Balozi
Dora Msechu akichangia majadiliano kuhusu ajenda ya uwezeshaji wa
wanawake wakati wa mkutano wa Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la 67 la
Umoja wa Mataifa, katika mchango wake, Balozi Dora Msechu alizungumzia
juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kukomboa mwanamke na
mtoto wa kike dhidi ya vitendo vya kikatili, unyanyasaji na ukosefu
wa huduma za kuridhisha za huduma ya afya ya mama mjamzito. Aidha
katika mchango wake, Balozi Msechu amesisitiza haki na fursa ya
wanawake kushiriki katika majadiliano ya kutafuta amani ili kuifanya
dunia kuwa mahali salama.
Rais
wa Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa, Bw. Vuc Jeremic ambaye
ameahidi kufanya kazi kwa Karibu na Kamati ya Tatu ya Baraza hilo
inayohusika na masuala ya Maendeleo ya Jamii, Haki za Binadamu na
Utamaduni katika kusukuma mbele ajenda zinazohusu maendeleo ya
wanawake, fursa sawa za kijinsia na uwezeshaji.
Na Mwandishi Maalum
Wakati
Rais wa Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa, Bw Vuc Jeremic
akisisitiza haki za wanawake kama nguzo muhimu katika kufikia usawa wa
kijinsia. Tanzania kwa upande wake imesisitiza haja na umuhimu wa
wanawake kushirikia katika majadiliano ya kutafua amani ili kuifanya
dunia kuwa mahali salama.
Akihutubia
kwa mara ya kwanza Kamati ya Tatu ya Baraza hilo inayojihusisha na
masuala ya, pamoja na mambo mengine maendeleo ya jamii, haki za binadamu
na utamaduni. Bw. Jeramic ameahidi kufanya kazi kwa karibu na
kamati hiyo katika kutetea maslahi yanayolenga kumuinua na kumuendeleza
mwanamke katika nyaja zote.
Kwa
siku mbili mfululuzo wajumbe wakati hiyo wamekuwa wakijadiliana na
kubadiliana mawazo kuhusu ajenda inayohusua maendeleo ya wanawake, huku
wakipokea taarifa mbalimbali kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki Moon na Wakuu wa Mashirika yaliyochini ya Umoja huo.
Rais
wa Baraza kuu la 67 la UM akatumia fursa hiyo pia kuwahimiza wajumbe
wa Kamati hiyo kufanya kazi kwa karibu na Baraza la Uchumi na Fedha (
ECOSOC) katika masuala mtambuka ambayo yanahusu maendeleo ya wanawake.
Akasema
Kamati hiyo ni muhumi sana katika kushughulikia masuala ya haki za
binadamu zikiwamo za wanawake na ndiyo maana aliamua kwenda kuzungumza
na kamati hiyo kuihakikishia utayari wake wa kushirikiano nao katika
mwaka huu wa urais wake.
Baadhi
ya mambo muhimu yaliyojadiliwa na wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na
kuendelea kwa hali ya unyanyasaji na ubaguzi dhidi ya wanawake,
kuendelea kwa vitendo vya ukatili dhidi yao kama vile ubakaji, kuendelea
kwa tohara za wanawake na ukosekanaji wa fursa mbalimbali za kujiamulia
mambo yao wenyewe zikiwamo fursa za uchumi, elimu, ajira na huduma
bora na kuridhisha za uzazi salama na biashara haramu ya binadamu.
Akichangia
majadiliano hayo, msemaji wa Tanzania katika Mkutano huo Balozi Dora
Msechu alisisitiza pamoja na mambo mengine kwamba, haki za mwanamke ni
pamoja na haki ya kushiriki katika majadiliano na michakato ya
kutafuta amani ili kuifanya dunia kuwa mahali salama zaidi.
Balozi
Msechu akasema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kwamba fursa
sawa kwa wanawake na watoto wa kike ni haki ya msingi. Na kwamba
wanawake wakielimishwa na kuwezeshwa wanaouweza mkubwa wa kuendesha
uchumi na kuimarisha jamii katika ujumla wake.
Akasema
kwa kutambua mchango wa wanawake katika utafutaji wa amani na kubwa
zaidi katika kukuza uchumi na maendeleo ya jamii, serikali imetoa
kipaumbele cha pekee katika ajenda ya usawa wa kijinsi na uwezeshaji wa
wanawake.
Akaeleza
pia juhudi mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika katika kukomesha
aina zote za unyanyasaji na maovu dhidi ya wanawake na kwamba juhudi
zimekuwa zikifanyika za kurekebisha baadhi ya sheria zikawamo za ndoa na
mirathi ili kuondoa vipengele vinavyomkandamiza mwanake.
Kwa
upande wa changamoto, Balozi Dora Msechu amezitaja chanagamoto hizo ni
pamoja na ukosefu wa huduma za uhakika za afya ya mama wajawazito na
kwamba hali hiyo imesababisha kuendelea kupotea kwa maisha wa wanawake
na watoto wachanganga chini ya miaka mitano.
No comments:
Post a Comment