Wednesday, October 17, 2012

WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAKUTANA NA MKURUGENZI MTENGDAJI WA VODACOM TANZANIA


Vodacom kuwekeza zaidi kwa jamii
·        Yatenga Bil 2.5 kufadhili miradi ya huduma za jamii 2012/2013
·        Kunufaisha Elimu, Afya, Mazingira na Uwezeshaji kiuchumi wanawake
·        M-pesa kuzidi kuwa huduma bora
·        Mkongo wa Taifa kuboresha huduma za mawasiliano
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom imesema itaendelea kutoa kipaumbele katika kusaidia huduma za jamii nchini kama shemu ya dira ya biashara ya kampuni hiyo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw Rene Meza alipokutana na Wahariri Wakuu wa vyombo vya habari nchini jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kuzungumza  na wakuu hao wa vyumba vya habari kwa lengo la kuzungumzia shughuli za Vodacom hapa nchini.
Amesema katika kuendeleza azma hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania kwa mwaka huu wa fedha imetenga shilingi bilioni mbili na nusu kufadhili miradi mbalimbali ya kijamii katika maeno makuu manne elimu,afya, mazingira na uwezeshaji kiuchumi wanawake.
Rene amesema mafanikio ya kibishara ya Vodacom hupimwa sanjari na namna inavyowekeza katika jamii kupitia kitengo chake cha Vodacom Foundation jambo ambalo linaifanya kambpuni hiyo kuwa karibu zaidi na jamii.
Amesema mafanikio ya uwekezaji wake katika jamii – CSR yameonesha mafanikio makubwa kupitia miradi mbalimbali ukiwemo wa fistula ambao umeleta staha na faraja kwa wanawake waliokuwa wakisumbumuliwa na tatizo hilo na mradi wa MWEI.
Akizungumzia huduma ya M-pesa Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema Vodacom itaendelea kuwa makini kuhakikisha mfumo wa huduma hiyo unaendelea kuwa imara na wa kuaminika sokoni ikitambua nafasi iliyonayo katika kupunguza tatizo la upatiakanji wa huduma za kibenki nchini.
Rene amesema ni jambo la wazi kwamba huduma ya M-pesa imekuwa nguzo muhimu katika maisha ya watu kwa sasa ikitoa urahisi wa kutuma na kupokea fedha wakati wowote mahali popote hapa nchini kuzindi hata kupitia mifumo ya kibenki.
Miamala yenye thamani ya kiasi cha shilingi bilioni moja hupita katika mfumo wa M-pesa kwa siku kutuma na  kupokea pesa pamoja na kufanya malipo mbalimbali. 
Kuhusu huduma za mawasiliano Rene amewaeleza wahariri kwamba kampuni hiyo kupitia mpango wake wa kuporesha na kupanua upatikanaji wa huduma itakamilisha mpango wa kujiunga na mkongo wa taifa kwa sehemu kubwa ya nchi ifikapo Mei mwakani.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa jukwaa la Wahariri nchini Bw Absalom Kibanda alisema uamuzi wa Rene kukutana na wahariri kila mwaka unajenga imani na ukaribu kati ya kampuni hiyo na vyombo vya habari tofauti na wakuu wengi wa makampuni binafsi ambao hawana utamaduni wa kudumu wa aina hiyo.
Rene aliyejiunga na Vodacom Tanzania Oktoba mwaka jana alikutana kwa mara ya kwanza na Wahariri Wakuu wa Habari Novemba mwaka jana ambapo aliwaelezea dira na mikakati yake ya kuhakikisha Vodacom inaendelea kuongoza soko la huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini.

No comments: