Thursday, October 11, 2012

Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF waendelea kwa siku ya pili leo jijini Arusha

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PPF,Dk. Adolf Mkenda akitoa muongozo wa kikao mapema leo asubuhi ikiwa ni siku ya pili ya Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau PPF unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha.
 Mwenyekiti wa Kikao cha kwanza cha Mkutano wa Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau PPF,kilichokuwa kikihusu maswala ya Tehama katika sekta ya Hifadhi za Jamii,Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,Dk. Marina Njelekea akitoa muongozo kwa Wadau wa PPF waliopo kwenye mkutano huo.
Mtoa Mada iliyokuwa ikihusu maswala ya Tehama katika sekta ya Hifadhi za Jamii,Dk. Chaula Job Asheri akiwasilisha mada yake hiyo kwa Wanachana na Wadau PPF waliopo kwenye Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau PPF,unaendelea kufanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha leo.
Mchangia Mada iliyokuwa ikihusu maswala ya Tehama katika sekta ya Hifadhi za Jamii,Dk. Ernest Kitindi akifafanua maswala mbali mbali yahusuyo mada hilo iliyowasilishwa na Dk. Chaula Job Asheri katika Mkutano wa Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau PPF,unaendelea kufanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha leo.
Meneja Muendeshaji wa Hoteli ya Gold Crest ya jijini Mwanza,Deepak Rawat akizungumzia hoteli hiyo iliyojengwa na PPF.
Rachel Mwinchumu na Mwanae Ernest Mwinchumu wakitoa ushuhuda wao mbele ya Wanachana na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 22 wa Mwaka,juu ya PPF walivyoweza kumsaidia yeye na Mwanae anaesomeshwa na PPF katika Shule ya msingi ya St. Joseph Millenium (darasa la sita).PPF ambayo ni Mfuko pekee unaotoa fao la Elimu nchini endapo Mwanachama anapokuwa amefariki akiwa kwenye ajira.PPF imeweza kumsaidia Mama huyo pamoja na Mwanae baada Mumewe Kufariki Ghafla.
Mtoto Ernest Mwinchumu akitoa shukrani kwa PPF kwa kuweza kumsomesha yeye na kumsaidia mama yake.
Mtoa Mada ya pili katika Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wadau na Wanachama wa PPF,iliyokuwa ikihusu Mambo Muhimu yanayopaswa kufuatwa na wanachama wa PPF,Nicander Kileo akiwasilisha mada yake hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa PPF,David Mataka akichangia Mada katika Mkutano huo.
Wadau wa Mkutano huo wakiuliza Maswali.
Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri,Neville Meena akiuliza swali lililokuwa likihoji juu ya huduma za kifedha zinazoendeshwa na Makampuni ya simu za mikononi.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Ludovick Utouh (kushoto) akijadiliana jambo na Dk. Chaula Job Asheri.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF,William Erio akitoa taarifa wakati wa Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha leo.
Dk. Chaula Job Asheri akiwasilisha mada ihusuyo maswala ya Tehama katika sekta ya hifadhi za jamii.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PPF,Dk. Adolf Mkenda (kushoto),Mkurugenzi Mkuu wa PPF,William Erio na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Ludovick Utouh (kulia) wakiwa katika picha ya Pamoja na Rachel Mwinchumu na Mwanae Ernest Mwinchumu ambaye anasomeshwa na PPF kupitia Fao la Elimu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba,Nehemiah Mchechu (katikati) nae ni mmoja wa Wadau wa PPF wanaohudhulia Mkutano huo.
Wadau na Wanachama mbali mbali wa PPF wakifuatilia kwa makini Mada mbali mbali zitolewazo kwenye Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau PPF,unaendelea kufanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha leo.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa PPF wakipitia taarifa kwenye kompyuta.
Wahariri: Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima,Absalom Kibanda na Mhariri wa Gazeti la Uhuru,Jane Mihanji.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Ludovick Utouh (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa PPF,David Mataka wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Uhusiano wa PPF,Lulu Mengele.
Warembo wa PPF wakiwa kwenye Mkutano huo.

No comments: