Friday, January 4, 2013

DK. HARRISON MWAKYEMBE ATEMBELEA UWANJA WA NDEGE SONGWE MBEYA


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),Mhandisi Suleiman S. Suleiman akimwelezea Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe jinsi uwanja wa ndege wa songwe unavyofanya kazi toka uzinduliwe mwezi wa 12 mwaka jana na kuwa sasa uwanja huo umebaki maeneo ya maegesho ya ndege kubwa kama boing 737 

Mmoja ya wahandisi wa ujenzi wa uwanja huo wa songwe akimwelezea waziri wa uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe hatuza za mwisho za ujenzi wa maegesho  ya ndege kubwa.
Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzani,Jenerali Davies Mwamnyange akisalimiana na kuagana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman katika Uwanja wa Ndege wa Songwe kabla ya kuanza kwa ziara ya waziri wa uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe 
Mkuu wa Majeshi,Jenerali Davies Mwamnyange akiondoka uwanjani hapo kurejea Jijini Dar,mara baada ya kumaliza Mapumziko yake mafupi
Huu ni mnara  wa kuongozea ndege katika kiwanja hicho cha Songwe Mbeya
Mwongoza ndege mwandamizi John Chambo akimwezea Waziri Mwakyembe jinsi wanavyofanya kazi ya kuongoza ndege kwa kutumia mnara huo
Mkuu wa kitengo cha hali ya hewa Issa Hamad akimwelezea waziri mwakyembe juu ya shughuli zao za upimaji wa hali ya hewa uwanjani hapo na mkoa kwa ujumla.
Hili ndilo eneo la maegesho ya ndege kubwa aina ya boing 737 ambalo mwishoni mwa mwezi huu wa kwanza litakamilika
Hili ni eneo la kutua ndege na kurukia  barabara hiyo ya ndege inaurefu wa zaidi ya kilometa 3.5 km

 
Hii ni sura ya mbele ya uwanja huo wa songwe Mbeya
Hili ni jengo la kikosi cha zimamoto uwanjani hapo
Hawa ni waandishi wa habari walioanza kuripoti ujenzi wa uwanja huo tangu unaanza kujengwa mpaka sasa kulia kabisa  ni Chales Mwakipesile,Brand Nelson,Felix Mwakyembe na Joseph Mwaisango inaelekea kuna kitu wanashangaa
Waziri wa uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake katika uwanja huo wa songwe amesema kuwa uwanja wa Songwe wa kimataifa ni kati ya viwanja vikubwa viwili kujengwa baada ya uhuru ukitanguliwa na uwanja wa Mkoa wa Kilimanjaro kwani viwanja vingine vimekuwa vikifanyiwa marekebisho 
Kikao
Picha na Mbeya yetu

No comments: