Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa,David Shambwe (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua
rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Mindu,Upanga jijini Dar
es Salaam.Wengine pichani toka kulia ni Meneja Mahusiano ya Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa,Muungano Saguya,Meneja
Masoko na Utafiti wa Shirika la Nyumba la Taifa,Itandula
Gambalagi na mwisho ni Meneja
wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Upanga,Benedict Kilimba.
Meneja
Masoko
na Utafiti wa Shirika la Nyumba la Taifa,Itandula
Gambalagi akiwaonyesha baadhi ya Waandishi wa Habari sehemu ya Mradi wa
Jengo Jipya lililopo Mtaa wa Mindu,Upanga jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa,David Shambwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kutembelea mradi wake mpya wa Mindu,Upanga jijini Dar es Salaam.
Kwa
mara nyingine tena Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo 24 Oktoba, 2012
limezindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Mindu,
jijini Dar es Salaam.
Ujenzi
wa mradi huu ulianza rasmi mwezi Novemba mwaka 2011, na unatarajiwa
kukamilika rasmi Aprili 2013 na mteja kuweza kukabidhiwa nyumba yake
mwezi Mei 2013, ikiwa ni miezi 18 baada ya kuanza ujenzi.
Mradi unatarajiwa kugharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi bilioni 11 mpaka
utakapomalizika, fedha zinazogharamiwa na Shirika kutoka vyanzo
mbalimbali vya mapato ikiwemo fedha za mikopo ya benki.
Mradi
huu uliopo mtaa wa Mindu eneo la Upanga, takribani mita 100 kutoka
Hospitali Kuu ya Taifa Muhimbili, una sehemu ya nyumba 60 za kuuzwa
zilizopo kwenye majengo pacha ya ghorofa 15, uko sehemu zenye huduma
zote muhimu za kijamii zikiwamo hospitali, shule, maduka, na masoko.
Pia Mradi unatarajiwa kuboresha maisha ya wanunuzi wa nyumba hizi kwani
upo karibu kabisa na katikati ya jiji na kwamba mnunuzi anaweza kwenda
kazini bila kutumia gharama yoyote ya usafiri wa gari.
Aidha,
nyumba zipo ndani ya uzio kwa ajili ya usalama wa wakaazi wake na kuna
maegesho ya magari ya kutosha.
Nyumba 60 tu zinazouzwa ambapo kila nyumba ina vyumba vitatu vya kulala,
vyo vinajitegemea. Kila nyumba ina ukubwa wa mita za mraba 141 (sq.m),
sebule iliyoungana na eneo la kula chakula, choo cha umma, jiko kubwa la
kisasa na eneo la kufulia na kuanikia nguo.
Sifa
za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo maalum la kukusanyia taka, nyumba
zote zina viyoyozi, vifaa vya kung’amua moto, sehemu iliyotengwa maalum
kwa ajili ya kufanyia mazoezi (gym), bwawa la kuogelea (swimming pool)
na eneo kubwa la ziada la maegesho ya magari.
Kila
nyumba itauzwa kwa bei ya TZS 272,050,673.08 bila kodi ya ongezeko la
thamani (VAT ) na TZS 321,019,794.24 ikiwa na kodi ya ongezeko la
thamani (VAT).
Tunawahamasisha na kuwakaribisha watanzania wote walio nchini na nje ya
nchi kujitokeza ili kununua nyumba hizo.
Wanaweza
kufanya mawasiliano na Makao Makuu ya Shirika, Ofisi zetu za Mikoa au
kupitia barua pepe na kukamilisha taratibu mapema kwa ajili ya kuweza
kuingia kwenye mchakato ulio wazi wa manunuzi.
Katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba, Shirika linajenga nyumba
za gharama ya juu, kati na chini ili kuwahudumia watanzania wa kada
zote.
Katika
azma hiyo, nyumba 10,000 zitakazojengwa kufikia 2015 zitahusu watu wa
kipato cha juu na nyumba 5,000 zitakazojengwa kufikia mwaka huo zitakuwa
ni nyumba za watu wa kipato cha chini.
Shirika
limeanza kujenga nyumba za gharama ya kati na juu ili kupata faida
itakayoliwezesha kuwajengea watu wa kipato cha chini nyumba za gharama
nafuu. Hii inatokana na ukweli kuwa Shirika halipati ruzuku toka
serikalini ya kujenga nyumba kwa ajili ya wananchi wa kipato cha chini.
Mradi
huu wa Mindu tunaouzindua hii leo, ni moja ya miradi ya ujenzi wa
nyumba za watu wenye kipato cha juu..
Ukiwa mdau na mnunuzi mtarajiwa, ama una ndugu/rafiki anayetamani
kununua nyumba katika mradi huu, wasiliana na Kitengo cha Mauzo simu
namba 0754 444 333; barua pepe: sales@nhctz.com na pia tembelea tovuti
ya Shirika www.nhctz.com kwa maelezo zaidi.
Links:
Facebook: http://www.facebook.com/nhctz
No comments:
Post a Comment