Friday, December 7, 2012

KRFA yampinga Rais wa TFF,Leodegar Tenga

CHAMA cha Soka mkoa wa Kagera (KRFA), kimempinga Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga na kamati yake ya utendaji kwa kupinga mchakato wa marekebisho ya Katiba ya shirikisho hilo.

 Mwenyekiti wa KRFA, Jamali Malinzi amesema kuwa katika kikao cha kamati yake ya utendaji kilichoketi Desemba Mosi mjini Bukoba wamekubaliana kutoshiriki mchakato wa marekebisho hayo ya katiba yanayoendeshwa kwa njia ya waraka na kudai kuwa ni batili.

 "Mchakato wa TFF wa kubadili katiba ya TFF kama ulivyoanishwa katika warakata wa TFF kwa vyama wanachama wake ni batili kwa kuwa haukidhi matakwa ya katiba ya TFF kifungu cha 22 (1). Kifungu hicho cha 22 kinasema kuwa mkutano mkuu wa TFF ndio pekee wenye mamlaka ya kubadili katiba ya TFF, aidha kifungu kidogo cha 30 1-6 kinaeleza taratibu nzima ya mchakato wa kubadili katiba ikiwa ni pamoja na kutoa notisi ya siku 45, kuitisha mkutano mkuu na kupigak ura na wajumbe theluthi mbili kuridhia. 

"Hakuna mahali popote kwenye katiba ya TFF panapotamka kuwa katiba ya TFF itabadilishwa kwa wanachama kuzungushiwa waraka kupiga kura na kuandika jina na saini na kisha kuituma kura makao makuu ya TFF sisi kama KRFA hatutashiriki.

"alisisitiza Malinzi Mapema wiki hii Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisikika akisistiza kuwa mchakato huo wa kubadili Katiba ya TFF kwa njia ya waraka uendelee kufanyika kwasababu shirikisho hilo hivi sasa halina pesa za kuitisha mkutano mkuu kwa ajili ya zoezi hilo na kuwataka wanachama wake kukubaliana na njia hiyo.

 "Tunataka katiba yetu ilindwe na iheshimiwe na watu wote mana katiba ndio muongozo mkuu wa vipi mpira uendeshwe nchini mwetu, Katiba ya TFF ndio iliyomuweka Tenga madarakani pamoja na kamati yake ya utendaji, katiba inatutawala wote hakuna aliye juu ya katiba.

" alisema Malinzi alionyesha kushangazwa na kauli ya TFF kudai kuwa ufinyu wa bajeti kuwa ni kikwanzo kikuu kinachozuia mkutano mkuu wa kubadili katiba usifanyike. "TFF bila kujali kama vyama vya mikoa vina pesa au la ilitoa ratiba ya chaguzi za mikoa na kusisitiza ifuatwe, TFF haikutoa hata shilingi moja kusaidia zoezi hili, iweje wao washindwe kama mikoa inayojiendesha bila vyanzo vyovyote vya mapato iliweza sababu hii haina matinki.

"alisema kwa kuhoji Alisema TFF inatakiwa kuitisha mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba ya shirikisho hilo kwa faida ya soka la Tanzania ikiwa ni pamoja na kuepukana na marumbano mbalimbli yanayoweza kujitokeza endapo litakiuka taratibu.

 Katika hatua nyingine, Malinzi alisema kitendo cha kuwambia kipengele cha club licencing kisipoingizwa kwenye katiba ya TFF basi vilabu vya Simba na Azam vitazuiwa kushiriki michuano ya CAF mwakani ni kichekesho kwa kuwa TFF taarifa ya kutakiwa kuingizwa kipengele hicho walikuwa nazo mapema toka mwaka 2006 kwenye mkutano wa Fifa uliofanyika Berlin, Ujerumani mwaka huo na kusainiwa na Rais wa Fifa Sepp Blatter Oktoba 29 mwaka 2007 na agizo hilo lilisisitizwa iwapo kipengele hicho hakitaingizwa klabu hazitaruhusiwa kushiriki michuano ya CAF na Fifa.

 "Tenga ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya CAF baada ya kupokea waraka wa FIFA kuhusu suala hili alikaa na kutoa ratiba ya mchakato wa utekelezaji wa agizo hilo, ratiba ilionyesha hadi Desemba 2011 kila nchi mwanachama wa CAF ilitakiwa iwe imeingiza, siku saba zimesalia tangu amalize muda wake wa uongozi Desemba 14 tunambiwa Simba na Azam tusipotisha kipengele hiki hazitashiriki. 

"Mwezi April mwaka huu TFF ilifanya mkutano wake mbona hawakukiweka kipengele hiki kama ajenda?"alihoji na kusema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 4.5.1. kwenye waraka wa FIFA kinaruhusu nchi wanachama kuombea kibali klabu zake na kuitaka TFF kufanya hivyo kwa kuziombea kibali cha kushiriki michuano ya CAF mwakani timu za Simba na Azam.

1 comment:

Anonymous said...

Ishu ya club licencing inahitaji maandalizi,namuunga mkono malinzi,tuombe kupewa muda wa kujipanga.Na kwa nini Tenga avunje katiba,asijivunjie heshima.