Monday, January 28, 2013

SEKRETARIETI YA CCM YATEMBELEA MRADI WA DARAJA LA MARAGARANI MKOANI KIGOMA LEO

Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM,ukiongozwa na Katibu Mkuu,Ndg. Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye ukiwa katika matembezi ya kuangalia maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Maragarasi na Ujenzi wa Barabara ya kutoka Kidawe mpaka Uvinza kwa kiwango cha lami leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza na Meneja wa Kampuni ya HANIL ambao ni Wakandarasi wa ujenzi wa Daraja hilo,Bw. Jung-Sik You kutoka nchini Korea.
Meneja wa Kampuni ya HANIL ambao ni Wakandarasi wa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Maragarasi na Ujenzi wa Barabara ya kutoka Kidawe mpaka Uvinza kwa kiwango cha lami,Bw. Jung-Sik You (kushoto) akitoa maelezo machache juu ya maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana na kuahidi kuwa mpaka ifikikapo mwezi Septemba ama Oktoba,Daraja hilo litakuwa limeshakamilika na kulikabidhi kwa Serikali.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia) akizungumza na Meneja wa Tanroads Kigoma,Inginia Narcis Choma wakati Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM ulipofanya ziara katika eneo la Mto Maragarasi ili kujionea hali ilivyo ya Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Maragarasi na Ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kutoka Kidawe mpaka Uvinza.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nguruka,Wilayani Uvinza mkoani Kigoma leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza na Wazee wa Kijiji cha Nguruka,Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma leo,wakati alipofanya ziara ya kutembelea vijiji viwili vya Wilaya hiyo ya Uvinza.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM),Martin Shigella akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Nguruka,Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma leo.
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Nguruka,Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nguruka,Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma leo,waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza na pia kusikiliza shida zao wakati alipofanya ziara ya kutembelea vijiji viwili vya Wilaya hiyo ya Uvinza.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Uvinza,Wilayani Uvinza mkoani Kigoma leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Uvinza,Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma leo
Babu akitabasamu wakati akimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (hayupo pichani) wakati alipokuwa akihutubia.
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akijadiliana jambo na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye.

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya,Dokii akiimba moja ya nyimbo zake alizozitunga kwa ajili ya CCM.
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa pamoja na Katibu wa CCM katika kata ya Nguruka,Asha Baraka wakati wa matembezi ya kuingia kwenye kijiji hicho cha Nguruka mkoani Kigoma leo.
Katibu wa CCM katika kata ya Nguruka,Asha Baraka akiwasalimia wananchi wake.
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi waliokuwa wamejipanga barabarani kumuona.
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa na mmoja wa watoto wa kijiji hicho cha Nguruka.
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiimba nyimbo na wananchi wa kijiji cha Nguruka.

No comments: