Dar es Salaam Desemba 18, 2012 … Kufuatia changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa taarifa muhimu za hali ya hewa nchini, sasa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na kampuni ya Vodacom Tanzania zimefanikisha kuwawezesha watanzania kuweza kupata taarifa muhimu za hali ya hewa kwa njia ya haraka zaidi na rahisi
Mfumo huu maalumu utawezesha upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa kupitia njia ya simu utasaidia kwa kiasi kikubwa na kutoa nafasi ya wahusika kuchukua tahadhari pale inapobidi na pia kuweza umma kupanga shughuli zao za kila siku.
Akizungumzia mpango huo mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dr.Agnes Kijazi, amesema kuwa Mamlaka hiyo inajitahidi kadri inavyoweza kutumia fursa za kiteknolojia zilizopo ili kuweza kuhakikisha kuwa watanzania wanapata taarifa za hali ya hewa za mara kwa mara pale wanapohitaji.,
“Nchi yetu ni kubwa sana na maeneo mengi yanatofautiana kwa hali ya hewa, wakati mwingine nyenzo zinazotumika kutoa taarifa ya hali ya hewa haziwafikii watu wote pale wanapokuwa, njia ya simu ni bora zaidi kwani watu wengi wanatumia simu hivyo ni rahisi pia taarifa hizi kuwafikia watu wengi zaidi, alisema Dr. Kijazi na kuongeza kuwa kuna watu ambao wanasafiri kwa njia ya maji na anga ni muhimu sana watu hawa kupata taarifa hizi za kabla ya kusafiri ili waweze kuchukua tahadhari. itakuwa ni jambo jema sasa watanzania kupata taarifa hizi muda wote wanapo hitaji,” alisema Dr. Kijazi
“Tunayo fursa nzuri ya kutumia maendeleo ya teknolojia kuhakikisha kuwa tunawapatia watanzania uwezo wa kupata taarifa hizi za msingi,”
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa amesema kuwa wanafuraha kuungana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania katika kuwapatia watanzania taarifa za hali ya hewa kupitia njia ya simu, ikumbukwe pia TMA ndio chombo kilichopewa Mamlaka ya kutoa taarifa za hali ya hewa nchini.
“Sekta ya mawasiliano ya simu imekuwa kwa kiasi kikubwa sana kila mtu anahitaji kuwa na mawasiliano ya simu changamoto ya upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa sasa itakuwa imetatuliwa kwa kiasi kikubwa,” alisema Twissa na kuongeza kuwa, Vodacom tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufikia wateja wengi zaidi kutokana miundombinu tuliyonayo. Tunatumia mitambo yenye teknolojia ya juu na ninaamini kuwa katika maendelea ya kiteknolojia Vodacom tumefanikiwa sana,” alisema Twissa.
“Sasa tumeweza kuwafikia hadi wakazi wa kisiwa cha Gozba kisiwa ambacho kwa muda mrefu kimekuwa hakina mawasiliano, wakazi wengi wa eneo hilo wanajihushisha na shughuli za uvuvi kwa kuwawezesha wao kupata taarifa za hali ya hewa kwa njia ya simu kutawasaidia sana.
“Wateja wa Vodacom sasa wanaweza kupata taarifa hizi kwa njia rahisi sana kwa kuandika neno Wthr na Mkoa anaotoka na kisha kutuma kwenda 15588, Mfano mteja atatakiwa kuandika Neno Wthr Dar alafu watume kwenda 15588. Na hapo watapokea ujumbe wa kukubaliwa kuunganishwa na huduma na kuanza kupokea ujumbe wenye taarifa za hali ya hewa na kutozwa shilingi 100 kwa kila ujumbe.
Alihitimisha Twissa kwa kuwasihi watanzania kutumia fursa hii kupata taarifa za hali ya hewa na kujijengea utamaduni wa kutafuta na kupata taarifa hizo ili kuwa na tahadhari endapo kuna tatizo lolote linaweza kujitokeza
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji, Starfish Mobile East Africa Limited, Rashma Bharmal Shariff, amesema kwa sasa teknolojia inayo mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na teknolojia ya simu inaendelea kurahisisha mawasiliano kwa kufanya yawe yanapatikana kila sehemu na kwa gharama nafuu.
Amesema kuwa mikakati ya ushirika maridhawa, kama ushirika ulioundwa na TMA, Vodacom Tanzania na Starfish Mobile, habari za uhakika zinaweza kupatikana kwa urahisi na kwa haraka zaidi. Kwa mfano, wakulima wataweza kupata taarifa za hali ya hewa, jambo ambalo ni muhimu ili kupata matokeo mazuri katika shughuli zao za kilimo.
Kwa ujumla, taarifa za hali ya hewa zitamsaidia mtu kuweza kupanga jinsi ya kulinda rasilimali zake - iwe ni mkulima, mmiliki wa nyumba au hata mtalii.
Mwisho
Kuhusu Vodacom Tanzania:
Kampuni ya Vodacom Tanzania Limited ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na jamii katika shughuli za maendeleo kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation. Vodacom Foundation ina nguzo kuu tatu: Afya, Elimu na Ustawi wa Jamii. Hadi sasa taasisi hiyo imechangia zaidi ya miradi 120 ya kijamii nchini. Aidha, imeshinda tuzo mbalimbali za kitaifa na za kimataifa katika nyanja ya Uwajibikaji wa Mashirika kwa Jamii. Hizi ni pamoja na East African CSR Awards na Diversion and Inclusion Award ambayo hutolewa na kampuni mama ya Vodafone .
Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania inayotumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano. Vodacom Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South Afritca, ambayo pia ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) Limited inamiliki hisa ailimia 65 Vodacom Tanzania na asilimia 35 zilizobaki zinamilikiwa na Mirambo Ltd.
Vodacom Tanzania imetangazwa kuwa Super Brand (Chapa Bora Zaidi) kwa miaka mitatu mfululizo, kutoka 2009 -2011.
Kwa mawasiliano:
Matina G. Nkurlu
Meneja Mahusiano
Vodacom Tanzania Limited.
Mlimani City Jengo namba 1. Ghorofa ya kwanza.
Simu namba: 0754 710 099
Kwa taarifa zaidi kuhusu kazi za Vodafone Foundation, Tembelea.
No comments:
Post a Comment