kiongozi wa kwanza wa kanisa hilo Katoliki kujiuzulu baada ya takribani miaka 600, iliyopita wakati kiogozi wakanisa hilo alipojiuzulu. Alichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa hilo mwezi April 19, 2005 wakati huo alikuwa na umri wa miaka 78 – akimzidi mtangulizi wake wa kiti hicho baba mtakatifu Yohane Paulo II kwa miaka 20 wakati alipochaguliwa kiongozi wa kanisa hilo.


Alikuwa pope wakwanza kutoka Ujerumani kwa takribani miaka 1,000 iliyopita, na ni pope wapili asiye muitaliano katika mlolongo wa viongozi wakanisa hilo. Aliweza kusafiri nje ya Itali walao kwa wastani mara nne kwa mwaka lakini hakufikia rekodi ya mtangulizi wake.

Pamoja na changamoto nyingi alizokutana nazo wakati wa uongozi wake ikiwemo zile za ubakaji wawatoto. Kiongozi huyo aliweza kusimamia vizuri kile kinachoitwa “family values” na alipinga kwa nguvu zote utoaji mimba, ndoa za jinsia moja na « euthanasia » yaani kuwaondolea uhai wale wanaosadikiwa kuwa na maumivu makali au umri ulichoka sana. Uhai wa binadamu ikiwa ni moja ya thamani aliyopewa binadamu toka kwa muumba wake yaani mwenyezi Mungu. Kiongozi wakanisa hilo huchaguliwa na viongozi wa juu wakanisa hilo maarufu kama ma-kardinali. Ambaye kwa Tanzania itawakilishwa na Kardinali Pengo.

Afrika inakardinali ambaye anaweza kufikiriwa na wachaguzi hao. Ambaye ni Kardinali Peter Turkson(64) ambaye pia ni mkuu ya depatimenti/idara ya Haki na Amani katika Vatican. Huzungumza kwa ufasa lugha za Kifante, Kiingereza, Kifaransa, Kiitaliano, Kijerumani, Kiebrania, Kiaramaiki, Kiarabu na kigiriki.

Nimezaliwa wa Ghana. Aliteuliwa kuwa Kardinali mwaka 2003.

Kardinali mwingine anayeweza kufikiriwa kutoka Afrika, japokuwa umri unamtupa mkono ni Kardinali Francis Arinze, 80, kutoka Nigeria pia ni chaguo wezekano kuongoza kiti hicho.

Mzaliwa wa Nigeria, 1932, the 80- anaweza kuwa mwafrika wa kwanza katika kipindi cha miaka 1,500 kukalia kiti hicho cha mtakatifu Petro. Kardinali Arinze alipewa daraja la Upadri 1958 na akawa askofu wakwanza kijana duniani kote akiwa na miaka 32, mwaka 1965. Aliteuliwa kuwa Kardinali mwaka 1985.

Wakati huo huo viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa siasa na dini mbali mbali wameupongeza uamuzi huo wabusara na kumtakia afya njema kiongozi huyo. Viongozi hao ni pamoja na waziri mkuu wa Uingereza ndugu David Cameron, Kansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel, chifu rabbi Yona Metzger wa Israeli, rais wa Ufaransa ndugu François Hollande na wengineo wengi.

Ifuatayo ni sehemu ya ujumbe wa baba mtakatifu uliotolewa kwalugha ya kilatini kwa viongozi wa “consistory”, au baraza la viongozi wa kanisa hilo, akitangza mpango wake huo wakujiuzulu leo jumatatu asubuhi. Ujumbe huo unasema:

"Dear Brothers,

I have convoked you to this Consistory, not only for the three canonizations, but also to communicate to you a decision of great importance for the life of the Church. After having repeatedly examined my conscience before God, I have come to the certainty that my strengths, due to an advanced age, are no longer suited to an adequate exercise of the Petrine ministry. I am well aware that this ministry, due to its essential spiritual nature, must be carried out not only with words and deeds, but no less with prayer and suffering. 

However, in today's world, subject to so many rapid changes and shaken by questions of deep relevance for the life of faith, in order to govern the bark of Saint Peter and proclaim the Gospel, both strength of mind and body are necessary, strength which in the last few months, has deteriorated in me to the extent that I have had to recognize my incapacity to adequately fulfil the ministry entrusted to me. 

For this reason, and well aware of the seriousness of this act, with full freedom I declare that I renounce the ministry of Bishop of Rome, Successor of Saint Peter, entrusted to me by the Cardinals on 19 April 2005, in such a way, that as from 28 February 2013, at 20:00 hours, the See of Rome, the See of Saint Peter, will be vacant and a Conclave to elect the new Supreme Pontiff will have to be convoked by those whose competence it is.

 "Dear Brothers, I thank you most sincerely for all the love and work with which you have supported me in my ministry and I ask pardon for all my defects. And now, let us entrust the Holy Church to the care of Our Supreme Pastor, Our Lord Jesus Christ, and implore his holy Mother Mary, so that she may assist the Cardinal Fathers with her maternal solicitude, in electing a new Supreme Pontiff. With regard to myself, I wish to also devotedly serve the Holy Church of God in the future through a life dedicated to prayer."

Imeandaliwa na Frederick Meela, kwa msaada wa vyanzo mbalimbali.
Ndugu yenu kabisa wa Francophonie, tawi la Ufaransa.

No comments: