Friday, January 4, 2013

SAFARI YA MWISHO YA MAREHEMU SADICK JUMA KILOWOKO (SAJUKI)

 Waombolezaji wakiwa wamejipaga tayari kwa kuupokea Mwili wa Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akiwa katika Mazungumzo na Baba Mzazi wa Marehemu Sadick Juma Kilowoko,Mzee Juma Kilowoko,Meya wa Manispaa ya Ilala,Mh. Jerry Silaa (kulia) na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba Mara baada ya Mazishi wa Msanii wa Filamu,Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) yaliyofanyika mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kisutu,jijini Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Mazungumzo na Meya wa Manispaa ya Ilala,Mh. Jerry Silaa (kulia) na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba wakati wa Mazishi wa Msanii wa Filamu,Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) yaliyofanyika mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kisutu,jijini Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Kikwete akimsiliza kwa makini Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba.
 Waombolezaji wakiwa Makaburini.
 Mh. Zitto Kabwe akiwa katika Mazungumzo na Wadau.
 Mh. Iddi Azzan akizungumza na Mwandishi wa habari wa Gazeti la Tanzania Daima,Andrew Chale.
Mpiga Picha wa Gazeti la Uhuru,Akimapa taswira yake Maridhawa wakati wa Mazishi wa Msanii wa Fimalu,Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) Makaburi ya Kisutu jijini Dar leo.(halafu unaona mtu hapa anavyotafuta picha zake kwa mbinde,baadae unakuwa watu wengine wanakopi na kuweka kwenye Blogu zao tena bila hata ya aibu,wakijidai wamepiga wao.yaani sio fea kabisaaaaa)
 Maelfu ya Waombolezaji wakimzima Sajuki leo kwenye Makaburi ya Kisutu.
 Wadau mbali mbali wakiwa makaburini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika mchana huu kwenye Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam.
Mwili wa Marehumu Sadick Juma Kilowoko ukiwasili kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo tayari kwa Mazishi.

No comments: