Sunday, December 2, 2012

Tanzania Red ribbon Fashion Gala 2012 yafana sana

 Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House na Muandaaji wa Onyesho la Mavazi la Tanzania Red ribbon Fashion Gala,Khadija Mwanamboka (kulia) akikabidhi cheti kwa Mwanamitindo Maarufu nchini,Flaviana Matata ambaye ni Muanzilishi wa taasisi ya kusaidia jamii iliyo kwenye matatizo ya Flaviana Matata Foundation,wakati wa kuadhimisha Miaka Mitano ya Onyesho la Mavazi la Tanzania Red Ribbon Fashion Gala ambalo hufanyika Desemba 1,kila mwaka ikiwa ni kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani,lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House na Muandaaji wa Onyesho la Mavazi la Tanzania Red ribbon Fashion Gala,Khadija Mwanamboka (kulia) akikabithi Cheti kwa Dada Halima Rashid.
Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House na Muandaaji wa Onyesho la Mavazi la Tanzania Red ribbon Fashion Gala,Khadija Mwanamboka (kulia) akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi wa Hoteli ya Giraffe,Dk. Charles Beccon.
Wanamitindo wakipita jukwaani kuonyesha mavazi mbali mbali yaliyobuniwa na Wabunifu wa hapa nchini.
Waendeshaji wa Onyesho hilo,Evans Bukuku (picha ya juu) na Abby wakionyesha nao umahiri wao wa kutembea jukwaani kwa mwendo wa kiuana Mitindo.

Mwanamitindo Maarufu nchini,Flaviana Matata (kushoto) ambaye ni Muanzilishi wa taasisi ya kusaidia jamii iliyo kwenye matatizo ya Flaviana Matata Foundation akiongoza mnada wa nguo walizozivaa kwa ajili ya kukusanya hela ya kusaidia wahitaji walio chini ya Taasisi hiyo,ambapo hadi mnada wa vitu mbali mbali unamalizika jumla ya shilingi Milioni 72 ziliweza kukusanywa hiyo jana.Kulia ni Mwanamitindo,Jenuffer Bash.
Wadau wakifatilia kwa Umakini Onyesho hilo.
Mdau Raqey pia ndani ya nyumba.
Wadau.
Wabunifu wa Mitindo maarufu hapa nchini,Khadija Mwanamboka na Asia Idarous wakiwa na furaha ya kutosha kutokana na ufanisi mzuri wa kazi zao.
........... pamoja na Hawa ndani ya nyumba.
Mboni Masimba a.k.a Mamaa wa Mboni Show.
Mdau Jahhu Mohamed Kessy.
kila goti litapigwa ukiwa kazili,bila kujali umevaa nguo gani.
Kila aliefika ukumbini hapo alikuwa amependeza sana.
Mnada ukiendelea kufanyika.
Wadau kutoka TBL.
Nguo za kiume zilizonadishwa hapo zilienda kwa Mohamed Dewji Foundation.
Mdau Luca wa Bongo5 akiwa na Masap wake,Nancy Sumari.
Wabunifu wa Mitindo wakicheki mambo yao.
Watu kibao walihudhulia Onyesho hilo.
Mkurugenzi wa Hoteli ya Giraffe,Dk. Charles Beccon (kulia).
Wapiganaji katika sekta ya Picha wakiwakilisha ndani ya Red Ribbon Fashion Gala.
Wadau wa MO Blog.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe akiwa na Madam Ritha Paulsen,Maria Sarungi na Mwanamuziki Mkonge nchini,Lady Jay Dee wakati wa Onyesho la Mavazi la Red Ribbon Fashion Gala lililofanyika kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam.
Mnada wa nguo.
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe akienda sambamba na Msanii Linex wakati wakiimba wimbo wa Leka Dutigite ulioimbwa na Wasanii mbali mbali wanaotokea Mkoani Kigoma.
Mh. Zitto Kabwe akiflow na mistari kadhaa ya Wimbo wa Leka Dutigite.(Daahhh......!! kumbe Mh. nae yuko fitiiiiii.....!!)
Mh. Zitto Kabwe pamoja na mshabiki wake aliepanda jukwaani kuimba nae wakiaga mara baada ya kumalizika kwa Onyesho hilo. 
Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House na Muandaaji wa Onyesho la Mavazi la Tanzania Red ribbon Fashion Gala,Khadija Mwanamboka (kushoto) akiwa kwenye picha ya Pamoja na Mameneja wa Vinywaji kutoka TBL(Victoria Kimaro [wa pili kushoto] na Pamela Kikuli [Ndovu/Castle Lite]) pamoja na Mwanalibeneke Othman Michuzi.
Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House na Muandaaji wa Onyesho la Mavazi la Tanzania Red ribbon Fashion Gala,Khadija Mwanamboka (kulia) akiwa na Mbunifu wa mitindo Mustafa Hassanali (pili kushoto),Miss World Africa 2005,Nancy Sumari alieambatana na wa ubani wake Luca.
Ahmad Michuzi (kushoto) na Othman Michuzi wakiwa na Keki yenye mchoro wa Utepe Mwekundu.
Othman Michuzi na Shamim Mwasha wa 8020Fashions.
wengine kule,wengine huku.
Othman Michuzi na Zeinul Mzige wa Mo Blog.
Kutoka Kulia ni Flaviana Matata,Othman Michizi,Mamaa wa Mitindo Asia Idarous na Shamim Mwasha wa 8020Fashions Blog.

No comments: